Ukistaajabu ya Musa Utaona ya Ndugai. Wanakufa wabunge CCM ila wanalindwa wa Chadema wakapime afya zao

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Siku zote huwa naamini kwenye usemi ule wa kwamba ukiwa na hasira jaribu kujiepusha kufanya maamuzi, kwani unaweza ukaonekana kituko. Hakuna ubishi kuwa wiki hii yote au tokea wabunge wa Chadema waondoke bungeni kwa ajili ya kuji-quarantine kuna mtu mmoja pale bungeni na si mwingine bali Job; akili yake haikuwahi kukaa sawa tokea waondoke, na hii inathibitishwa na kauli mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa mara kwa mara kama sio kila siku tokea waondoke. Kauli hizo zikiambatana na matusi, kejeli kusudi tu waonekane sio watu wema kwenye jamii.

Moja ya maamuzi alofanya ni kuwaagiza kuwa wanaporudi bungeni wahakikishe wanapima Covid-19. Jambo la kushangaza na ambalo Job alisahau ni kwamba hili wazo la kupima Wabunge wote lilitoka kwao Chadema baada ya kuona wabunge wa CCM wanaanza kupukutika na hivyo kuomba wabunge woote wakapime. Na hivyo kuwaagiza Chadema peke yao wakapime ilkuwa ni kama kumsukuma mlevi.

Kilichoshangaza umma badala yeye kama Boss wao kuitumia fursa hii kuwaagiza wabunge wote wakapime hasa CCM ambao ndio wanaongoza kwa kuzagaa nchi nzima i.e Mawaziri na wabunge wengine, mpaka wamekamatwa wakiwinda haramu. Yeye alipeleke hasira zake Chadema, jambo ambalo limewasaidia saana kujua afya zao.

JOB BWANA
 
Yule fupi alisomea mambo ya wanyama pori
Nashangaa kupewa uspika!
Alitakiwa kuwa ranger.
Halafu mkuu jifunze kuweka paragraph.
 
Kwanza kapimaje wakati maabara ni feki?hata matokeo hayo ni feki!!!!kama papai na mbuzi wamepima positive tusemeje vipimo ni halali? Nchi ina vituko hii!!
 
Daraani tulifundishwa kua Dola ina mihimili mitatu,Serikali Bunge na Mahakamani, ila kwa sasa tunaona ni Serikali,Serikali, Serikali Eti Mihimili ulii jichimbia zaidi.
 
Back
Top Bottom