Ukisoma hapa maisha kwako hayatakuwa mzigo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukisoma hapa maisha kwako hayatakuwa mzigo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 2, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna wakati ambapo huwa tunasema tunajaribiwa, tunapewa mitihani na mungu. Hali hii iko duniani kote na kwa kila binadamu kutegemea tu mazingira ya mitihani hiyo. Wakati huu ni ule ambapo kila tulicho nacho kama ulinzi wetu hujaribiwa. Huu ni wakati ambapo huwa tunayatazama maisha kama yasiyo na haki na yanayoonea au kutazama upande mmoja. Hiki ni kipindi ambapo imani zetu, thamani ya utu wetu, viwango vya subira zetu na uwezo wa kujizatiti hufikishwa kwenye ukomo, ambao tunadhani hatuwezi tena kuwa na vitu hivyo.

  Ukweli ni kwamba siyo kuwa watu walifanikiwa hawana au hawakupitia mitihani katika maisha, tena huenda wamepitia mitihani mizito kuliko wale ambao hawana mafanikio maishani mwao. Mahali ambapo hakuna matatizo ni kaburini tu, lakini kwenye maisha matatizo ni lazima kwa yeyote.

  Watu wanaofanikiwa kupitia mitihani ya maisha na wale wanaoanguka kabisa kufuatia mitihani hiyo hutofautiana katika jambo moja tu, jinsi wanavyoichukulia mitihani hiyo na wanachokifanya baada ya kukumbwa nayo. Kinachowatofautisha siyo kile kilichotokea, yaani mitihani bali wanavyotazama na kuchukulia kile kilichotokea na matendo yao baada ya mitihani hiyo kutokea.

  Ni wangapi kati yetu ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huchukulia mitihani hiyo kama mwisho wa maisha yao. Huanza kuchanganyikiwa na hata kuamua kujiuwa? Ni wangapi ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huanza kuwanyooshea kidole wengine kwamba ndio wamewasababishia matatizo hayo kwa kuwaloga au kwa njia nyingine? Ni wangapi ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huamua kuingia katika ulevi ili kupoteza mawazo? Bila shaka ni wengi, wengi, wengi sana, pengine ukiwemo na wewe.

  Hebu jiulize kama leo hii utapoteza kazi yako, utapoteza biashara yako, kuunguliwa na nyumba na kufiwa na mpendwa wako katika kipindi kisichozidi miezi mitatu, utafanyaje? Wengi wetu kwa kujifurahisha tunaweza kusema tutamshukuru mungu, lakini ukweli ni kwamba hatutakumbuka kama kuna Mungu na kama tutakumbuka, tutaishia kumtukana.

  Wale wanaoamini katika Uislamu au Ukristo watakubaliana nami kwamba, vitabu vitakatifu vya dini hizo vinahimiza kuwa tukubali kwamba yote mema na mabaya yametoka kwa mungu na yameletwa kwetu kwa sababu ya wema a siyo ubaya. Hili siyo suala la dini tu bali ndiyo ukweli wenyewe, kwamba hakuna tukio baya katika maisha.

  Kwa nini basi tusiamini kwamba matukio yote yanayotutokea huwa hayana nguvu ya kutuathiri hadi pale tunapoyapa tafsiri tuitakayo. Kama tukifukuzwa kazi, kwa nini tusilichukulia tukio hilo kama lile la kupata kazi. Huwa tunasema, "lakini hiyo ni vigumu" kwa sababu tumeshazoea kuyatafsiri matukio kwa mazoea tuliyolelewa au kukulia.

  Nakuomba kuanzia sasa ujaribu, kama uko kwenye mitihani ya maisha, jiambie kutoka ndani kabisa ya moyo, kwa kuamini kwamba utainuka tena, utaweza kusonga mbele, halafu uone matokeo yake. Kama utajiambia kwamba tukio hilo ni changamoto na linakusaidia kujirekebisha ni wazi utashangazwa na matokeo yake. Wewe hutakuwa mtu wa awali kushangazwa na matokeo yake bila shaka.

   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,669
  Trophy Points: 280
  Well said!But nikuulize swali la kizushi!Nini faida ya unachokifanya sasa?Faida yake ni leo au kesho?Usijibu kimazoea fikiria kwanza!
   
 3. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Mimi nimependa sociology yako hii, nadhani inasaidia kutafakari!
   
 4. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  haya mambo tumeyasoma sana kwenye mavitabu ya kisocial namna ya kufanikiwa na mambo katha wa katha yanayomsonga mwanadamu dail na utatuzi wake, lakin wapi life bado gumu kila kukicha,matatizo kibaaaao!?!?!
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mtambuzi .... Thank you.
   
 6. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  ashadii hujaangusha gari mpaka sasa? Manake tanesco wanaboa mgao huu hamna cha kufanya zaid ya kuvinjar na jf, huku ndo tunatolea machungu ya mgao
   
 7. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  ashadii hujaangusha gari mpaka sasa? Manake tanesco wanaboa mgao huu hamna cha kufanya zaid ya kuvinjar na jf, huku ndo tunatolea machungu ya mgao
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  ha ha ha... sikuwepo jamvini ndo naingia bana,
  wengine umeme uwepo usiwepo kama kawa...lol
  Naona kwako faida lkn... wa kuingilia JF unapata wapi?? (umeme)
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Haya mambo ni magumu na hayazoeleki. Ni rahisi kusema na kuwafariji waliokumbwa na mitihani ila ni ngumu sana kuyapokea maneno ya fraja kama yale ambayo siku zote tunawapa wenzetu.

  Ni bora tu kumshukuru Mungu kwamba walau hadi leo hayajakukuta au kama yalishakukuta basi yalikuacha salama bila kuingia kwenye orodha ya vichaa wanaoshinda majalalani!
   
Loading...