Ukistaafu, ukitumbuliwa, ukiacha kazi utakuja kuishi na sisi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Hakuna Jambo linawatesa wastaafu na waliotumbuliwa kama kuwaza namna yakuja kuishi uraiani na sisi. Wengi wa wadosi wa siku hizi wamewekeza sana kuaribu maisha ya wanaowaongoza kuliko kuwaletea maendeleo wanannchi.

Viongozi wetu wamekuwa wepesi sana kumwita subordinate wake fisadi, mwizi nk bila kujala kama kuna ushahidi au la.

Nguvu inayotumiwa kuwatesa wadogo imekuwa kubwa kuliko hata nguvu waliyotumia babu zetu enzi za ukoloni.

Kinachowasumbua sasa hivi ni kupanga pa kwenda kuishi nafamilia yake akistaafu au kuachishwa kazi, wengi waliokuja kuishi huku kijijini wamejikuta wakipokea lawama kutoka kwa wale waliowaaribia maosha. Kijijini na uraiani pamekuwa si sehemu salama kwa baadhi ya wastaafu hasa wale waliowekeza kubomoa future za watu kwa lengo lakulinda mishahara yao.

Pensheni imekuwa chungu na wengi wamekuwa wamepatwa msongo wa mawazo na kufa au ku-paralize mara tu wanapostaafu. Mapokeo mabaya wanayokutana nayo yamefupisha maisha yao.

Niwaombe viongozi na watumishi wa Umma kujiuliza watakwenda kuishi wapi baada ya muda wa utumishi wao kwisha? Je, utakuja kwetu kama adui au rafiki?
 
Back
Top Bottom