Ukistaajabu ya kuua Albino Tz utayaona haya mapya ya Benin

MWILI NYUMBA

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
817
252
Nimeshtushwa sana na habari hii wakati naperuzi kurasa za BBC. Amakweli dunia inaelekea mwisho sasa.

Hivi karibuni kumezuka tabia ya kufukua maiti na kukata vichwa vyao na sehemu nyingine za mwili kwaajili ya mambo ya kishirikina ikiaminika kuwa hutumika kwaajiri ya kusafishia nyota (kwa wafuasi wa dini ya Voodoo wanaokadiriwa kufika 40% ya population ya Benin).Hivi karibu katika jiji la Port-novo (mji mkuu wa Benin) makaburi yanayokadiriwa kufika 100 yamekumbwa na unyama huu.


Kwa undani zaidi waweza fuata link hii ya BBC " http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-20550303"
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,852
2,718
Waganga wanaakil sana eti........ Ukiona hvo ujue Maeneo ya kuzka yamekuwa machache.
 

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
381
87
Ujinga tu wala si mwisho wa dunia. Waafrika hukimbilia majibu mepesi mepesi mbona ulaya hawafanyi hivo? Huo mwisho wa dunia ni Afrika tu? Acheni ujinga!
 

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
20,481
27,095
wadanganye wajinga wenzio.
Manabii wakubwa wote hawakujua kuwa siku ya mwisho itakuja lini.
Wewe mwongo umeambiwa na nani juu ya tarehe 23/12/2012

wapi kasema itakua siku ya mwisho?. acha kudandia treni kwa mbele. au unataka kujenga jina kupitia kwa flora?. pole sana dogo. mia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom