Ukisoma haya maoni unaweza kudhani kuna Zitto Kabwe wawili duniani!

Mkuu MsemajiUkweli si kweli kwamba kwa jinsi na namna Rais Magufuli, mwanasayansi, anavyoendesha siasa Tanzania imewaweka wanasiasa katika wakati mgumu wa kutokujua waseme na watende nini?
Zitto ni kama anatoa matamko ya "kutegesha"!
 
Maoni ya Zitto Kabwe yamenifanya nizidi kuwa na shaka/ajizi (reservation) kwa yale ambayo anayasema lakini pia yanayosemwa na wanasiasa wa Tanzania!

Kwa muda wa siku 12, Zitto amebadili msimamo kwa jambo ambalo mazingira yake bado ni yaleyale. Ni kama anachokishauri anakifanya kulingana na upepo unavyovuma bila kujali kama huo upepo niwa muda mfupi au muda mrefu!

Nakumbuka mwaka 2013, Zitto aliwahi kusema tusiwaamini wanasiasa, Chama Tawala wala Wapinzani.

Ukitaka kusoma alichokisema Zitto kuhusu kutowaamini wanasiasa unaweza kugonga hapa;

LINK>>>Zitto Kabwe: Msiwaamini wanasiasa, chama tawala wala wapinzani

Nadhani Zitto haifuati kanuni inayosema, ''ukiwa muongo usiwe msahaulifu''

Haya ndiyo aliyoyasema Zitto ndani ya siku 12!





Katika moja ya mambo ambayo wanasiasa hasa wa upinzani yanawaangusha ni kukosa msimamo thabiti au kuwa vigeugeu kwa yale wanayoyasema na kuyatenda.

Zitto aliyeshauri bunge lifanye vikao vyake ili Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona lakini baada ya 12, Zitto huyo huyo anashangaa kwa nini bunge lifanye vikao vyake wakati kuna Janga la ugonjwa wa COVID-19?

Ni kama vile ametegesha mtego kama bunge likiahirishwa atajitokeza na kusema, unaona nilitoa ushauri wa kuahirisha bunge na wameufuata! Kama bunge halitaahirishwa na Waziri wa fedha kupeleka hoja bungeni, atajitokeza tena na kusema, unaona nilishauri serikali ipelekwa hoja bungeni kuhusu Janga la COVID-19.

Jiulize, mtu ambaye alifuata ushauri wa Zitto aliotoa tarehe 17/03/2020 na kuanza kutayalisha repoti ili apeleke bungeni, baada ya siku 12 anasikia tena ushauri ukitoka kwa Zitto huyo huyo akishangaa kwa nini bunge liendelee wakati kuna Janga la COVID-19.

Kwa misimamo hii ndio maana kampuni ya utafiti inayoitwa Afrobarometer ilifanya utafiti na kugundua wanasiasa wa upinzani wanaaminiwa na wananchi kwa asilimia 36.
Zitto ni akili kubwa sana kwa mtu kama wewe kumuelewa. Kuna njia nyingi za kufanya mikutano wakati wa majanga kama haya, hivyo sio kosa lako lakini.
 
Back
Top Bottom