Ukistaajabu ya Musa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukistaajabu ya Musa...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 27, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ameifukua maiti ya mumewe toka kaburini kwasababu maiti hiyo ilizikwa huku mumewe akiwa amevalishwa meno ya bandia ambayo yalikuwa si ya kwake.Phyllis Manis hakutaka mumewe apumzike kaburini huku akiwa amevalishwa meno ya bandia ambayo si ya kwake.

  Phylis aliifukua maiti ya mumewe, Keneth iliyokuwa imezikwa kwenye makaburi ya Chattanooga, Tennessee ili aweze kumvalisha meno ya bandia aliyokuwa akivaa kila siku.

  Televisheni ya WTVC ya Marekani iliripoti kwamba, wakati Keneth alipokuwa amelazwa hospitali kwenye chumba cha watu mahututi, madaktari waliyachanganya meno yake ya bandia na meno ya bandia ya mtu mwingine hali iliyopelekea Keneth avalishwe meno ya bandia ya mtu mwingine.

  Baada ya mazishi ya Keneth ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 76, Phylis aligundua waleti na funguo za mgonjwa aliyekuwa amelazwa chumba kimoja na Keneth zikiwa zimechanganywa na baadhi ya vitu vya Keneth yakiwemo meno ya bandia aliyokuwa akiyavaa Keneth enzi za uhai wake.

  "Mume wangu amelala kaburini akiwa na meno ya bandia ya mtu mwingine, siwezi kuruhusu hali hii itokee kwani najua yeye mwenyewe asingependa iwe hivyo", alisema Phylis alipokuwa akihojiwa na televisheni ya WTVC.

  Msemaji wa hospitali ya Parkridge Medical Centre ambako tukio hilo lilitokea alisema kwamba hospitali inaomba radhi na imekubali kulipa gharama za kuifukua maiti ya Keneth pamoja na kumnunulia meno mapya mgonjwa ambaye meno yake ya bandia alivalishwa Keneth kimakosa.

  "Najua sasa mume wangu atapumzika vizuri na pia familia yetu itaweza kupumzika", alisema Phylis baaada ya maiti ya mumewe kufukuliwa ili kuvalishwa meno ya bandia aliyokuwa akiyavaa enzi za uhai wake.
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  hayo meno bila shaka yalikuwa ya mime mwenza, maana wanawake wqa siku hizi wengi ni kama Nazjaz na Faiza Foxy
   
 3. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  cjawai sikia híi.kweli kua uyaone
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Dunia haiishi vituko
   
 5. S

  Sweetlove Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je hyo ya iringa bibi kafariki na kuzikwa baba yake kamuuru maiti ifukuliwe kisa mume wake hakumalizia mahari enzi za ujana kwa hyo maiti ilizikwa tna baada ya mahari kumaliziwa.thats dunia and other stories.
   
 6. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Watu wana hela za kuchezea! Kibongo bongo inawezekana?
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,585
  Trophy Points: 280
  Inaonyesha ni jinsi gani mama anajali, si kwa uzima tu hadi kifo na baada ya kifo.
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Alitaka kupata umaarufu tu.
   
Loading...