BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Tangu lini mahakama ikapangiwa muda maalumu wa kumaliza kesi na siri kali!? 
Hapa si kuna ushahidi tosha kwamba siri kali inaingilia kazi za mahakama? Kwa jinsi Slaa anavyoendesha siri kali huko bungeni, siri kali itakubali hii kesi isisikilizwe tena? jibu tunalijua.
Je, gharama za kuanza upya kesi hii nani atazibeba? maana jury wanaweza kuwa wamesahau ushahidi uliotolewa na hivyo itabidi kuanza upya.
Kesi ya Slaa yaahirishwa
na Mustafa Leu
Tanzania Daima
KESI namba 20 ya mwaka 2005 iliyofunguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karatu, kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo, imeahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na muda uliokuwa umewekwa kusikiliza kesi hiyo kwisha kabla ya kesi kufikia ukingoni.
Akiahirisha kesi hiyo ambayo imekuwa ikiendelea katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa muda wa wiki nzima mfululizo kwa vipindi ya asubuhi na mchana, Jaji Robert Makaramba alisema kuwa, kesi hiyo kuendelea kusikilizwa au kutokuendelea kutategemea na uamuzi wa serikali ambayo itapanga utaratibu mwingine.
Kesi hiyo ilifunguliwa na wanachama watatu wa CCM wakipinga matokeo yaliyokipa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ushindi wa Jimbo la Karatu ambapo, Dk. Willbroad Slaa alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi kwa kumshinda mgombea ubunge wa CCM, Patrick Tsere ambaye baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Mawakili wa pande zote za walalamikaji, utetezi na serikali kwa pamoja walikubaliana na uamzi huo wa kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi taratibu nyingine zitakapopangwa.
Kesi hiyo ilichelewa kuanza kusikilizwa kutokana na walalamikaji kuchelewesha kuwasilisha vielelezo mahakamani katika muda uliokuwa umepangwa.
Hadi jana, alikuwa ni shahidi mmoja tu wa kwanza, Joseph Haim ndiye aliyekuwa akiendelea kutoa ushahidi wake wa kupinga matokeo kati ya mashahidi 25 wanaotarajiwa kutoa ushahidi wao.
Wakili wa utetezi, Tundu Lissu aliiambia mahakama hiyo kuwa, muda uliokuwa umepangiwa kesi hiyo umekwisha kutokana na upande wa walalamikaji kuchelewa kukamilisha vielelezo vyao.
Katika kesi hiyo, mshitakiwa wa kwanza ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wa pili ni Mbunge wa Karatu, Dk. Slaa, hivyo kesi hiyo iwapo itapangwa, lazima izingatie ratiba ya vikao vya Bunge.
Katika hatua nyingine, shahidi wa kwanza wa CCM, Haim alishukuru hatua ya mahakama hiyo ya kuahirisha kesi hiyo ili aweze kuishi huru kwani amekuwa chini ya kiapo tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa na hivyo kukosa amani na uhuru.
Hali hiyo imetokana na kutokukamilika mapema ushahidi wake ambao alikuwa akiutoa mahakamani na hatimaye kuonekana kuchoswa na maswali aliyokuwa akiulizwa mara kwa mara na mawakili kutokana na kukaa kizimbani kila siku asubuhi na mchana.