Ukisikiliza audio ya kocha wa Yanga, ameongea ukweli mtupu. Uongozi wa Yanga haupendi kuambiwa ukweli

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,517
Habari wadau,

Nimesikiliza Audio ya kocha wa Yanga maneno aliyoyasema ni ya kweli tupu. Mimi ni mwanayanga ila sijasikia sehemu akitutukana.

Viongozi wa Yanga wameibadilisha tafsiri ya maneno ya kocha ili walinde vibarua vyao na kujitetea maovu yao kwa mashabiki.

Kocha amesema anashangaa mashabiki wa Yanga wakiwa wanazomea hovyo hovyo tu kama sio binadamu wenye akili, kama nyani ama mnyama ambaye hana IQ.

Hii viongozi wa Yanga wameibadili na kusema amesema wanaYanga wote ni manyani.

Binafsi nimewai kuona mtu akiambiwa anaongea kama chiriku ila sijawai kuona akisema ameambiwa yeye ni chiriku.

Mtu anaambiwa ana tamaa kama fisi, aimaanishi yeye ameambiwa ni fisi

Viongozi wa yanga wajanja sana, wanajua madudu yao wamemuangushia kocha jumba bovu

Kocha huyu mzungu hajamsajili yikpe wala molinga wala mchezaji yeyote, sasa waliosajili madudu wanamuangushia jumba bovu.

Kwa maneno ya kocha Mkataba wa Yanga na kocha aliambiwa anapewa nyumba nzuri sehemu salama Dar, akaambiwa analipiwa DSTV, akaambiwa atalipiwe wireless internet ila Yanga hawajatimiza hata moja.

Walisema atapewa gari limsaidie usafiri Dar hajapewa.

Viongozi wamejaa uswahili Swahili kocha analalamika.

Sasa why wabadilishe maana.

Hoja inajibiwa kwa hoja, ilipaswa hoja za kocha zijibiwe kwa hoja kama je alitimiziwa masharti ya mkataba wake yote?

Sikiliza audio hapo chini kisha utoe hukumu.

Mchawi ya Yanga ni Msolla, Mkwassa na waswahili wengine.

Pongezi sana kwa Simba na Mo kwa kuachana na Waswahili na kuweka mzulu awaongoze.

Mbumbumbu

Mo.jpg
 
Kwahyo katika mifano yote akaona atumie mfano wa nyani, uyo ni mpumbavu tena mjinga Hana busara
Acheni kujificha kwenye hoja dhaifu hizo!! Jibuni hoja za msingi alizoainisha, yaani kuitwa CHURA, na mbongo mwezako ni sawa tu, ila mzungu kukufananisha na NYANI, kutokana na matendo yako amekudharirisha?!!! Ila viongozi wenu wanawafahamu uwezo wa mashabiki wao ndio maana wanaleta upuuzi kama huu na wanajua mtawa sapoti!!! Eti bila aibu afukuzwe nchini haraka kwa mamlaka gani waliyo nayo? Wewe umemfukuza kazi basi, hayo mengine sio yako,. JIBUNI HOJA HIZO KWANZA.
 
Kocha amesema anashangaa mashabiki wa Yanga wakiwa wanazomea hovyo hovyo tu kama sio binadamu wenye akili, kama nyani ama mnyama ambaye hana IQ.
Angeongelea tu hayo yanayohusu mazingira magumu ya kazi (usafiri, nyumba, viwanja vibovu, marefarii wabovu au wanapendelea), ingeweza kutosha na pengine hata angepata watetezi wengi tu. Hakuwa na sababu ya kufananisha mashabiki na nyani wakati anajua kuna upepo mbaya wa wabaguzi wengine wa rangi (sio yeye) ambao katika soka wamekuwa wakilitumia sana jina la nyani au kurusha ndizi uwanjani kwa blacks kuwalinganisha na nyani. Hapo ndipo alipochemka, na kwa kweli itamletea matatizo zaidi kama itafika huko juu kwa wenye soka
 
Kwanza inabdi ujue alikuwa na sababu gani kuwaa attack mashabiki kwa maneno makali km hawajaelimika, iQ zao ndgo km manyani blabla nyingi wakati ugomvi wake yeye ni kati ya viongoz wa timu na yeye na sio mashabiki. Kwanza hana busara principal za uongozi hajui ni mbaguzi dhahiri halina kukwepesha chochote. Na pia nataka nikujuze mm ni shabiki wa Simba tena damu ila apa nazungumza km muafrika mtanzania. Hajapangiwa nyumba,gari,dstv bla bla zote ila lakujiuliza mashabiki wanahusika vipi hapo je ndio waliotakiwa walipe hayo mahitaji yake au...kwa maoni yangu kakosea Sana tena sio kawakosea yanga tuu, kawakosea watanzania pia na waafrika kwa ujumla. Umaskini wetu usiwe sababu ya mpuuzi mmoja kutuongelea maneno machafu alafu avumiliwe.
Acheni kujificha kwenye hoja dhaifu hizo!! Jibuni hoja za msingi alizoainisha, yaani kuitwa CHURA, na mbongo mwezako ni sawa tu, ila mzungu kukufananisha na NYANI, kutokana na matendo yako amekudharirisha?!!! Ila viongozi wenu wanawafahamu uwezo wa mashabiki wao ndio maana wanaleta upuuzi kama huu na wanajua mtawa sapoti!!! Eti bila aibu afukuzwe nchini haraka kwa mamlaka gani waliyo nayo? Wewe umemfukuza kazi basi, hayo mengine sio yako,. JIBUNI HOJA HIZO KWANZA.
 
Kihistoria ubaguzi dhidi ya mwafrika anatumiwa nyani hivyo yalikuwa makosa makubwa maana nyani anatumika kumbagua mwafrika,angewafananisha wanayanga na mafisi au mnyama mwingne isingeleta madhara
 
alishawahi kutukana makocha weusi wa south africa,hawamtaki hata arudi tena huko,ni mbaguzi yule jamaa na mlalamishi sana
andika luc eymael vs komphella,hat ahabari ya yanga imeripotiwa sana south africa na wamefurahia jamaa hapendwi kule,hapa kuna siku hakupewa mkono na refa akalalamikia ubaguzi hata south alishafanya hivyo,mimi huwa namuona kama akili zake haziko sawa na hata viongozi wa yanga nayo ni mataahira hayajui yanachofanya
1.JPG

2.JPG
 
siyo mara ya kwanza kutukana huyu jamaa south africa hawamtai kabisa,huyuhuyu simba ilivyochukua ubingwa aliwapongeza haraka leo anasema yanga ni maskini ndiyo maana wanaonewa aisee senzo alifanya la maaana sana kukataa application yake alivyoomba kazi simba
Former PSL coach sacked after comparing supporters to ‘monkeys and dogs’
 
Kwanza inabdi ujue alikuwa na sababu gani kuwaa attack mashabiki kwa maneno makali km hawajaelimika, iQ zao ndgo km manyani blabla nyingi wakati ugomvi wake yeye ni kati ya viongoz wa timu na yeye na sio mashabiki. Kwanza hana busara principal za uongozi hajui ni mbaguzi dhahiri halina kukwepesha chochote. Na pia nataka nikujuze mm ni shabiki wa Simba tena damu ila apa nazungumza km muafrika mtanzania. Hajapangiwa nyumba,gari,dstv bla bla zote ila lakujiuliza mashabiki wanahusika vipi hapo je ndio waliotakiwa walipe hayo mahitaji yake au...kwa maoni yangu kakosea Sana tena sio kawakosea yanga tuu, kawakosea watanzania pia na waafrika kwa ujumla. Umaskini wetu usiwe sababu ya mpuuzi mmoja kutuongelea maneno machafu alafu avumiliwe.
Hiyo unayokimbilia ni inferiority complex!! Hapo kuwa masikini limeingia vipi? Nyie mashabiki amewapa makavu kutokana na kuwa mnawazomea baadhi ya wachezaji anapowanga, wakati yeye kama kocha anaona mchezaji anatimiza majukumu yake, kama alivyopewa, vile vile lawama nyingi mnawabebesha wachezaji, na benchi la ufundi bila kuangalia ubabaishaji wa viongozi wenu!! Mtu hajalipwa stahiki zake kama mkataba unavyosema, hilo hamulioni!!! Mnachotaka ni matokeo tu!!! Tatizo la ushabiki mandazi wa TZ, kila mtu anajifanya ana utaalam wa mpira, hiyo ni taaluma kama u daktari, utasikia ohooo pale angemuanzisha fulani, halafu kule chini akawa fulani, hii mechi tungeshinda huyo anayesema hivyo ukimpa mpira danadadana tu kupiga umpe hall la msimbazi center!!! Na hao mnaowaita wachambuzi wa soka ndio wanawaharibu tofautisheni PRE MATCH ANALYSIS, na POST MATCH ANALYSIS, Post match analysis kila mtu anaweza kwani mapungufu yameshaonekana!! Wangapi walijiingiza kwenye ukocha hadi wakashusha timu, lakini kwenye uchambuzi utadhania bonge la kocha!!! Ndio maana utakuta eti mtu anapendekeza MWL KASHASHA, Apewe timu ya taifa!!! Hahaaa, ushabiki mandazi bwana!! Ndio maana ni vigumu kwa kocha anayejitambua hasa mzungu kufundisha mpira wa bongo muda mrefu!! Kocha aje awape mataji yote utasikia sawa, lakini tuna taka sexy football!!! Huyu hatufai!! Akija wa sexy football utasikia sawa timu inacheza mpira wa kitabuni lakini, hatufungi magoli!!! Na viongozi wameshawaelewa aina ya mashabiki wala hawapati tabu!!! waambieni viongozi waache ubabaishaji.
 
Ni Bora ww umezungumza kwa facts mkuu maana kn mpuuz mmoja yeye anamtetea kwa upuuzi alioufanya, kwenye maisha nadhani ukidai haki yako isiwe sababu ya ww kuvunja sheria na taratibu Bali ni kufuata sheria na taratibu madhubuti ili kuipata haki yako sawia
alishawahi kutukana makocha weusi wa south africa,hawamtaki hata arudi tena huko,ni mbaguzi yule jamaa na mlalamishi sana
andika luc eymael vs komphella,hat ahabari ya yanga imeripotiwa sana south africa na wamefurahia jamaa hapendwi kule,hapa kuna siku hakupewa mkono na refa akalalamikia ubaguzi hata south alishafanya hivyo,mimi huwa namuona kama akili zake haziko sawa na hata viongozi wa yanga nayo ni mataahira hayajui yanachofanya
View attachment 1518452
View attachment 1518453
 
Naona Sasa yanga mnavuna mlichopanda. Alafu msimu ujao msipochukua kombe mbaki mkilialia Simba anabebwa.
 
Ukwel ni kwamba ata sijamaliza kuisoma ulichoandika, huenda ulichoandika kina maana sana ila kweny hili sio sehemu sahihi kuyazungumza hayo. Huyu jamaa amevuka mipaka. Sipingi Kuna mambo ya yanga wanazingua ila uyu jamaa amevuka mipaka amezingua na huo ndio ukwel

Back
Top Bottom