Ukistaajabu ya Serikali utayaona ya Bunge

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,681
1,109
Kumekuwa na sintofahamu zinazo ichanganya nchi katika kipindi hiki takribani Wiki sasa.

Mitandao ya jamii ime trend sakata la mheshimiwa Zitto kuandika barua ya kuzuia $ 500 millions,kwa maana ya kupinga matukio yanayo endelezwa na serikali, yanayo vunja misingi ya haki na usawa kwa raia na wananchi kwa ujumla wao.

Sakata la pili ni kutumbuliwa kwa mh. Kangi Lugola ambaye alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani, kwa kutumia madaraka yake vibaya kusaini mikataba ya kununua vifaa vya zimamoto bila idhini ya bunge wala serikali kuwa na taarifa.

Matukio yote, serikali na bunge yameyasimamia kwa pamoja.

Tukianza na Mh. Zitto Kabwe, serikali imemtuhumu kukosa uzalendo kwa kuzuia fedha hizo.

Lakini serikali haijaguswa na sababu za kuzuia fedha zisitolewe na Bank ya dunia ila imeumizwa na zuio la fedha.

Hapa kuna utata. Ikiwa nchi yetu imesaini mikataba ya dunia ya haki mbalimbali za binadamu ikiwamo elimu kutolewa bila upendeleo, iweje serikali iumizwe na uzuiaji wa fedha hiyo, badala ya kuitazama sheria hiyo kama ina mapungufu na ina kiuka haki hizo.

Mara ngapi rais amekuwa akizuia wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni, wasirudi shuleni, hali inayo ua ndoto za mabinti hao.

Lakini ni ukweli usiopingika matukio mengi yanayo wakumba mabinti zetu yanayo pelekea kushika mimba ni pamoja na mazingira magumu na hatarishi wanayo kumbana nayo watoto wa kike.

Mazingira ya kubakwa, kudanganywa kwa lengo la kusaidiwa masomo,offer za vyakula kutokana na hali ngumu za maisha majumbani kwao.

Serikali inajua hili na changamoto zinazo wakabili mabinti hawa, lakini hakuna sheria inayo wabeba wala kuwatetea, hali inayo sababisha mfumo dume unao athiri maisha ya mabinti hawa kisaikolojia.

Kwa kulitambua hilo unapokuja na hoja za kumfanya Zitto Kabwe kuwa msaliti kwa nchi, ni kujionyesha jinsi gani serikali isivyo juwa au tofautisha kati ya nchi na serikali.

Pili sababu zake nyingine ni ukandamizaji wa demikrasia nchini na ukiukwaji mkubwa wa misingi ya haki.

Watanzania wa kosoaji wa matendo ya utendaji mbovu wa serikali ni waathirika wa ukiukwaji haki hizo,zinazo kanyagwa na serikali, kwa serikali kuwashughulikia ipasavyo ikipingana na ibara 18 ya katiba inayo toa uhuru wa majadiliano.

Kwa msingi huo, Zitto Kabwe Mzalendo asiyeogopa,mbali na kuwakilisha kilio cha muda mrefu cha vyama vya siasa vya upinzani, anasimama pia kama icon ya wanyonge wa nchi hii wasio na sauti kutokana na hofu ya utawala huu, kwa kuwa ukisema una tengenezewa kesi, una tishwa na vikundi vya kihuni vinavyo pata media coverage kwa kujiita wanaharakati huru wanao mlinda rais na serikali yake.

Mbaya zaidi pamoja na katiba yetu kuzuia uundwaji wa jeshi na mamlaka hiyo imeanishwa kwa mujibu wa katiba, bado serikali imekaa kimya ikibariki kikundi hicho kinacho jinasibu kuwa kina jeshi kubwa litakalo washughulikia wakosoaji hao, kilitaja short list ambayo wengi waliotajwa wameshughulikiwa.

Ajabu bunge,chombo cha uwakilishi wa wananchi nacho kimeingia kwenye mtego wa ukiukwaji haki za kupata elimu kwa upendeleo kama nilivyo kwisha sema hapo juu.

Chombo hiki chenye mamlaka ya kutunga sheria kimeacha mipaka ya kazi na makujumu yake kwa mujibu wa sheria na kujifanya kuwa chombo cha serikali kinacho tumika kudhibiti wawakilishi wa wananchi kupaza sauti za wasio na sauti.

Hapo ndipo mshangao kwa spika kumtafutia jinai mbunge kwa kutumia nembo ya bunge, wakati mbunge huyo ni sehemu ya bunge kwa maana ya mwakilishi wa walipa kodi toka jimbo la Kigoma.

Bunge linaingia kwenye mgogoro na mwakilishi huyo usio na tija kwa maslahi ya Taifa.

Lakini spika ana shindwa kuelewa mwanasheria mkuu wa serikali si mwanasheria mkuu wa bunge, ukizingatia muktadha na maudhui ya mihimili hii miwili.

Kwa maagizo haya ya spika yanalifanya bunge kuonekana idara ya serikali na si mhimili unao jitegemea.

Kwa kuzingatia mantiki ya hoja ya Mh. Zitto una sababu ya kufanya hivyo.

Ikiwa maazimio ya bunge hayatekelezwi kwa mujibu wa sheria na kanuni za bunge, kwa nini isitumike njia ya kuwaadabisha serikali kwa kuzuia mikopo isiyo hata na baraka na bunge. Inayo sababisha deni la taifa kukuwa bila mpangilio!!!

Ni udhaifu mkubwa kwa chombo hiki ambacho kimekuwa kikitekeleza majukumu ya serikali na kuacha majukumu yake ya kibunge.

Sakata la pili ni utumbuliwaji wa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani.

Suala hili lina ukakasi mkubwa ukilichunguza kiundani, kwa kuwa chombo kinacho ibua miradi mbali mbali toka serikali kuu ni kikao cha Baraza la mawaziri, ambacho rais ni mwenyekiti wake.

Lakini pia anayetoa vibali vya kusafiri nje ya nchi ni rais pia kwa kujiridhisha na sababu zinazo sababisha Safari hizo.

Hebu tujiulize ilikuwaje haya yote yakatokea pomoja na kuwa na mlolongo mrefu unaopitia kwa rais. Kwa waziri na katibu mkuu wake pamoja na kiongozi wa jeshi la zimamoto kusaini mikataba ya kisheria bila idhini ya serikali wala mwanasheria mkuu kujua, wala kupata kibali cha safari ambacho hutolewa na ikulu!!!

Je huenda ikulu imekuwa si sehemu salama tena kwa watendaji wake kumzoea rais na kufikia hatua ya kutoa kibali bila ridhaa yake kwa maana ya kumzunguka rais!!!

Tumeshuhudia viongozi wengi hasa wa upinzani kuzuiliwa kwa Safari zao za kiserikali kama Mameya huko airport kwa kukosa kibali, ilikuwaje confirmation ya ujumbe wa wizara ya mambo kutokuzuiliwa ikiwa haukuwa na baraka za ikulu!!!

Kwa sakata hili la Kangi tuna la kujiuliza pia kabla ya kuhukumu hii double standard.

Sakata la Kangi na wenzake halina tofauti na watuhumiwa wa kesi za uhujumu uchumi, japokuwa ukamataji wao umetofautiana. Wakina Kabendera, Tito na wenzake kwanza walipotea ghafla, wakatafutwa vituo vyote hawakupatikana, Bandar ikasemekana walikamatwa na polisi hatimaye wakatuhumiwa watakatishaji fedha kwa maana ya wahujumu uchumi.

Sheria ya utakatishaji fedha au uhujumu uchumi kwa mujibu wa sheria zetu hauna dhamana.

Lakini kumekuwa na kilio cha wananchi kikitaka haki itendeke kwa watuhumiwa kuwa huru mpaka pale upepelezi utakapo kamilika, ndiyo wafikishwe mahakamani, kwa suala la Kangi na wenzake huenda taratibu zimeanza kutumika, na kama ndivyo hivyo kwanini sasa akina Kabendera na Ruge wasingie kwenye utaratibu huo au kuna matabaka ya ushughulikiaji watuhumiwa!!!!

Kwa hili nalo bunge limejitega tena, spika kaitaka kamati ya PAC ilitazame hili kwa kuwa huenda kuna udanganyifu mkubwa, lakini kuna tuhuma za ubadhirifu ambao ziliibuliwa na prof Asad wakati akihudumu kama CAG kuhusu ubadhirifu wa manunuzi ya nguo za askari wetu, japokuwa kwenye Hansard za bunge Mh. Kangi amemuita CAG muongo, bila bunge kumtaka kufuta kauli yake kwa kuwa kulikuwa na bifu kati ya CAG na Spika.

Leo kuitaka kamati inayo shughulika na fedha za umma PAC kuchunguza tuhuma hizi wakati bunge hili hili lilimwekea kifua waziri kuinanga taarifa ya CAG na CAG kulinaliweka bunge katika ipi!!!

Bunge kupinga hoja ya kuundwa kamati ya kuchunguza huku ikiamini kuna tuhuma za ubadhirifu haioni inajikanyaga yenyewe.

Na kwa kuwa PAC imekuwa ikifanya kazi bega kwa bega na ofisi ya CAG iliyo tuhumiwa ni waongo wakubwa, na kwa kuzingatia check and balance kwanini sasa bunge lisikubali kuunda kamati huru kama iliyo kuwa ya Mwakiyembe ili kupata ukweli wa tuhuma hizi.

Deal yeyote ni connection ,kwa kutumia kamati huru kila kitu kitakuwa wazi, ni vizuri sasa kwa kiti cha spika kulitazama hili kwa mapana na marefu.

Tulijadili kwa kina kwa maslahi mapana ya taifa letu. Mungu ibariki Tanzania.
 
Ni ujinga na siasa za hovyo, kwani awamu gani za uongozi watoto wa kike waliopata mimba waliendelea na shule? Huu ni utoto na ujinga
 
kwani ilani zilikuwa copy n paste hadi awamu zote zifanane

umeisoma ilani ya ccm 2015-2020 kuhusu ilo suala inasemaje

kama ujinga na siasa za hovyo ni kwa
aliye inadi iyo ilani na kuapa kuisimamia

utoto na ujinga uko kwa anaye itekeleza ilani na kukwepa baadhi ya vipengele
 
nimewasikia wabunge wakichangia suala la zitto yaani hadi huruma,uwezo wa kuchambua mambo uko chini sana. wote wanaimba zzk msaliti ashughulikiwe naamini ukimbana 1-1 aeleze usaliti wa zzk hakuna mwenye uwezo huo.

mwingine anasema zzk kaandika barua kwa niaba ya wabunge wote basi anapendekeza na wao waandike barua kumkana et hawajamtuma zzk unabaki unashangaa kule zimeenda hoja na mzungu kazielewa wala zzk hajasema katumwa kuwawakilisha.
 
Ukistaajabu ya Zitto Kabwe utauona na ujinga wake pia wa kufikilia:
Zitto Kabwe haelewi kitu kinachoitwa kichochea cha Kufanya kitu (Driving force): Kwa Mtoto wa kike kumruhusu kuendelea na masomo akiwa mjamzito ni uhalalishaji wa ndoa za utotoni na Mimba mashuleni, pia ni uhalalishaji wa Wanafunzi kuanza kufanya ngono wakiwa shuleni hali ambayo itawapelekea muda mwingi kufikilia kufanya Mapenzi na kuoana wakiwa Watoto badala ya kujidhatiti kwenye masomo yao kwa Maslahi yao na Taifa kwa ujumla, kuwasababisha Watoto wa kike kukosa haki yao ya Msingi ya kulelewa na Wazazi wao kama Watoto kwani nao wanajikuta ni Wazazi kwa mtoto/Watoto wao wakiwa bado wadogo, kutengeneza matishio mapya na makubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi mashuleni ambavyo vitaongezewa point kwenye causes of HIV is Zitto Kabwe attempt in 2020, Kuzigeuza shule zahanati na vituo vya kusomeshea Wazazi badala ya Watoto, kuwaathili kisaikolojia Watoto kutopenda masomo kutokana na kusoma na Wazazi wao na kutoithamini Elimu, Watoto kukosa muda wa kunyonyeshwa Wazazi wao wakiwa Darasani. Hata hiyo haki ya mtoto kunyonya Zitto Kabwe hakuiona si ni ujinga uliopitiliza.
Tukumbuke hao wanaomtumia Zitto Kabwe ndio haohao Wanaobuni kila siku cc tuwe chini kifikra na kiuchumi na wao wawe juu kifikra na kiuchumi.
Zitto Kabwe ametokea nchi za vita, na wanamfahamu kama siyo Mtz na hana machungu na Tanzania na kizazi cha Watanzania wala hana Miiko, maadili na Tamaduni za kitanzania, na wanajua akiwavuruga Watanzania papo pa yeye na Familia yake kuhifadhiwa.
Kwa minajili hiyo Zitto Kabwe acha tabia zako Mbaya na chafu za kutaka kutuharibia taratibu zetu kwa mpunga uliopewa. Wewe umeenda Taifa ambalo Dada na Kaka yake Wanashaea Bwana mmoja ambayo kwao ni haki, watu wanaotaka Watoto wa kiume Wafanyane kama wanavyokufanya wewe, nidhamu shuleni isiwepo kuathili ufundishaji wa Walimu.
Zigo ni mmoja wa Magonjwa Mapya ukiachana na Corona na Ebola
 
Muda wamabadiliko umefika na ifahamike kuwa wapinzani wameanza kucheza siasa za ngazi tofauti na CCM wakati wao wanaendelea kucheza siasa za karne ya zamani.

Mambo yalipofikia kwa sasa ni magumu na ukiona watu wazima na wenye akili timamu wanajikita kwenye hoja za kumjadili mtu badala ya hoja ujue wameishiwa hoja na ukistaajabu ya kunyimwa fedha na benki ya dunia utayaona ya mgodi Buzwagi nakama ilikuwa sakata la mgodi wa Buzwagi kumpaisha Zitto na upinzani ndivyo itakavyokuwa 500mil za benki ya dunia.

Sitanii kauli za Bulembo na Ngamia tena zilizo tolewa Bungeni ni hatari walitakiwa wasome alama za nyakati katika siasa za karne hii unatakiwa kujua kuusoma upepo na siyo kuburuzwa na mahaba kwa ajili ya mtu au kitu. Tulitakiwa kujiuliza haya: Je kuna hoja kwenye msimamo wa Zitto? Je na kama hakuna hoja mbona Washington imemuunga mkono kwa kutoa matamko mbalimbali tena katika kipindi kifupi?

Tanzania ni kubwa kuliko mtu mmoja au kikundi cha watu, wanaharakati huru au jeshi la kuwashughulikia "wasaliti". Kilicho bora kuliko yote ni maridhiano ya kitaifa. Jifungieni sehemu zungumzeni mazungumzo yata leta mwanga angavu kwa na kuleta mshikamano na umoja miongoni mwa vyama vya siasa.
 
Ukistaajabu ya Zitto Kabwe utauona na ujinga wake pia wa kufikilia:
Zitto Kabwe haelewi kitu kinachoitwa kichochea cha Kufanya kitu (Driving force): Kwa Mtoto wa kike kumruhusu kuendelea na masomo akiwa mjamzito ni uhalalishaji wa ndoa za utotoni na Mimba mashuleni, pia ni uhalalishaji wa Wanafunzi kuanza kufanya ngono wakiwa shuleni hali ambayo itawapelekea muda mwingi kufikilia kufanya Mapenzi na kuoana wakiwa Watoto badala ya kujidhatiti kwenye masomo yao kwa Maslahi yao na Taifa kwa ujumla, kuwasababisha Watoto wa kike kukosa haki yao ya Msingi ya kulelewa na Wazazi wao kama Watoto kwani nao wanajikuta ni Wazazi kwa mtoto/Watoto wao wakiwa bado wadogo, kutengeneza matishio mapya na makubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi mashuleni ambavyo vitaongezewa point kwenye causes of HIV is Zitto Kabwe attempt in 2020, Kuzigeuza shule zahanati na vituo vya kusomeshea Wazazi badala ya Watoto, kuwaathili kisaikolojia Watoto kutopenda masomo kutokana na kusoma na Wazazi wao na kutoithamini Elimu, Watoto kukosa muda wa kunyonyeshwa Wazazi wao wakiwa Darasani. Hata hiyo haki ya mtoto kunyonya Zitto Kabwe hakuiona si ni ujinga uliopitiliza.
Tukumbuke hao wanaomtumia Zitto Kabwe ndio haohao Wanaobuni kila siku cc tuwe chini kifikra na kiuchumi na wao wawe juu kifikra na kiuchumi.
Zitto Kabwe ametokea nchi za vita, na wanamfahamu kama siyo Mtz na hana machungu na Tanzania na kizazi cha Watanzania wala hana Miiko, maadili na Tamaduni za kitanzania, na wanajua akiwavuruga Watanzania papo pa yeye na Familia yake kuhifadhiwa.
Kwa minajili hiyo Zitto Kabwe acha tabia zako Mbaya na chafu za kutaka kutuharibia taratibu zetu kwa mpunga uliopewa. Wewe umeenda Taifa ambalo Dada na Kaka yake Wanashaea Bwana mmoja ambayo kwao ni haki, watu wanaotaka Watoto wa kiume Wafanyane kama wanavyokufanya wewe, nidhamu shuleni isiwepo kuathili ufundishaji wa Walimu.
Zigo ni mmoja wa Magonjwa Mapya ukiachana na Corona na Ebola
Sijui tunaishi dunia ipi? Je mmeshajiuliza kuhusu wanaopata mimba ya utotoni ni kina nani? Wanaishi katika maisha gani? Wazazi wao wana maisha gani? Maisha ya kujifunzia ya koje? Hawa watoto wakiitwa wazinifu ni halali? Je tunajua nani amewabesha mimba? Je wanaofanya hivyo siyo sawa wahujumu uchumi?
 
Zamani mzazi alimfukuza mwanae alopata mimba saa nyingine kupiga nusu kuua!! Hawa ndiyo ccm wanaofikiri kinguvu badala ya kufikiri kwa utulivu, wanafata 'mgawa cheo' anatakaje na wakotayari kudhalilika kisa kumtetea bwana wao,kwaajili ya kumfurahisha bwana wao watampinga hata muumba wao kama walivyosikika kutaka Muumba akishukuru kibwana chao..shame!!
Waliopata mimba wangesimamishwa masomo miaka 2 (kulea mimba miez 9 baadae mtoto naye mwaka) kisha warudi shule elimu nihaki ya msingi kwa KILA binadamu, mean while elimu itolewe kuzuia ngono/mimba/ukimwi mashuleni lkn sio kumnyima elimu maana nimtz na akikwama nchi inakwama!! Kesho watasema mwanafunzi mwenye ukimwi afukuzwe maana hawatalijenga taifa... Hawashangai mataifa mengine yanawatetea watoto wao yenyewe yanataka kuwaangamiza kwakujidai yako strict! Stupid nonsense
 
nimewasikia wabunge wakichangia suala la zitto yaani hadi huruma,uwezo wa kuchambua mambo uko chini sana. wote wanaimba zzk msaliti ashughulikiwe naamini ukimbana 1-1 aeleze usaliti wa zzk hakuna mwenye uwezo huo.

mwingine anasema zzk kaandika barua kwa niaba ya wabunge wote basi anapendekeza na wao waandike barua kumkana et hawajamtuma zzk unabaki unashangaa kule zimeenda hoja na mzungu kazielewa wala zzk hajasema katumwa kuwawakilisha.
Hapa unazungumzia wabunge wa bunge lipi? Rejea Prof Assad, Retired but not Tired CAG....maoni yake yako kwenye Hansard ya kamati kwamba yeye ataendelea kutumia neno "dhaifu" bila kepepesa macho.

Hatuna wabunge na bunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu lengo si kumnyima elimu....Mazingira yetu hayaruhusu kuruhusu mimba shuleni. Marekani mtoto analindwa kwa sheria kali ambapo kabla hujatongoza lazima uulize umri.. Bongo tunapima kwa vichuchu vikichomoza...sheria za ubakaji TZ hazina nguvu kutokana na baadhi ya makabila kubaka ndio njia ya kupata mchumba, ndoa za utotoni ruksa (tunaoa mimba), ... unaona walimu shule za msingi wanavyowakaanga vibinti.. na mzazi wa kijijini mtoto wake kabakwa anapewa laki 3 kesi kwishne...

Hatujafikia standard ya kumlinda mtoto.. japo kuna kifungo lakini many of unreported cases.

In a primitive way anaambiwa mtoto jichunge mwenyewe ukipata mimba shauri yako...

The moment tukiruhusu itakuwa wenye mimba wengi than wasio na mimba...

Naungana na kila anayetetea mabinti wenye mimba waendelee kusoma ila mazingira na standard zetu haziruhusu kuruhusu mimba shuleni...

Badala ya kutumia logic tunatumia sheria mbovu ili tubaki salama..
Zamani mzazi alimfukuza mwanae alopata mimba saa nyingine kupiga nusu kuua!! Hawa ndiyo ccm wanaofikiri kinguvu badala ya kufikiri kwa utulivu, wanafata 'mgawa cheo' anatakaje na wakotayari kudhalilika kisa kumtetea bwana wao...shame!!
Waliopata mimba wangesimamishwa masomo miaka 2 (kulea mimba miez 9 baadae mtoto naye mwaka) kisha warudi while elimu nihaki ya msingi kwakila binadamu,elimu itolewe kuzuia ngono/mimba/ukimwi mashuleni lkn sio kumnyima elimu maana nimtz na akikwama nchi inakwama!! Kesho watasema mwanafunzi mwenye ukimwi afukuzwe maana hawatalijenga taifa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom