Ukisikia urithi ndio huu; Mwananchi Kosovo ampa kura Hayati Magufuli badala ya wagombea waliokusudiwa

Mwanafalsafa

Platinum Member
Jun 24, 2007
662
851
UKISIKIA URITHI NDO HUU

Tarehe 14/11/2021 kulikuwa na uchaguzi wa mzunguko wa pili wa Meya wa Prizren, ambao ni mji mkuu wa kihistoria wa nchi ya Kosovo. Katika uchaguzi huo wagombea wawili walioongoza kwenye matokeo ya mzunguko wa kwanza uliofanyika Oktoba 2021 walichuana ili kupata mshindi.

Shakir Totaj wa chama cha PDK aliibuka mshindi kwa 51.01% ya kura, akimbwaga mpinzani wake (ambaye ndo alikuwa Meya anayetetea kiti) bwana Mytaher Haskuka wa chama cha LVV, ambaye aliambulia 48.99% ya kura.

Ila aliyetia fora kwa sisi waTanzania ni mpiga kura aliyepiga kura hii:

Magufuli.JPG


Hayati Dr. John Pombe Magufuli amepata umaarufu mkubwa duniani kutokana na sera yake ya kushughulikia tatizo la UVIKO. Sera ambayo imeonesha matokeo chanya kwa nchi ya Tanzania kuwa ni nchi pekee duniani ambako 99.99% ya raia walikuwa wanaishi kwa uhuru bila wasiwasi wowote kuhusu UVIKO na wanaendelea kufanya hivyo hata sasa.

Kwenye nchi za Ulaya (ambapo Kosovo ni mojawapo) suala la UVIKO limeambatana na ukosefu wa uhuru kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kutokana na jinsi serikali za bara hilo zilivyoamua kulishughulikia tatizo hilo.
 
UKISIKIA URITHI NDO HUU

Tarehe 14/11/2021 kulikuwa na uchaguzi wa mzunguko wa pili wa Meya wa Prizren, ambao ni mji mkuu wa kihistoria wa nchi ya Kosovo. Katika uchaguzi huo wagombea wawili walioongoza kwenye matokeo ya mzunguko wa kwanza uliofanyika Oktoba 2021 walichuana ili kupata mshindi.
Source ndugu au ni wewe upo huko?
 
Source ndugu au ni wewe upo huko?
Ndio yeye mwenyewe huyo anajitekenya na kucheka , mwenyewe, hakuna Mkosovo hapo ni TAGA hilo, makaratasi ya kura Ulaya huwa yanagaiwa na vyama kwenye kampeni mengi mengi tu , kwenye adress yako kila Chama kitakutumia hizo karatasi. Ila ukifika kwa wasimamizi siku yakupiga kura , pale utaingiza moja tu.
kwa hili TAGA linataka kutuona hatujaishi ulaya na hatujuhi kitu.
 
Hata Lucifer ni maarufu

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Habari.

Kuna watu waliimba na kuhubiri,
Kusujudu na kurukaruka.
Kunywa bia na kuponda bata la kufa mtu kwamba kwa maisha yao yatakuwa bora mno baada ya Magufuli.

Leo ni miezi 8 bila Magufuli lakini kila wakigeuka huku hakuna umeme, wakigeuka hakuna maji ,wakigeuka huku mbolea lakini moja, wakigeuka huku wanafukuzwa kwenye migodi ,wakigeuka huku wanafukuzwa kwenye mitaa, wakigeuka huku Mungu wao yuko jela kwa ugaidi.

Leo ndiyo wamejua Magufuli alikuwa anafanya kwa ajili yao?
Jinga kabisa na bado mtaendelea kuwa watumwa hivyo hivyo.
Waliowadanganya wamtukane Magufuli wote wamepata mabwana Ulaya wanalishwa bure.

Malipo ni hapa hapa duniani.
 
Back
Top Bottom