Ukistaajabu samaki mchanga, hujamuona samaki wa jangwani

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
"Njoo unisaidie kazi fulani, la sivyo hatutakula jioni hii." Nilimfuata. Aliingia ndani ya kibanda chake akatoka na ndoo yenye maji. Aliingia nayo mwenye zizi la mijusi akayamwaga hayo maji juu ya jiwe moja pana lililokuwa limebonyea kidogo katikati. Mijusi walikimbia haraka kunywa maji. Wakati wakinywa alishika mijusi kama ishirini hivi akawatumbukiza ndani ya ndoo. “Nifuate," aliniambia. Nilimfuata hadi nyuma ya kibanda. Alitoa kisu akaanza kuwakata vichwa na kisha akawapasua "Kazi yako ni kuondoa hayo matumbo." Nilifanya kwa kinyaa kazi niliyopewa, lakini nilijitahidi kuficha

Kijana aliingia kibandani akarudi na ndoo nyingine iliyokuwa na maji kidogo, akaanza kuwasafisha. Kazi hii ilipokwisha tuliongozana naye kibandani. Moto ulikokwa haraka. Akawaweka hao mijusi juu ya wavu wa chuma na kuwabanika

"Wana mafuta mengi," alisema akimeza mate,
"Sikujua mijusi wanaliwa.
"Zamani zile wakati chakula kilipokuwa kingi niliwaita mijusi. Sasa siwaiti hivyo tena. Hawa ni
samaki wa jangwani."
"Ni watamu?"
"Kuzidi samaki wa majini. Ulaini wa minofu yao uko kati ya nyama ya mbuzi na samaki wa majini, kati ya joto na baridi. Ni kama viungo vyote vimo ndani yake tayari."
"Umekaa hapa muda gani?" nilimuuliza kubadilisha mazungumzo.
"Miaka mingi tangu wakati ule wa njaa kuu. Sasa sitaki kuhama tena. Sijui mahali pengine penye samaki wengi wa jangwani na watamu kama hawa."
"Uliwezaje kuwafuga hawa samaki wa jangwani?"

“Nilianza kwa kuwapa mchwa na sisimizi. Baadaye niliwawekea maji. Wakati huo maji yalipatikana mbali sana. Nilikuwa bado sijagundua chemchemi iliyo karibu na kibanda hiki. Nilizoea kuondoka asubuhi na kibuyu changu na kurudi jioni na maji. Baadaye samaki wa jangwani waliponiona tu na kibuyu walinifuata wenyewe hadi nyumbani, wakanisubiri karibu na lile jiwe nilipozoea kumwaga maji machafu. Baada ya miezi walinizoea kabisa. Wakawa hawaendi mbali na kibanda changu. Mwishowe nililizungushia jiwe ukuta, likawa kama zizi. Wameweza kutunza uhai wangu hadi hivi sasa. Si hivyo tu. Hawa samaki wa jangwani hawana dhana ya kukataa. Hukubali kila kitu kwa kutingisha vichwa vyao kama alama ya heshima. Wanatuliza kidogo ile hali ya ubwana aliyo nayo binadamu."

"Una raha ya kutosha?"
"Raha? Unanikumbusha shairi moja lisemalo Raha ya kweli kinaya, kukinai yako hali.'Hapa nilipo nimekwisha pazoea. Ni kama nimefungwa hapa. Kuhama siwezi."
"Huna uhuru yaani?"
"Uhuru! Dunia inahitaji uhuru gani ili ipate kuzunguka kwenye mhimili wake? Hakuna binadamu asiyekuwa na nguvu za kuzunguka kwenye mhimili wake mwenyewe. Uhuru huu umefichama katika mcheko. Hakuna binadamu asiyecheka." Wakati huu kazi ya kuwabanika hao samaki wa jangwani ilikuwa tayari. Alianza kuwapanga vizuri ndani ya chungu na kisha akaweka maji. Alitenga
chungu juu ya mafiga, akakifunika."

"Utakaa nami kwa muda au una haraka ya kwenda huko uendako."
"Haraka ninayo, ila niko radhi kukaa nawe kwa siku chache."
"Vizuri. Nitapata muda wa kukuonyesha baadhi ya mambo ambayo ninafanya."
Kimya.

"Umeoa?" nilimwuliza kwa utulivu. Alinitazama.

"Hapa nilipo sina mke. Kwa sasa hivi sioni haja. Kuna kazi muhimu ambayo nafanya.'

Tuliendelea kuzungumza. Tukawa tunabadilishana mawazo kuhusu mada mbalimbali. Samaki wa jangwani walipokuwa tayari, alitenga sufuria la ugali.

"Unga unaupata wapi?”

"Hulima mpunga na mahindi kidogo humu bondeni. Shida hufunza mengi." Chakula kilipokuwa tayari nilianza kuwa na wasiwasi
wa kutapika. Lakini nilipomwona yeye anakula kwa hamu kubwa nilifumba macho nikauambia moyo kuwa nilikuwa nakula samaki wa majini.

"Hawa samaki wana ladha ya aina yake," nilisema baada ya kumeza matonge mawili.

"Hujui namna ya kuwala," alisema akinitazama; “Kwanza unakula sehemu nyororo ya tumboni, halafu unamwanzia kwenye mkia na kumalizia na minofu ya kifuani.” Baada ya chakula hatukuwa na mazungumzo marefu. Alinitayarishia kitanda nikalala. Sikupata
usingizi kwa sababu ya wingi wa mbu. Nililala jogoo la kwanza lilipowika. Mbu nao wakafaidi sadaka ya damu. Kifungua kinywa cha asubuhi kilikuwa cha mchuzi mzito wa matumbo ya samaki wa jangwani.

Tulipomaliza, aliwafungulia wale samaki wa jangwani mlango wa ukuta, wakatoka nje kwenda machungani.

"Wamekwishazoea," alisema "Ikifika jioni watarudi wenyewe mwenye zizi lao."
 
Giant, ndio mwisho au kuna mwendelezo wa supu ya jangwani?
 
Hii Ni Kwa Mabaharia
 
Oops Ndiyo Kama Huyu
20211022_150740.jpg
 
Ndoto ya alfajiri alfajiri hua inakupeleka kwenye uhalisia hasaaa.
Siyo ndoto tu mkuu, hata unachokiwaza alfajiri huwa kina mashiko na kinatekelezeka.

Akili huwa imetulia haijakumbana na musukosuko na adha za mchana.
 
Back
Top Bottom