Ukisoma vizuri ripoti ya CAG hutatamani kubakia CCM sema tu hakuna chama mbadala kinachoongozwa na Mtakatifu

Mimefanikiwa kuisoma ripoti yote ya CAG aliyoitoa hivi karibuni na kumkabidhi mh Rais.

Ripoti nimeielewa.

Ukiitafakari hii ripoti hutakuwa na hamu ya kuishabikia CCM kwa sababu kama chama dola kimeshindwa kuikata mirija ya ufisadi na rushwa katika mifumo ya serikali.

Tatizo ni kwamba hatuna chama mbadala cha siasa chenye afadhali, vyama vyote ndio " wale wale"

Zamani mambo kama haya wajeda walikuwa wanajitwalia uongozi lakini hizi ni zama za demokrasia.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
KUWA CCM NI KUJIHAKIKISHIA KWENDA MOTONI SIKU UKIFA
 
NCHI YA KIDEMOKRASIA lakini CCM Inaendesha nchi kwa SELF KRASIA tulikuwa na tatizo la mtu na chato,leo naona mtu kukaimu uraisi baada ya mh Kusafiri KWENDA USA naona kaimu Raisi nae huyo kapaa Kwenda kwao BUHIGWE KIGOMA,huko mama nae kakutana na mawe ya kudai katiba MPYA,hivi lingetokea la kutokea tungetangaziwa Toka Buhigwe,naona tungeona kama ameroga huyu kaimu Raisi.
 
Baada ya utafiti wa muda mrefu kwenye siasa za Tanzania; sasa kwa kujiamini sana naweza kusema CCM haijawahi kuwa tatizo na Tanzania hatuna tatizo la chama cha siasa bali watu.

Tuna kundi kubwa sana la watu wa ovyo ambao wametawanyika karibu kila mahali kwenye jamii. Katika mazingira kama hayo, kama chama cha siasa kitaundwa na watu kutoka kwenye jamii hii hii, hakuna namna ambayo tutakwepa kuona miujiza.

Narudia tena, tatizo sio CCM tatizo ni jamii.
Jamii ndo ilivuruga uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na kuiba kura kwenye uchaguzi mkuu 2020? Unawezaje kutumia vyombo vya dola kuiba kura,halafu uingie madarakani uzuie watumishi wa umma kuiba pesa za umma? NISAIDIE PLZ
 
Back
Top Bottom