ukisoma hii utafurahi sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ukisoma hii utafurahi sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtende, Oct 25, 2010.

 1. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  jamani kweli naamini watanzania wamechoka

  leo nilikuwa huku shinyanga vijijini kwa ajili ya kuwaelimisha vijana umuhimu wa kuhudhuria kupiga kura siku ya jumapili,mida ya jioni nikajisogeza katika kijiwe kimoja ambocho ndio kuna tv pekee ya kijiji(kwa wale wenyeji kijiji kinaitwa mwamalula) mida hiyo watu walikuwa wamejirundika wengi sana wamekaa kimya wanaangalia taarifa ya habari,na kwa wakati huo habari iliyokuwa hewani ni ya kampeni za dk slaa,kilichonishangaza zaidi baada ya habari za kampeni ya dk slaa zilifuatia habari za thithiem,sikujua watu walisambaratika vipi huku nyuma wakiacha maneno machafu ambayo sikutegemea,kwa kweli ilinitia moyo sana

  katika hali ya kushangaza baba yangu ni kigogo wa ccm kwa muda mrefu sana katika ngazi ya wilaya ila leo amenipigia sim na kuniuliza kama nimejiandikisha kupiga kura,nikamjibu kuwa nimejiandikisha na kura ntapiga

  BABA AKANIAMBIA "NAOMBA UMPIGIE SLAA KURA" nikamwambia tupo pamoja

  JF chagua SLAA kwa maendeleo
   
 2. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  .
  Tupo pamoja mkuu. Ccm ni mwizi ambae baada ya kukomaa anajiibia mwenyewe. Hivyo wao kwa wao hawaelewani tena kwani lugha imechafuka.
   
 3. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  SLAA for president 2010 wakuu no coments on this.
   
 4. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hii inatia moyo sana! Mungu ibariki Tz!
   
 5. T

  The King JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mie nilipita kijiwe cha taxi drivers leo basi nikakuta wanaongea kuhusu uchaguzi nikasimama pale ili kusikiliza. Yaani! nilifurahia sana kuona wengi wao walivyo na ufahamu mkubwa na kampeni zinazoendelea. Wengi wao walidai wao ni waislam na hawaamini kauli ya thithiem kwamba Chadema na Rais Mtarajiwa wanataka kuleta udini, wanataka kuleta umwagaji wa damu au kuleta ukabila. Pamoja na kujua kwamba thithiem watafanya ujambazi wa kuiba kura lakini walikuwa wanahimizana kupiga kura kwa Dr Slaa na Wabunge wa Chadema. Inatia moyo sana.
   
 6. A

  Annony Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli nimefurahi sana! :smile-big: Athante thana kwakweli!
   
 7. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bravo. Chadema. Operesheni inaendelea huyo mama lazima ajifungue 31.10.2010. mafisadi wanalia............
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  tantalilalilalila tantalilalilalila tantalilalilalila tantalilalilalila ................(hiyo ni ala ya music wajumbe, naanza kushangilia ushindi wa Dr. wa ukweli) nimeandaa kreti 10 za bia na mapipa 4 ya gongo kwa ajili ya sherehe siku ya kuapishwa Slaa, karibuni sana kwa wale walevi wa sikukuu tu kama mimi, nawapa mualiko rasmi.)
   
 9. D

  Dopas JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwaliko rasmi wapi Zumbemkuu? Kwenye JF, toa adress walau ili tuje. Sema sinza, ilala, temboni,.... kwa Dsm. Au kwingine....

  Ila ukweli ndo huo, lazima tujiandae kusherehekea ushindi, usisahau kuwakumbusha ndugu jamaa, marafiki, hadi kijijini kwako wampigie kura DR. WILBROAD P. SLAA, a.k.a presidaa 2b na wabunge wa Chadema.

  Ila kwa kweli mwaka huu muhimu ni Rais. Mtu asimind kama mbunge wake wa CCM ni mali kwa maendeleo ya taifa kama alivyo Mwakyembe, anaweza kumpa kura, ila ya Rais zote kwa Slaa. Tuwaelimishe watu wetu hasa kijijini kuwa kama kura ya mbunge-makini atampigia wa ccm, rais ampigie wa Chadema, Dr. Slaa.

  Ila kwa maeneo ambao Chadema kuna mgombea wa Ubunge, basi kura apewe ili serikali iweze kuundwa. Ni hayo tu kwa leo.
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280

  kila siku naweka vocha za mitandao yote za dola mbili kila mtandao kuwahamasisha kwenda kupiga kura. subiri dopas ntawajulusha mahali, asaiv haifai maana gongo haijahalalishwa naweza nkafuatwa. siku moja kabla hajaapishwa ntawataarifu wana JF wapenda mitungi waje tusherehekee.
   
 11. v

  vickitah Senior Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Hapo umenena mkuu si hatuna tatizo na chama, rangi ya mtu, wala dini, wala kabila lake.. tuna tatizo na viongozi wabovu tu kwa kweli!!
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ccm hawaamini kama wamechokwa
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Jana jioni wakati najiandaa kukata tiketi ya kivuko nikakuta watu wanne wameweka kijiwe huku wakimsikiliza mmoja wao ambaye alikuwa anawahubiria kwamba wasichague upinzani kwa kuwa hakuna kitakachobadilika na mambo ni yaleyale. Aisee nilisimama na kuwaomba radhi kisha nikawaambia kwamba mkichagua upinzania hasa dr. slaa mambo yatabadilika naomba huyu mwenzenu aelewe hivyo. Watu watatu walishangilia sana na yule pro-kikwete akabaki amenyeshwewa.

  Nilimharibia sana, naamini alikuwa na kazi ya kuanza upyaa propaganda zake kwani niliposema hivyo nikawapa na data za angalizo na ubaya wa propaganda chafu za kuonesha kwamba upinzani umeshindwa.

  Jamani tujitume mda wa ziada huu
   
 14. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Sio Shinyanga na Mwanza pekee, hapa majuzi nilikuwa jimboni Mlalo wilayani Lushoto - Tanga, hapo ni Slaa na Kagonji tu. Huu mwaka una mambo makubwa yaja.
   
 15. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hapa soko kuu Arusha nimepita jioni ndani ya soko nikakuta mzozo wa wanaouza pumba za kuku, nafaka na samaki na niliposikiliza nikakuta wanajadili adhabu ya kuwapa CCM siku ya tarehe 31/10. Vyama viwili vilikuwa vinabishaniwa yaani CHADEMA na CCM. Nilipomwita pembeni muuzaji maarufu wa maharage nikamwuuliza kuhusu upepo wa kisiasa aliniambia wameganyika katika CCm na CHADEMA lakini akasema asilimia 80 wanaunga mkono CHADEMA. Basi nikatoka zangu nikasema basi TUMEMALIZA KAZI
   
 16. b

  bahati stanz Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo gud gud sana. msisahau sala zenu rafiki zangu.
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Safi sana nimeipenda thread yako!lakini kuna sehemu moja hukunifurahisha,baba yako alipokuambia "umpigie kura Dr Slaa,wewe ukamjibu tupo pamoja"ulipaswa umuulize kwa nini Dr Slaa na si JK,hili swali lilikuwa na umuhimu mkubwa ili kuchochea udadisi wa mambo,ili kujua zaidi watu wa kijijini wana mtazamo gani na Dr slaa?na je wanajua kuwa JK ni msanii namba moja!.Hata hivyo nashukuru sana kwa mchango wako!
   
 18. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Ukishapata mtu anakuambia atamchagua DR.Slaaaaaaaa kwa furaha huwezi kumbuka kumwuliza habari za JK:yield:
   
 19. K

  Kibode Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nataka kuwakumbusha jamani kuna kundi ambalo bado halijaamka vizuri na mageuzi haya kundi hili ni lile la kina mama wanaobaki majumbani,kina dada wanaotuuzia vinywaji mida ya jioni (bar maids) mara nyingi nimekuwa nikiuliza swali kichokozi tu kuwa,utapiga kura mwaka huu?Majibu ninayopata ni either siwezi kupiga kura sababu hata nikipiga CCM wataiba tu,na atakayejibu kuwa atapiga kura atakuambia nitapigia CCM ukimuuliza kwa nini anakuuliza unafikiri CCM itatoka madarakani,kinachotia moyo ni kwamba unapochukua muda wako kidogo kuwaelimisha huwa ni wepesi wa kubadilika fikra.

  Ombi langu,tujitahidi kuongea na yeyote kuhusu uchaguzi na ikibid tuwachokoze kuhusu itikadi zao,itatusaidia kuongeza idadi ya kura kutoka kwa "un decided voters".
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ha ha ha haa!! katika kila vikundi 20 utakavyokuta wajadili hali ya uchaguzi, 90% ya wajumbe wanamshabikia Dr. Slaa. DR. wa ukweli.
   
Loading...