Ukistaajabu ya Mussa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukistaajabu ya Mussa...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 19, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,438
  Trophy Points: 280
  Date::11/19/2008
  Waziri asihi vyombo vya habari kuachana na habari za EPA, migomo ya walimu
  Festo Polea na Kuruthum Ahmed
  Mwananchi

  NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwamtumu Mahiza amevitaka vyombo vya habari nchini kuachana na habari zinazohusu sakata la wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje, (EPA) pamoja na masuala ya migomo ya walimu kwa madai kuwa masuala hayo tayari yametafutiwa ufumbuzi.

  Badala yake alivitaka vyombo hivyo kuelekeza nguvu hizo katika habari nyingine ikiwa ni pamoja na kufichua na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanafunzi.

  Waziri Mahiza alisema hayo jana wakati akizindua kampeni ya “Jifunze bila woga” iliyofadhiliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Plan-Tanzania yenye lengo la kupinga ukatili wa kijinsia mashuleni.

  Mahiza alisema anachukizwa kuana masuala ya EPA na migomo ya walimu ikishikiliwa bango kila kukicha wakati tayari malalamiko hayo yamefika mwisho kwa sababu walimu wameanza kulipwa na watuhumiwa wa EPA wameshafikishwa Mahakamani.

  “Sasa tubadilishe CD, kila wakati EPA na migomo ya walimu, waandishi wa habari na vyombo vya dola tubadilike, mimi nikiona mnalivalia njuga kwa kufichua masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, kuwafichua waharibifu wa wanafunzi, kisha wakakamatwa nitafurahi sana,” alisema Waziri Mahiza

  Mahiza alitumia nafasi hiyo kulaani walimu wote wanaoharibu watoto kijinsia kwa kutumia udhaifu wa wanafunzi wa kike na kiume kwa kuwarubuni kwa kuwapa vitu vinavyowashawishi kama Simu na magari.

  Alisema masuala ya ukatili wa kijinsia yanaongezeka licha ya kukemewa mara kwa mara.

  Aliwataka viongozi wa dini mbalimbali nchini kuandaa makongamano yenye lengo la kuombea laana walimu na watu wengine wanaorubuni wanafunzi bila kujali maisha yao ya baadae.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ipo haja ya kubadili CD... hakuna la kustaajabu hapo
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tukinyamaza, mawe yatapiga kelele. In fact CD ndiyo kwanza inaanza kukolea. Hapo EPA hakuna kunyamaza mpaka kieleweke halafu itafuata Meremeta, Deep Green, IPTL, Richmond, Kiwira, CIS, madai ya wastaafu EAC na .....haponi mtu.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,438
  Trophy Points: 280
  Habadili mtu CD mpaka kieleweke! Muziki ndiyo kwanza umeanza na waruka majoka wanaifurahia CD hiyo. DJ can you replay my favourate number EPA again and again and again!!! Ingekuwa mwaka 47 EPA ingeshasahaulika siku nyingi tu lakini hii ni 2008 mpaka kieleweke tumechoshwa na usanii usiokwisha.
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Yeye huyo waziri inamhusu nini jamani mbona anatafuta maswahiba yasiyomhusu????maana uozo wao huko wizarani wakae chonjo.......awe mpole na apime maneno yake asitafute cheap publicity
   
 6. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwamtumu Mahiza amevitaka vyombo vya habari nchini kuachana na habari zinazohusu sakata la wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje, (EPA) pamoja na masuala ya migomo ya walimu kwa madai kuwa masuala hayo tayari yametafutiwa ufumbuzi

  Mahiza alisema anachukizwa kuana masuala ya EPA na migomo ya walimu ikishikiliwa bango kila kukicha wakati tayari malalamiko hayo yamefika mwisho kwa sababu walimu wameanza kulipwa na watuhumiwa wa EPA wameshafikishwa Mahakamani.
   
 7. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mwantunu, hivi hujui watuhumiwa wa EPA kufikishwa mahakamani nayo ni habari?
   
 8. L

  Lorah JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  waambie mpaka tujue mwisho wake kama alitegemea mambo yameisha ndo kwanza unaanza na tukitoka tutarudisha richmond, meremata au kiwira mpaka 2010 ndo utaisha sasa hivi itakuwa EPA update si jui tuifungulie kabisa forum yange na magazeti watenge ukurasa ulioandikwa HABARI ZA UFISADI WA EPA na TV kipindi cha EPA hewani tutabeba mpaka kizazi cha saba
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Huyo Mama amenishangaza sana jana kwenye TV, nadhani ameingilia majukumu ya Wizara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii (Maendeleo ya Jamii). Sasa kama anataka Wanahabari wageuze CD kwenda kwenye masuala ya unyanyasaji, hiyo CD ikielekezwa huko Waziri Sitta naye akisema geuzeni CD andikeni kuhusu Migomo ya Walimu itakuwaje?

  Kwa kifupi ajue kuwa WaTanzania kwa sasa priority ni EPA, Elimu (Migomo ya Walimu na Wanafunzi) na baada ya hapo tutataka kujua kuhusu Meremeta, Tangold, Deep Green Finance na ubadhirifu mwingine. Ajue kuwa jukumu la kuandika habari ni la Wanahabari wenyewe na jukmu la habari ipi ipewe kipau mbele ni la Wahariri na Waziri.
   
 10. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2008
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mhamishiwa Waziri, napenda kukueleza kuwa hiyo CD upande mmoja haujaisha kwanini ugeuze wa pili? Wizi wa mitihani umesahau? Ujenzi wa shule nzuri karibu na watoto wanapotoka itasadia kutopenda masuala ya magari na lifti za vibopa. Hivi umeuleta kama mjadala, pendekezo au vipi.
   
 11. L

  Lorah JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tafadhali mpelekeeni ujumbe huu

  Tutaacha kuzungumzia EPA pale kesi itakapo isha kwani tuna experience tuliyoipata Richmond alipojiuzulu Lowasa tulimaliza na nyie mkatulia sinahabari imefikia wapi hope JK atatuambia mwisho wa mwaka kama atakuwa nchini
  na walimu mpaka alipwe mwalimu wa mwisho kwa sababu tumeyaona ya wazee wa East Africa.
  ya migomo ya chuo mpaka rais azungumze suala la vyuo vingi kufungwa kwa pamoja sio la kulivyalia suti na kwenda LIBYA km hakuna kitu ni swala la kuahirisha safari na kutuma ujumbe kuna emegency imetokea nchini kwangu sitaweza kuhudhuria kikao anyways ndo vijana wa siku hizi wazee wamelala mlangoni kwakwe yeye anapita na ving'ora kama ni takataka tu poor me...
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,963
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Mama Bakari Mahiza,nafikiri umekalia kuti la kuanguka,CD unazozisikia ni ule mlio wa kuti kuanza kumeguka na kuanguka.Waandishi wa habari ambao ni kioo cha jamii ndio wanatujulisha juu ya kuti bovu linalotaka kuanguka.Isije ikawa ajabu kuti hilo litakapomeguka kabisaa! maana CD yake tumeshaicheza.Kumeguka kimya kimya wataumia wengi zaidi maana wanao umia na huo wimbo wa EPA, Richmond n.k. wanajua nyimbo hizo walizitunga vipi.Endelea kucheza mama ,na kama wewe hazikuhusu basi kaa chini na wenyewe wenye CD hizo wataendelea kunengua, kama waandishi wetu na vyombo vya habari wanavyo koleza vibwagizo!!!!!
   
 13. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Ukistaajabu ya Musa ..... Utaona Jeetu Patel, i mean utaona ya Fi**uni huyu jitu patel
   
 14. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Ukistaajabu ya Musa ..... Utaona ya Jeetu Patel, i mean utaona ya Fi**uni huyu jitu patel
   
 15. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Ukistaajabu ya Musa ... Utaona ya Jeetu Pateli,,,, i mean utaona ya huuy Fi**uni jeetu patel
   
 16. BrownEye

  BrownEye Member

  #16
  Nov 20, 2008
  Joined: Jul 31, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  cd inayogusa wengi siku zote hupigwa sana au kijana umesahau? Hizo cd zinazogusa na kukandamiza walalahoi tu tumeshazichoka, hakuna anayevutiwa nazo.

  Sasa dhuluma basi ni kelele... Mpaka kieleweke!!!!
   
 17. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuna mwalimu wangu alinifundisha kuwa 'Unless we put meaning into it, a word has no meaning'. Akafafanua kidogo kuwa maana ya neno hutokana na jamii sio mtu fulani mfano waweza kuwa mwanaume kijinsia lakini jamii fulani inayotambua mwanaume aliepita jando isikutambuwe kuwa mwanaume.

  Hivyo basi jamii yawatanzania ndio inayojua ni kwa kiasi gani suara la EPA and ndugu zake limeshughurikiwa sio Mahiza? Hivyo awaachie wanahabali jamii ikiridhika automatically suala la EPA, etc litakuwa historia, hivyo namsihi awaache wadili nao. Kwani tatizo nini eti Mh, au na wewe upo nini?

  Suala la unyanyasaji kijinsia jamani wana JF tuliangalie kwa mapana kidogo. Sijafanya research lakini nimefanya observation kama mwanajamii. Kwa observation yangu unyanyasaji halisi nauona kwa vijana wa kiume kuliko wa kike. mtakubaliana na mimi vijana wa kike wengi wanajitegesha kwa tamaa zao na kukosa maadili. na swala hili hata baadhi ya mama zao wanachangia sana. Mimi naona hata uile sheria ya kumwadhibu mwanaume kwa kosa la kupeana mimba na msichana wa shule haiko sawa kwa sababu inawanyanyasa vijana wa viume kijinsia. Mi naona waadhibiwe wote sawa kabisa hii ndio suruhisho la kukomesha mimba mashuleni. Wasichana wengi wanao shika mimba mashuleni ni wale ambao CV zao hazijatulia katika masuala ya mahusiano. Na mara nyingi unakuta ni wasichana wa kuanzia kidato cha 2 - 4. Sasa jamani wana JF katika ulimwengu huu wa Dotcom. Msichana huyu wa Form 2 - 4 kwanini akubali kushika mimba na yeye ni mwanafunzi. Mbona wenzao kwenye nchi zilizoendelea wanakuwa na boyfriends na wanafanya mchezo mbaya kuanzia primary na hawashiki mimba???
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Huyo wazili si mlaumu ndio uwezo wake wa kufikilia.
  Ukiona ivyo kwenye ilo zengwe anaguswa indirectly.
  Tumelizwa billioni 133 unasema tubadili CD,hana ata haya
   
 19. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  “Sasa tubadilishe CD, kila wakati EPA na migomo ya walimu, waandishi wa habari na vyombo vya dola tubadilike,...................!!!!
   
 20. B

  BeNoir Member

  #20
  Nov 20, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh!! mama Mahiza mbona utakuwa na kazi kusimamia CD ipi ichezwe na ipi isichezwe!!
  Labda ujaribu kunzia kwenye hizo circle zenu muache ufisadi na viini macho, ndipo CD itabadilishwa.

  Kazi ipo. Ukimuamsha aliyelala............
   
Loading...