Ukistaafu serikalini, unaweza ukaajiriwa tena na sekta binafsi? Na makato ya NSSF yakaendelea?

Superfly

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
965
1,966
Kama heading inavyojieleza, yaan mtu huyu aliestaafu serikalini, anaweza akawa muajiriwa wa sekta binafsi na serikali ikamtambua na ikaendelea kumuwekea akiba yake kwenye mfuko wa NSSF??

Nawasilisha.
 
Kama heading inavyojieleza, yaan mtu huyu aliestaafu serikalini, anaweza akawa muajiriwa wa sekta binafsi na serikali ikamtambua na ikaendelea kumuwekea akiba yake kwenye mfuko wa NSSF??

Nawasilisha.
Serikali haihusiki na wewe kupelekewa pesa mifuko ya hifadhi ya jamii, mwajiri wako ndio ana jukumu la kukata michango yako na kuipeleka huko.

Kwa kuwa ulikuwa Serikalini, maana yake michango yako itakuwa PSSSF.

Na ukipata kazi sekta binafsi maana yake michango yako itawekwa NSSF.

Kwahiyo kama mafao yako ya mwanzo hukuchukua, then siku ukija kuchukua itakubidi ufanye michakato mara 2 separately.

Yaani ufuatilie pesa zilizoko NSSF kwa kufuata masharti yako halafu ukimaliza ufuatilie pesa zilizoko PSSSF kwa utaratibu wao.

Binafsi nakushauri, kama umemaliza mkataba au umefukuzwa KAZI, chukua chako ufe nacho. Ukipata kazi nyingine utaanza upya.

Hiyo Mifuko siyo ndugu zako wa kukutunzia hizo pesa, utazipoteza.
 
Mimi ninachoelewa ni kuwa Ukistaafu Serikalini unaweza ukaajiriwa kwenye private. Ila kwa kuwa mwanachama atakuwa ameshaanza kupata pensheni basi NSSF watamwandikisha kwenye mfumo wa hiari atachangia yeye 10% na mwajiri 10% kwa kuwa hata kazi yake itakuwa ya mkataba.Na akimaliza muda wa kazi NSSF itamlipa mkupuo pamoja na riba
 
Kama heading inavyojieleza, yaan mtu huyu aliestaafu serikalini, anaweza akawa muajiriwa wa sekta binafsi na serikali ikamtambua na ikaendelea kumuwekea akiba yake kwenye mfuko wa NSSF??

Nawasilisha.
NSSF ni disaster. Chukua mshahara bila makato ya NSSF
 
Back
Top Bottom