Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Warda, achakachua kabla ya ndoa na kuleta aibu kubwa!

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
ndoa.jpg
Na Richard Bukos
Ndoa iliyokuwa ifungwe kati ya Bwanaharusi, Joseph Kibarabara na mkewe mtarajiwa, Warda Halfa, imetibuka kufuatia Bibiharusi huyo ‘kutekwa’ na kufungiwa chumbani na mwanaume anayedaiwa ni hawara yake wa zamani, Risasi Jumamosi linamwaga mambo hadharani.

Varangati hilo lilijiri Novemba 7, mwaka huu maeneo ya Ukonga, Dar baada ya aliyekuwa Bibiharusi mtarajiwa, Warda kuacha njia ya kuelekea kanisani kufanya mazoezi ya kufunga ndoa ‘riheso’ na mumewe mtarajiwa, Kibarabara na kumfuata mwanaume aliyedaiwa ni hawara yake aitwaye John Laurent.

MCHEZO ULIVYOANZA:
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, hawara huyo alimpigia simu Warda siku moja kabla ya ndoa na kumuuliza kama habari anazozisikia anaolewa ni za kweli.
“Laurent alimpigia simu Warda kumuuliza kama kweli anaolewa, akamjibu ndiyo, akamwomba aende nyumbani kwake ‘wakachakachue’ kwa mara ya mwisho, naye akakubali akaenda,” kilisema chanzo.

Chanzo kiliendelea kuweka wazi kwamba, wakati Warda anakwenda kwa mwanaume huyo, mumewe Kibarabara alishampigia simu akimtaka wakutane kanisani kwa ajili ya ‘riheso’, wito ambao mwanamke huyo aliupuuza.

Habari zinadai, baada ya Warda kufika kwa ‘jamaa’ yake wa zamani walichakachua kweli, lakini ghafla mwanaume huyo alimnyang’anya simu kisha akaizima na kutoa funguo kwenye kitasa cha mlango huku akimwambia ‘HAKUNA KUTOKA’ licha ya kwamba alikuwa akijua mwanamke huyo atafunga ndoa kesho yake saa tisa Alasiri.


Ikazidi kuelezwa na chanzo chetu kwamba, njemba huyo aliendelea kustarehe na mke mtarajiwa wa mwenzake hadi Jumapili saa kumi na moja Jioni alipomwachia wakati ndoa ilikuwa ifungwe saa 9 Alasiri katika Kanisa la Sabato Ukonga (SDA).

MBINU ZA KUUA SOO ZAFANYWA:
Baada ya kubaini kosa kubwa walilolifanya, hawara huyo alimchukua Warda hadi kwenye Zahanati moja maeneo ya Manzese, Dar na kudanganya kwa daktari kuwa, mwanamke huyo alianguka ghafla na kupoteza fahamu maeneo ya hayo hivyo kupatiwa matibabu ya dharura.

Baada ya hapo, Warda alirudi nyumbani kwao ambako alikuta ndugu, jamaa na marafiki wamevimba sura kwa hasira, wengine wakikaribia kutumbuka kama siyo kupasuka.

Wakati hayo yote yanafanyika, inasemekana Bwanaharusi ambaye tayari na ‘bestman’ wake walikuwa ndani ya suti mpya, alikuwa akiwakaba koo wazazi aliowalipa mahari akidai chake huku habari nyingine zikinyetisha kuwa, alishabonyezwa na wadaku kuhusu mchezo mzima wa Bibiharusi na jamaa yake wa zamani.

KAMATI KUU YA FAMILIA YAKETI KWA DHARURA:
Kufuatia tukio hilo la aibu chanzo kinadai, ndugu wa pande zote mbili waliketi kwa dharura nyumbani kwa shangazi wa Bibiharusi, Kimara Baruti, Dar ili kutafuta mwafaka na ndipo ghafla alitokea Warda akiwa amechoka ile mbaya.

Ndipo alipobanwa kisawasawa aeleze kinagaubaga nini kilitokea hadi

akaitumbukiza familia yake katika aibu kama ile, lakini wakati akimeza mate ili kujieleza, liliibuka varangati zito lililosababisha Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Magomeni ‘Mviringo’, Mokola Maulid aliyekuwa kwenye kikao hicho kama ndugu, kupigwa baada ya upande wa Bwanaharusi kupandwa na jazba.

Kufuatia tafrani hiyo kuchukua muda mrefu huku wanandugu wa pande zote wakiwa na hasira, hasa mawifi, watu wenye hekima walishauri kwenda Polisi Kituo cha Mbezi Luisi, Dar ambako ukweli utabainika.

Safari ilianza mpaka Kituo cha polisi na kupokelewa na maafande wenye sifa zote katika mambo ya sheria na ulinzi wa raia huku wakiweka sawa kitabu kikubwa cha ‘kaunta’ kwa ajili ya kuchukua maelezo ya pande zote mbili.
BIBIHARUSI NA AFANDE MASAITOO:

Akielezea mkasa huo mbele ya Sajenti Masaitoo wa kituo hicho cha Polisi, Biharusi ambaye sherehe ya kumuaga ‘Send Off’ ilikuwa ya kukata na shoka ilifanyika Alhamisi ya Novemba 4, 2010, alisema:

“Jamani nisameheni ibilisi alinipitia. Jana nikiwa Manzese, mwenzangu (Kibarabara) alinipigia simu akitaka aniletee gari la kunipeleka kwenye ‘riheso’ lakini simu yake ilipokatika, hawara wangu wa zamani, Laurent naye alinipigia simu, akinitaka niende nyumbani kwake Kinondoni ‘tukaagane’.

“Nilipofika tuliagana, lakini baada ya kumaliza shida zake nilimwambia aniache niwahi kanisani kufanya riheso, yeye akagoma akaniambia hakuna kwenda popote na kunifungia mlango kwa

Afande Masaitoo alipomuuliza kwanini hakupiga kelele kuomba msaada kama na yeye hakunogewa na uhondo, Bibiharusi Warda aliinamisha kichwa huku akisema: “Ibilisi alinipitia.”

Afande Masaitoo alimuuliza tena: “Kama mchumba ‘ako alikupigia simu akuletee gari kukupeleka kwenye riheso kanisani, kwanini uliacha safari hiyo na kwenda nyumbani kwa hawara?”

Biharusi: “Nilijua nisingechukua muda mrefu na ningeweza kuwahi kanisani baada ya kumalizana na mpenzi wangu wa zamani.”
BWANAHARUSI AKATAA KUFA NA TAI SHINGONI:

Baada ya Bibiharusi huyo kuweka hadharani ‘mauchafu’ yake hayo, Afande Masaitoo aliyekuwa akiongoza kikao cha usuluhishi alimshauri Bwanaharusi mtarajiwa kumsamehe mchumba wake na kuendelea naye (afe na tai shingoni), vinginevyo aende mahakamani kufungua kesi ya madai.

Bwanaharusi alifyatuka pale pale mbele ya umati kuwa, hawezi kumoa tena mwanamke huyo aliyethubutu kwenda ‘kuchakachua’ siku moja kabla ya ndoa kwani amemdhalilisha kwa kiasi kikubwa.

VIDOKEZO MUHIMU:

Habari za ndani zinadai kuwa, bajeti ya ndoa hiyo ikiwa ni pamoja na sherehe za harusi iligonga shilingi milioni kumi na mbili, tayari Ukumbi wa Holland uliopo Msimbazi Centre jijini Dar ulishalipiwa shilingi laki nane huku sare za harusi zikigharimu milioni kadhaa, vinywaji na chakula vya kumwaga, ndugu wengine wakitoka nje ya Dar kuja kuserebuka.
 
hahaha mbona ishu kama hizo za kuchakachua kabla ya harusi uswazi ni za kawaida sana. Nakumbuka 200-2002 niliisha Mbagala maeneo ya Sabasaba pale, kuna demu mmoja aliletwa na dada yake pale eti aje ajifiche mpaka siku ya harusi, huyo demu alitokea Buguruni, sasa kilichotokea kumbe jamaa lake la zamani likawa linakuja kumega kila wiki. Demu alikaa miezi miwili kwa sista yake, ilipofika siku moja kabla ya harusi jamaa lake likawa linamtafuta limmege siku ya mwisho demu akawa hataki kupokea simu, jamaa jioni mida ya saa mbili likamfuata demu mpaka hapo home kwa sista ake, bibi harusi mtarajiwa kuona kafwatwa na jamaa akaona isiwe tabu ngoja nikamwambie jamaa haiwezekani aende zake, weeeee jamaa alikuwa na ukame na nadhani alitaka kumvurugia tu demu si akambembeleza demu eti ampe cha fasta pale pale kwenye michongoma demu na yeye akili zijui zilikuwa wapi si akakubali eti fanya haraka kumbe kwa mbali kidogo wahuni wa kitaa wanaiona ile issue, walipoanza tu shuhuli aaagh watoto hawa hapa, nyie mnafanya nini hapa maskini wakakurupushwa ilikuwa aibu maana ilibidi kikao kikae wawapoze wale wahuni ili wasiseme, jamaa kesho yake akachoma ubani akaoa daaaaaaaaaah sasa wana watoto wawili yule wa kwanza mmmmmmmmmh inaonekana kachakachuliwaaaaaaaaa tehetehe
 
Duh hii nikali, ila kama anavyosema, msela hapo juu, mambo hayo yapo sana.
 
Mwanangu,hii kali.
Jamaa Mungu amemwepushia balaa,maana wangeoana hali ndo ingekua mbaya zaidi.
Kwa kifupi huyo mwanamke alikua hampendi huyo bwana harusi,maana angekua na mapenzi ya kweli asingejipeleka kuchakachuliwa.
 
Wanasema Mke Bora Hutoka Kwa Mungu. Bwana harusi amshukuru Mungu kwa kumuonyesha mapema kuwa huyo hakuwa wake!
 
Hii iliwahi kutokea huku Moshi. Tena inahusisha familia fulani ya kimangi. Demu aliitwa na jamaa wakapeane vya mwisho wakanogewa. Mbaya zaidi hata kwenda kurembwa hakutokea. Kaja kupatikna saa 11 jioni chumbani kwa jamaa yuko hoi. Muoaji alikataa lakini kuepusha kashfa jamaa akapewa kilo kadhaa akakubali shingo upande. Si unajua tena unapooa kwenye koo zenye feza maana shangazi naye mumewe wa zamani ana mpunga wa kisawasawa! Vyombo vya habari vya kumwaga achilia mbali makampuni yenye kuingiza fweza kila siku. Jamaaa baada ya kuoa kaacha mke Moshi yuko huko mikoani anasaka maisha. Wanaume wote wawili walikuwa marafiki sana ila sasa huyu akiingia hapa yule huyoooooo anatokea kule. Noma sana.
 
ndoa.jpg


Na Richard Bukos
Ndoa iliyokuwa ifungwe kati ya Bwanaharusi, Joseph Kibarabara na mkewe mtarajiwa, Warda Halfa, imetibuka kufuatia Bibiharusi huyo ‘kutekwa' na kufungiwa chumbani na mwanaume anayedaiwa ni hawara yake wa zamani, Risasi Jumamosi linamwaga mambo hadharani.

Varangati hilo lilijiri Novemba 7, mwaka huu maeneo ya Ukonga, Dar baada ya aliyekuwa Bibiharusi mtarajiwa, Warda kuacha njia ya kuelekea kanisani kufanya mazoezi ya kufunga ndoa ‘riheso' na mumewe mtarajiwa, Kibarabara na kumfuata mwanaume aliyedaiwa ni hawara yake aitwaye John Laurent.

MCHEZO ULIVYOANZA:
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, hawara huyo alimpigia simu Warda siku moja kabla ya ndoa na kumuuliza kama habari anazozisikia anaolewa ni za kweli.
"Laurent alimpigia simu Warda kumuuliza kama kweli anaolewa, akamjibu ndiyo, akamwomba aende nyumbani kwake ‘wakachakachue' kwa mara ya mwisho, naye akakubali akaenda," kilisema chanzo.

Chanzo kiliendelea kuweka wazi kwamba, wakati Warda anakwenda kwa mwanaume huyo, mumewe Kibarabara alishampigia simu akimtaka wakutane kanisani kwa ajili ya ‘riheso', wito ambao mwanamke huyo aliupuuza.

Habari zinadai, baada ya Warda kufika kwa ‘jamaa' yake wa zamani walichakachua kweli, lakini ghafla mwanaume huyo alimnyang'anya simu kisha akaizima na kutoa funguo kwenye kitasa cha mlango huku akimwambia ‘HAKUNA KUTOKA' licha ya kwamba alikuwa akijua mwanamke huyo atafunga ndoa kesho yake saa tisa Alasiri.


Ikazidi kuelezwa na chanzo chetu kwamba, njemba huyo aliendelea kustarehe na mke mtarajiwa wa mwenzake hadi Jumapili saa kumi na moja Jioni alipomwachia wakati ndoa ilikuwa ifungwe saa 9 Alasiri katika Kanisa la Sabato Ukonga (SDA).

MBINU ZA KUUA SOO ZAFANYWA:
Baada ya kubaini kosa kubwa walilolifanya, hawara huyo alimchukua Warda hadi kwenye Zahanati moja maeneo ya Manzese, Dar na kudanganya kwa daktari kuwa, mwanamke huyo alianguka ghafla na kupoteza fahamu maeneo ya hayo hivyo kupatiwa matibabu ya dharura.

Baada ya hapo, Warda alirudi nyumbani kwao ambako alikuta ndugu, jamaa na marafiki wamevimba sura kwa hasira, wengine wakikaribia kutumbuka kama siyo kupasuka.

Wakati hayo yote yanafanyika, inasemekana Bwanaharusi ambaye tayari na ‘bestman' wake walikuwa ndani ya suti mpya, alikuwa akiwakaba koo wazazi aliowalipa mahari akidai chake huku habari nyingine zikinyetisha kuwa, alishabonyezwa na wadaku kuhusu mchezo mzima wa Bibiharusi na jamaa yake wa zamani.

KAMATI KUU YA FAMILIA YAKETI KWA DHARURA:
Kufuatia tukio hilo la aibu chanzo kinadai, ndugu wa pande zote mbili waliketi kwa dharura nyumbani kwa shangazi wa Bibiharusi, Kimara Baruti, Dar ili kutafuta mwafaka na ndipo ghafla alitokea Warda akiwa amechoka ile mbaya.

Ndipo alipobanwa kisawasawa aeleze kinagaubaga nini kilitokea hadi

akaitumbukiza familia yake katika aibu kama ile, lakini wakati akimeza mate ili kujieleza, liliibuka varangati zito lililosababisha Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Magomeni ‘Mviringo', Mokola Maulid aliyekuwa kwenye kikao hicho kama ndugu, kupigwa baada ya upande wa Bwanaharusi kupandwa na jazba.

Kufuatia tafrani hiyo kuchukua muda mrefu huku wanandugu wa pande zote wakiwa na hasira, hasa mawifi, watu wenye hekima walishauri kwenda Polisi Kituo cha Mbezi Luisi, Dar ambako ukweli utabainika.

Safari ilianza mpaka Kituo cha polisi na kupokelewa na maafande wenye sifa zote katika mambo ya sheria na ulinzi wa raia huku wakiweka sawa kitabu kikubwa cha ‘kaunta' kwa ajili ya kuchukua maelezo ya pande zote mbili.
BIBIHARUSI NA AFANDE MASAITOO:

Akielezea mkasa huo mbele ya Sajenti Masaitoo wa kituo hicho cha Polisi, Biharusi ambaye sherehe ya kumuaga ‘Send Off' ilikuwa ya kukata na shoka ilifanyika Alhamisi ya Novemba 4, 2010, alisema:

"Jamani nisameheni ibilisi alinipitia. Jana nikiwa Manzese, mwenzangu (Kibarabara) alinipigia simu akitaka aniletee gari la kunipeleka kwenye ‘riheso' lakini simu yake ilipokatika, hawara wangu wa zamani, Laurent naye alinipigia simu, akinitaka niende nyumbani kwake Kinondoni ‘tukaagane'.

"Nilipofika tuliagana, lakini baada ya kumaliza shida zake nilimwambia aniache niwahi kanisani kufanya riheso, yeye akagoma akaniambia hakuna kwenda popote na kunifungia mlango kwa

Afande Masaitoo alipomuuliza kwanini hakupiga kelele kuomba msaada kama na yeye hakunogewa na uhondo, Bibiharusi Warda aliinamisha kichwa huku akisema: "Ibilisi alinipitia."

Afande Masaitoo alimuuliza tena: "Kama mchumba ‘ako alikupigia simu akuletee gari kukupeleka kwenye riheso kanisani, kwanini uliacha safari hiyo na kwenda nyumbani kwa hawara?"

Biharusi: "Nilijua nisingechukua muda mrefu na ningeweza kuwahi kanisani baada ya kumalizana na mpenzi wangu wa zamani."
BWANAHARUSI AKATAA KUFA NA TAI SHINGONI:

Baada ya Bibiharusi huyo kuweka hadharani ‘mauchafu' yake hayo, Afande Masaitoo aliyekuwa akiongoza kikao cha usuluhishi alimshauri Bwanaharusi mtarajiwa kumsamehe mchumba wake na kuendelea naye (afe na tai shingoni), vinginevyo aende mahakamani kufungua kesi ya madai.

Bwanaharusi alifyatuka pale pale mbele ya umati kuwa, hawezi kumoa tena mwanamke huyo aliyethubutu kwenda ‘kuchakachua' siku moja kabla ya ndoa kwani amemdhalilisha kwa kiasi kikubwa.

VIDOKEZO MUHIMU:

Habari za ndani zinadai kuwa, bajeti ya ndoa hiyo ikiwa ni pamoja na sherehe za harusi iligonga shilingi milioni kumi na mbili, tayari Ukumbi wa Holland uliopo Msimbazi Centre jijini Dar ulishalipiwa shilingi laki nane huku sare za harusi zikigharimu milioni kadhaa, vinywaji na chakula vya kumwaga, ndugu wengine wakitoka nje ya Dar kuja kuserebuka.

Ahaa huyo bwana harusi alikua hajampenda mwanmke sasa hilondo kosa lakuacha kuooa siangemsamehe tu akvutajiko halafu kama anamuona mtoto tuliatulia mpeleke tanga kwa babu mambo yameisha
toto limesimama kama twiga unaliacha checkni chingo hoyo wakuu
lakini huyo Xwake mshenzi kamharibia mwenzaka labda walikua nakisa au kalazimishwa kuolewa mana wengine huwa sikwaridha zao
 
mweee.ndo maana mimi nimeamua kutulia tuliii na NYANZALA wangu...
 
Duuh hiyo kali ya mwaka nigekuwa mimi sijui ningechukua uwamuzi gani maana nasoma lakini ninahasira mbaya!
 
Hata ukioa Nyambizi utamegewa tu, mwanamke anaibilisi hasi na mwanaume ana ibilisi chanya, wakikutana lazima wavutane tu. hakuna ujanja. hata hao wanaosema wametulia ila wakiona pembeni totos inawaka kama mshumaa wanadata sana. Unajua, sehemu kubwa ya ubongo wa mwanaume inafikiria sex tu. Ngono jamani haiepukiki. Hata uoe mwanamke mbaya vipi (kwa mtizamo wako) lakini wapo jamaa tu watamchakachua. Sasa tufanyeje wanaume, maana nyeto nalo linaua mishipa ya fahamu. Inabidi tuchangie tu hakuna jinsi.
 
kali ya mwaka wa uchaguzi!... Wanawake ar weak... Huyo demu alifuata maslah tu kwa huyo mumewe alyemsaliti nina uhakika ht angeolewa angemegwa na ex's wake hata ambao kwa style ya huyo demu hawapungui 6!
 
mimi naogopa kukomenti ila nachojweza sema ndoa za siku hizi haziaminiki hata kidogo, usije ukaoa ukadhani uko peke yako, maana nyie mwazungumzia hao wanaoagana lakini mwajua kuna wengine ambao hawaagani isipokuwa wanawazuga nyie tu? kweli nawaambia wapo wanaoooa/wanaoolewa ilhali wanaendelea kama kawa na wapenzi wao wa zamani, soo nyie mnaooana na kuolewa mumuombe sana Mwenyezi Mungu awasaidie mpate wenzi waaminifu ila mkipata tofauti ni karaha mno.
 
Back
Top Bottom