Hii mada ndio kulinda regase? Uharo mtupu huu.UKISIKIA URITHI NDO HUU
Tarehe 14/11/2021 kulikuwa na uchaguzi wa mzunguko wa pili wa Meya wa Prizren, ambao ni mji mkuu wa kihistoria wa nchi ya Kosovo. Katika uchaguzi huo wagombea wawili walioongoza kwenye matokeo ya mzunguko wa kwanza uliofanyika Oktoba 2021 walichuana ili kupata mshindi.
Shakir Totaj wa chama cha PDK aliibuka mshindi kwa 51.01% ya kura, akimbwaga mpinzani wake (ambaye ndo alikuwa Meya anayetetea kiti) bwana Mytaher Haskuka wa chama cha LVV, ambaye aliambulia 48.99% ya kura.
Ila aliyetia fora kwa sisi waTanzania ni mpiga kura aliyepiga kura hii:
View attachment 2012845
Hayati Dr. John Pombe Magufuli amepata umaarufu mkubwa duniani kutokana na sera yake ya kushughulikia tatizo la UVIKO. Sera ambayo imeonesha matokeo chanya kwa nchi ya Tanzania kuwa ni nchi pekee duniani ambako 99.99% ya raia walikuwa wanaishi kwa uhuru bila wasiwasi wowote kuhusu UVIKO na wanaendelea kufanya hivyo hata sasa.
Kwenye nchi za Ulaya (ambapo Kosovo ni mojawapo) suala la UVIKO limeambatana na ukosefu wa uhuru kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kutokana na jinsi serikali za bara hilo zilivyoamua kulishughulikia tatizo hilo.