Ukisoma hapa utakumbuka enzi zileeeeee!

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Enzi hizo Redio ni Moja tu RTD ya ukweli.
Sasa basi ilikuwa raha kusikiliza mpira halafu mshinde.
Na inayofuata hapa sasa ni nukuu ya kipande cha mwisho cha matangazo ya mpira wa Miguu kati ya Simba ya Dar es Salaam na Yanga ya Tanzania.

'''eeh Mafundi mitambo wetu ktk matangazo haya walikuwa ni Noel Namaloe na Edward Kwilasa.

Na kule ktk Gari yetu ya Matangazo alikuwepo Obi Mwambungu.

Mtangazaji Mwenzangu ni Omar Jongo, Mimi ni Charles Hillary, nawarudisheni Studio Barabara ya Nyerere kwake Nadhir Mayoka kwa ajili ya vipindi vinavyoendelea.

Kutoka hapa uwanja wa Taifa sina la ziada,
Yanga 2-0 Simba...Asanteni
 
afu redio yenyewe mnasikilizia kwa balozi wa nyumba kumi!!!lol
 
".......ilinibidi niseme goli kabla mpira haujaingia wavuni x 2.........Ball Jaggler Malota Soma alikuwa amekwisha mpiga chenga Sahau Kambi..........!!! Simba 2 Yanga 1! Namna gani hapa Ball Jaggler....!!!!" Akaja Jongo nae ".....goooo.....dah! anakosa bao hapa Mmachinga.....lo golden opportunity never come twice x2....! Hii hata kule Wembey ipo"
 
Nilikuwa napenda sana utangazaji mpira wa charlessssssssss Hilary.alikuwa anamvuto na bashasha za mpira...kweli siku hazigandi!
 
Duuu, nimeipenda signature yako : kuchagua CCM 2010 ni sawa na kufukia mashimo bila kuweka mbegu...utavuna nini?
 
Gang Chomba nimekumiss mzee, umepotelea wapi?

Acid mi nipo ila si unajuwa tena Ligi zoote zenye utimamu zilikuwa ktk kipindi cha mapumziko.

Sasa tutakutana tena hapahapa coz sie wengine hatuzuruli kwenye majukwaa ya watu huko sijui ya uchumi, siasa, jockes, malavidavi na majukwaa mengine.

Sie tukiingia JF ni jukwaa la michezo tu.
 
Wewe ulitaka nishabikie timu gani zaidi ya...
Abajalo
Yanga
Ac Milan?
Yanga si yangu, ni yako pia.
Yanga ni ya wazalendo wa Tanzania.
Yanga ndo Tanzania.

ASHANTI,SIMBA,FC BARCELONA! Mie huwa nashabikia Yanga hasa inapokuwa inafungwa,sababu ya kuwahurumia baba na mama yangu na Gang Chomba pia!!!!!!! teh teh....!
 
Enzi hizo Redio ni Moja tu RTD ya ukweli.
Sasa basi ilikuwa raha kusikiliza mpira halafu mshinde.
Na inayofuata hapa sasa ni nukuu ya kipande cha mwisho cha matangazo ya mpira wa Miguu kati ya Simba ya Dar es Salaam na Yanga ya Tanzania.

'''eeh Mafundi mitambo wetu ktk matangazo haya walikuwa ni Noel Namaloe na Edward Kwilasa.

Na kule ktk Gari yetu ya Matangazo alikuwepo Obi Mwambungu.

Mtangazaji Mwenzangu ni Omar Jongo, Mimi ni Charles Hillary, nawarudisheni Studio Barabara ya Nyerere kwake Nadhir Mayoka kwa ajili ya vipindi vinavyoendelea.

Kutoka hapa uwanja wa Taifa sina la ziada,
Yanga 2-0 Simba...Asanteni

Enzi za akina Charles Hilary Ahmed Jongo na Salim Mbonde ilikuwa...nawarudisha studio zetu za Pugu road kuendelea na matangazo mengine...then unamsikia Marehemu Michael Katembo anapokea matangazo...Nyerere road imekuja wakati hao watangazaji wengine wameshastaafu na Hilary alishaondoka RTD..
 
Nilikuwa napenda sana utangazaji mpira wa charlessssssssss Hilary.alikuwa anamvuto na bashasha za mpira...kweli siku hazigandi!
Jamaa bado ana mvuto huwa namsikiliza siku mojamoja idhaa ya kiswahili ya BBC akitangaza ligi kuu ya Uingereza, kupitia Kiss FM
 
Back
Top Bottom