Ukisoma haya maoni unaweza kudhani kuna Zitto Kabwe wawili duniani!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Maoni ya Zitto Kabwe yamenifanya nizidi kuwa na shaka/ajizi (reservation) kwa yale ambayo anayasema lakini pia yanayosemwa na wanasiasa wa Tanzania!

Kwa muda wa siku 12, Zitto amebadili msimamo kwa jambo ambalo mazingira yake bado ni yaleyale. Ni kama anachokishauri anakifanya kulingana na upepo unavyovuma bila kujali kama huo upepo niwa muda mfupi au muda mrefu!

Nakumbuka mwaka 2013, Zitto aliwahi kusema tusiwaamini wanasiasa, Chama Tawala wala Wapinzani.

Ukitaka kusoma alichokisema Zitto kuhusu kutowaamini wanasiasa unaweza kugonga hapa;

LINK>>>Zitto Kabwe: Msiwaamini wanasiasa, chama tawala wala wapinzani

Nadhani Zitto haifuati kanuni inayosema, ''ukiwa muongo usiwe msahaulifu''

Haya ndiyo aliyoyasema Zitto ndani ya siku 12!

Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona- Zitto

- Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona kwa Uchumi wa Tanzania kwa ujumla na Bunge lijadili Kwa maslahi ya Taifa ili kutoa mapendekezo ya kibajeti kuhami Uchumi wa Nchi yetu na haswa kulinda biashara ndogo, Wafanyakazi kwenye sekta zilizo hatarini kama Utalii, huduma za vyakula, usafirishaji na uchuuzi.

Zitto Kabwe, MP
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
17/3/2020

Wananchi Wanapata ujumbe gani wanapoona Bunge linaendelea na vikao? Wanapata picha gani wanapomuona Rais wao anaendelea na mikutano yenye mikusanyiko? Nimemuomba kwa heshima zote Mheshimiwa Rais, hatua zichukuliwe kusimamisha vikao vyote vya Kiserikali ikiwemo Bunge, Mahakama n.k.

Bunge linaweza kukutana mwezi Mei na likaendelea na vikao tukiwa salama na tumedhibiti maambukizi. Mahakama zinaweza kukutana mwezi Mei na Mikutano mingine ya kiserikali inaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kama Video Conference, kama alivyofanya Waziri Mkuu juzi akiwa na Wakuu wa Mikoa.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb.
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo.

29 Machi 2020.

Katika moja ya mambo ambayo wanasiasa hasa wa upinzani yanawaangusha ni kukosa msimamo thabiti au kuwa vigeugeu kwa yale wanayoyasema na kuyatenda.

Zitto aliyeshauri bunge lifanye vikao vyake ili Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona lakini baada ya 12, Zitto huyo huyo anashangaa kwa nini bunge lifanye vikao vyake wakati kuna Janga la ugonjwa wa COVID-19?

Ni kama vile ametegesha mtego kama bunge likiahirishwa atajitokeza na kusema, unaona nilitoa ushauri wa kuahirisha bunge na wameufuata! Kama bunge halitaahirishwa na Waziri wa fedha kupeleka hoja bungeni, atajitokeza tena na kusema, unaona nilishauri serikali ipelekwa hoja bungeni kuhusu Janga la COVID-19.

Jiulize, mtu ambaye alifuata ushauri wa Zitto aliotoa tarehe 17/03/2020 na kuanza kutayalisha repoti ili apeleke bungeni, baada ya siku 12 anasikia tena ushauri ukitoka kwa Zitto huyo huyo akishangaa kwa nini bunge liendelee wakati kuna Janga la COVID-19.

Kwa misimamo hii ndio maana kampuni ya utafiti inayoitwa Afrobarometer ilifanya utafiti na kugundua wanasiasa wa upinzani wanaaminiwa na wananchi kwa asilimia 36.
Screenshot (49).png
 
Mkuu wanasiasa wa Tanzania kamwe usiwaamini. Kumbuka CHADEMA waliwaita majina yoote mabaya mh Lowasa na Sumaye. Lakini baada ya viongozi hao kuhamia katika chama chao waliwasifia kwa kila mazuri na kuanzisha slogan ya safari ya matumaini.

Hivyo basi kama wewe siyo mwanasiasa usijihangaishe na siasa za Tanzania. Kama Mh Rais angezuia mikusanyiko na kuamuru watu kubakia majumbani kwao na kwa bahati mbaya wananchi wakafa kwa njaa au maradhi yoyote wakiwa majumbani kwao tofauti na corona, huyo huyo zitto ndiye angetokea na kuilaumu serikali (Rais) kwa uamuzi huo.

Watu sisi tunao ndugu zetu Kenye, ukiongea nao wanasema bora waruhusiwe kujitafutia riziki yao ya kila siku hata waugue corona kulikoni mateso wanayoyapata.

Na kama unavyofahamu 80% ya waafrika riziki yetu iko miguuni mwetu. Ukitembea ndiyo unapata riziki. Chukulia mtu kama mama rishe, msukuma mkokoteni, muuza mbogamboga, agent wa usafiri nk mtu wa aina hii pasipo kutoka familia yake itaishi?

Wanasiasa wengi wanatetea matumbo yao kwa kuwahadaa wapiga kura. Na wapiga kura wengi wanatumia vichwa/akili za wanasiasa kuwaza. Hawaangaishi akili zao kutafasili matamko ya wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wanasiasa wa Tanzania kamwe usiwaamini. Kumbuka CDM waliwaita majina yoote mabaya mh Lowasa na Sumaye. Lakini baada ya viongozi hao kuhamia katika chama chao waliwasifia kwa kila mazuri na kuanzisha slogan ya safari ya matumaini.

Hivyo basi kama wewe siyo mwanasiasa usijihangaishe na siasa za Tanzania. Kama Mh Rais angezuia mikusanyiko na kuamuru watu kubakia majumbani kwao na kwa bahati mbaya wananchi wakafa kwa njaa au maradhi yoyote wakiwa majumbani kwao tofauti na corona, huyo huyo zitto ndiye angetokea na kuilaumu serikali (Rais) kwa uamuzi huo.

Watu sisi tunao ndugu zetu Kenye, ukiongea nao wanasema bora waruhusiwe kujitafutia riziki yao ya kila siku hata waugue corona kulikoni mateso wanayoyapata.

Na kama unavyofahamu 80% ya waafrika riziki yetu iko miguuni mwetu. Ukitembea ndiyo unapata riziki. Chukulia mtu kama mama rishe, msukuma mkokoteni, muuza mbogamboga, agent wa usafiri nk mtu wa aina hii pasipo kutoka familia yake itaishi?

Wanasiasa wengi wanatetea matumbo yao kwa kuwahadaa wapiga kura. Na wapiga kura wengi wanatumia vichwa/akili za wanasiasa kuwaza. Hawaangaishi akili zao kutafasili matamko ya wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu;
Umeandika mambo ya msingi sana ambayo yanafikirisha kwa mtu mwenye akili kubwa!

Yaani ukiwafuatilia baadhi ya wanasiasa na kuweka kumbukumbu kwa yale wanayoyasema, baada ya muda unaweza kujikuta unadharau kila wanalolisema!
 
Hawa watu akili zao hazina akili. Wanajibu hoza za msingi kwa matusi. Matusi ndiyo sera yao. Aliyepiga marufuki viloba Mungu ambaliki sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu;
Wala usihangaike na matusi yao. Sisi tutawaelimisha kwa hoja.

Wanatumia matusi ili watuondoe kwenye hoja na watupeleke kwenye eneo la kipumbavu ambalo wana uzoefu nalo!
 
Kwamba wakati Mh Zitto anaomba waziri wa Fedha alisema kua mswada upelekwe kwenye Bunge hili? na Bunge likipelekwa adi mwezi Mei ndiyo muda na maana ya kuwasilisha mswada utakua hauna maana tena?
Sijaona sehemu yoyote ambayo Zitto amesema kua mswada upelekwe kwenye vikao vya sasa.
Mleta mada wewe unaona hoja zote za Zitto hazina mashiko au amekosea kwa kuya wasilisha kwa muda mfupi?
 
Zitto ana ajenda zake za siri...good enough wanaintelijensia washafahamu hilo
Mleta mada alitaka Mh Zitto aseme kua '' Nashauri vikao vya Bunge zisogezwe mbeli adi mwezi Mei wakati huo waziri wa Fedha na Mipango alete mswada Bungeni ikionesha madhara ya mlipuko wa ugonjwa wa CORONA kwenye uchumi ili wabunge wajadili na kuishauri serikali''.
Mtoa mada hajui kua vyote vimeshauriwa kwa namna tofauti bali kwa kuipa uandaji wa taarifa na kuwasilisha mswada kwanza.
 
Kwamba wakati Mh Zitto anaomba waziri wa Fedha alisema kua mswada upelekwe kwenye Bunge hili? na Bunge likipelekwa adi mwezi Mei ndiyo muda na maana ya kuwasilisha mswada utakua hauna maana tena?
Sijaona sehemu yoyote ambayo Zitto amesema kua mswada upelekwe kwenye vikao vya sasa.
Mleta mada wewe unaona hoja zote za Zitto hazina mashiko au amekosea kwa kuya wasilisha kwa muda mfupi?
Mkuu;
Niliyoweka ni sehemu ya waraka wa ushauri wake. Kama unataka kujua kama alikuwa na maana ya bunge hili au la unakiwa kusoma waraka wote!

Kasome waraka wote!
 
Mnajiita wasema ukweli ila hampendi kabisa ukweli. Pathetic!!
Maoni ya Zitto Kabwe yamenifanya nizidi kuwa na shaka/ajizi (reservation) kwa yale ambayo anayasema lakini pia yanayosemwa na wanasiasa wa Tanzania!

Kwa muda wa siku 12, Zitto amebadili msimamo kwa jambo ambalo mazingira yake bado ni yaleyale. Ni kama anachokishauri anakifanya kulingana na upepo unavyovuma bila kujali kama huo upepo niwa muda mfupi au muda mrefu!

Nakumbuka mwaka 2013, Zitto aliwahi kusema tusiwaamini wanasiasa, Chama Tawala wala Wapinzani.

Ukitaka kusoma alichokisema Zitto kuhusu kutowaamini wanasiasa unaweza kugonga hapa;

LINK>>>Zitto Kabwe: Msiwaamini wanasiasa, chama tawala wala wapinzani

Haya ndiyo aliyoyasema Zitto ndani ya siku 12!

Katika moja ya mambo ambayo wanasiasa hasa wa upinzani yanawaangusha ni kukosa msimamo thabiti au kuwa vigeugeu kwa yale wanayoyasema na kuyatenda.

Zitto aliyeshauri bunge lifanye vikao vyake ili Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona lakini baada ya 12, Zitto huyo huyo anashangaa kwa nini bunge lifanye vikao vyake wakati kuna Janga la ugonjwa wa COVID-19?

Jiulize, mtu ambaye alifuata ushauri wa Zitto aliotoa tarehe 17/03/2020 na kuanza kutayalisha repoti ili apeleke bungeni, baada ya siku 12 anasikia tena ushauri ukitoka kwa Zitto huyo huyo akishangaa kwa nini bunge liendelee wakati kuna Janga la COVID-19.

Kwa misimamo hii ndio maana kampuni ya utafiti inayoitwa Afrobarometer ilifanya utafiti na kugundua wanasiasa wa upinzani wanaaminiwa na wananchi kwa asilimia 36.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom