Ukistaajabu ya Yuda Iskariote utaona ya Salum Ally, katibu wa uvccm-dsm! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukistaajabu ya Yuda Iskariote utaona ya Salum Ally, katibu wa uvccm-dsm!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donyongijape, Jan 31, 2011.

 1. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa wale wanaoijua story ya Yuda iskariote watakuwa wameanza ku-predict nini ninachotaka kukisema hapa. Jina la Salum Ally ni jipya kwa watu wengi nchini lakini ni jina maarufu sana miongoni mwa wanafunzi CKD (UDSM) hasa kwa mwaka huu wa masomo 2010/2011, pengine miongoni mwa wanafunzi wa sheria waliosoma 2007/2010 na baadhi ya waliokuwa wanaharakati chuoni katika miaka hiyo.

  Ninaomba niwafungue macho wana JF wote juu ya kijana huyu machachari na kilicho nyuma ya tamko zima la jana la uvccm.

  Kwa wale mliofuatilia mtafaruku wa kisiasa pale chuo kikuu hivi karibuni kuhusu kupindua serikali ya DARUSO mtanielewa zaidi, na wale ambao kwa bahati mbaya hawakuwahi kufuatilia nitajitahidi kuwaelewesha japo kidogo.

  Hivi karibuni UDSM kulikuwa na fukuto kubwa la mapinduzi liloongozwa na Salum Ally dhidi ya serikali inayoongozwa na Mathias Simon (KIPARA). Dai kubwa la mapinduzi haya yalikuwa ni kuiingizwa tena kwa DARUSO katika Shirikisho la Wanafunzi Tanzania (TAHLISO).

  Mtafaruku huu uliongozwa katika hisia kali zilizoibuliwa na Salum pamoja na kampani yake kwamba Kipara alikuwa akitumiwa na chama cha siasa, na chama hicho ni CCM. Wakijua kwamba wanafunzi wengi chuoni hapo wapo against na chama hicho hivyo wangeweza kuwachota kirahisi kutokana na kumhusisha kiongozi wao na chama hicho. TAHLISO ikawa chungu kwa Kipara, ambapo pia inasemekana yeye alishauriwa na wenzake ndani ya TAHLISO alipe deni la UDSM kwa miaka miwili na arudishe uanachama wa DARUSO aweze kugombea Uenyekiti kwani CCM ilikuwa imepandikiza mgombea na wana- TAHLISO hawakutaka kuongozwa na huyo ambaye ni Pandikizi la CCM. Serikali yake ikapinduliwa kwa hila,na baadaye kamati iliyoundwa na chuo ilimrudishia madaraka.

  Katika mchakato huu mzima, wanafunzi wengi walikuwa wamefichwa kitu kimoja nacho ni huyo SALUM ALLY, kiongozi wa mapinduzi. Bahati nzuri kwake, yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria na hivyo wale wote waliokuwa wakimjua kwa undani walikwishatoka shuleni.

  MGOMO WA MWAKA 2008,KUDAI 100%.

  Huu ulikuwa ni mgomo mkubwa pengine kuliko yote ya hivi karibuni kudai mkopo wa 100% kwa wanafunzi wote ambao ulisababisha takribani vyuo tisa kufungwa na serikali.

  Kwa UDSM, viongozi wa wanafunzi na wanaharakati miongoni mwao walikuwa ni David Silinde, Stephen Owawa,Odong Oduar, Machibya,'Aristotle',etc. Kipindi hiki ndicho ninachoanza kuwapa mwanga kuhusu Salum Ally, ambaye kwa hali ya kushangaza alikuwa kimya kama aliyemwagiwa kemikali aina ya Chloroform ambayo mtu akipigwa huwa anasinzia jumla, ijapokuwa alikuwa alikuwa mbunge. Hakushiriki hata kidogo,mpaka kwa masikio yangu kipindi kile niliwahi kuwasikia viongozi niliowataja hapo juu wakimshangaa, na mimi ninashangaa zaidi sasa, kwa nini kwenye suala la msingi kama lile hakushiriki?? Leo hii ndiyo anaona matatizo ya bodi na serikali yake??

  CONNECTION YAKE NA UVCCM..!

  Kama mtakumbuka vizuri, Odong Oduar kipindi anatimuliwa nchini kwenda kwao Uganda alikutwa na kadi ya UVCCM, kwa uhakika kabisa nawaambia kwamba kadi ile alipewa kwa ushawishi wa Ally ambaye inadaiwa mama yake ni mtu mkubwa ndani ya CCM, kwa hoja kwamba ili uishi vizuri 'bongo' kuwa na kadi ya UVCCM/CCM. Maskini Odong kwa kutokujua kwamba anajichimbia kaburi kutokana na ushawishi wa mtu asiyemjua vyema (maybe intelingensia) akaingia mkenge, na yakampata yaliyompata.

  HITIMISHO..

  Mapinduzi ya hivi majuzi chuoni na tamko la jana ndiyo yamenifanya niamue kumlinganisha na yuda isariote mtu huyu. Jaribu kufikiri, wiki kadhaa zilizopita ulikuwa unamponda mwenzio kwamba anatumiwa na CCM, leo hii wewe unaibukia huko huko, tukueleweje??.

  Kama umenisoma awali, utagundua Ally alipandikizwa ili aweze kuipindua serikali ya daruso iliyopo ili CCM iweze kutawala UDSM na kuweka mikakati michafu na baada ya kushindwa.. Sasa wameamua kufanya nini?.

  Kwa Kutoa tamko kama lile la JPILI lakupinga na kuin'goa bodi ya mikopo na hapo hapo TAHLISO kutoa la kwao (Pengine ni planned), ni system ya divide and rule!. Kwa sasa wanafunzi wanalazimishwa kuamini kuwa ccm inawajali ili kuregain trust vyuoni.

  Hapo unaweza kuona kuwa yeyote atakayepinga, hasa hao waliowakorofishana nao awali na wakashindwa (DARUSO,TAHLISO na hata chama chochote cha siasa ), wataonekana ni wabaya kwa wanafunzi na hivyo wao ccm kugain popularity kwamba wanatetea wanafunzi.

  Ndipo ninapolazimika kuona matamko haya ni ya Kisiasa yenye malengo ya kuongeza mtaji wa ccm vyuoni na kwa vijana baada ya kukosa support kwa siku za hivi karibuni na mtu aliyeonekana kuwa anafaa kupenyeza propaganda hii ni huyu Salum Ally ambaye wanafunzi wa UDSM sasa wanamuona ni ndumila kuwili na mnafiki mkubwa.

  Ngoja tusubiri tuone wema huu mpya wa uvccm na serikali yake..Kwani ninaona wazi kuwa Hakuna cha bodi kuvunjwa wala nini, ni kiini macho tu..tulio macho tumeishaona..Nawe weka yako wazi uone!

  Wabbilah Tawfiq.
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  asante sana kwa taarifa hii muhimu.naomba ichapishwe gazetini ili abaki uchi.title ni "salumu ally ni nani?"
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Umeishaamini mara hii? leve this to DARUSO so many things happening there! mwambie aweke details jamani habari za ki-mwanahalisi cum shigongo sio nzuri kwa afya ya ubongo
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Wabilah Tawfiq, Asalam alleikum, Warahmatullah, Wabarakat!!

  Uko juu sana Sheikh, Maalim, Ustaadh, Maulamaa,

  Nimeipenda sana hii kitu mkuu.

  Mimi siku zote nasema hakuna kitu CCM na taasisi zao watasema nikawaaminini. Na mtu yeyote mwenye fikra kama zangu ataishi nchi hii kwa raha mustarehe. Maisha yanakuwa matamu pale unapokuwa na akili ambayo haichakachuliki kireja-reja kama yangu.
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  huamini kama Odong Odwar alikuwa anamiliki kadi ya CCM?

  unataka details gani mkuu?

  au ndo nyie wakati wa kunji mlikuwa mnaingia darasani?
   
 6. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  MH, ndio maan anilisema siku moja kua uchafu uliomo ndani ya CCm ni zaidi ya wa kwenye madampo
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  My friend I am not in any side, I fail to conclude or to agree with the conclusions of thread starter! my intelectual ability is failing to be conviced. What I mean is that there could be so many things hidden that we dont know, politics up there is so confusing!

  My dear I wave wasted one solid year at home because of Kunji! You have also concluded from no where!!!! no more words!
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Wamekuwa wakifanya hivyo kwa siku nyingi sana pale UDSM tumeona mengi na wengine tumesingiziwa mengi tulimuachia Mungu na sasa Siku zao zinahesabika kama sio miaka mitano ni mitatu.
   
 9. m

  mzambia JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kawaida sana hiyo kwa ud kuwa na ,mapindikizi ya ccm
   
Loading...