Ukisikia Ujasiri ndio huu Sasa, Angalia Hawa watoto wanachomfanyia mama yao mzazi aliye mgonjwa mahututi

Ingelikuwa nchi zingine polisi wangetaka picha ifutwe na wahusika wapo lupango sasa hivi ata kama mama yako mzazi shitaka human right law; breach of privacy and dignity.

Huko ni kumdhalilisha marehemu yeye mwenyewe alitaka kupigwa picha akiwa anaondoka au ata kama yupo hai katika hali ile.

Wizara ya afya ipo na polisi wapo; lakini hakuna kitachofanywa kutoa somo kwa wengine wasithubutu upuuzi wa aina hiyo mbeleni.
 
Hao wanafurahia urithi, wamechoka kumuuguza mama yao anayeonekana kaugua muda mrefu, nina wasiwasi hata chakula walikuwa hawampelekei; ukute alikuwa akiuguzwa na ndugu wengine. Mwisho wao watagombania mali na watafarakana milele. Na hizo mali hazitadumu maana zina laana ya mama!
 
Hivi kuna ujinga kuzidi huu waliofanya? Hawa wameji-judge wenyewe na hakuna mtu aliyewa-judge.
Yawezekana kweli walichokifanya siyo sawa lakini kuwajudge kuwa walikuwa wanafurahia kifo cha mama wapate mali it is too far.
 
Yawezekana kweli walichokifanya siyo sawa lakini kuwajudge kuwa walikuwa wanafurahia kifo cha mama wapate mali it is too far.
Kama nilivyokujibu: wameji-judge wenyewe. Ni wenyewe wamekwenda too far na kuachia watu wafanye conclusion wanayotaka. Nikuambie: Lile gharofa lililoungua Uingereza miaka siku za nyuma na kuuwa watu lilileta sokomoko sana baada ya baadhi ya watalii kuwa wanakwenda pale kupiga selfie. Hii ni baada kabisa ya tukio lakini watu wengi wanakasirishwa kwa sababu ilionekana kama siyo ubinadamu. Kuna mifano mingi sana ya watu wengine mpaka wamefukuzwa kazini baada ya kupiga selfie na maiti au watu wanaogua. Hawa watoto wa huyu mama waliofanya hili tukio ni washenzi wa kiwango cha juu. Tena wanaonekana kabisa ni watu wazima. Kweli mama yako yuko hoi hospitalini anakaribia kufariki wewe unapata ujasiri wa kujipiga selfie na kisha uipost kwenye mitandao ya kijamii? Wangekuwa ndugu zangu ningewachapa fimbo kwani wameaibisha familia nzima.
 
MALEZI MALEZI MALEZI.......

Wahenga walikuwa na misemo iliyotafsiriwa kama methali, baadhi ya hizo methali ni;

1. Samaki mkunje angali mbichi
2. Mtoto wa nyoka ni nyoka
3. Utavuna ulichopanda
Nakadhalika wa kadhalika

Niache walengwa hapo juu niongelee jamii kwa upana ninayoiona mimi wewe na yule kila siku tunapotoka kuzunguka duniani na kurudi majumbani mwetu. Utakuta wazazi hawajishughulishi na malezi ya watoto wao, watoto wanakuwa huku wanalelewa kwa simu na camera baadhi wakipitia magausigeli vibonzo na wengine madereva an hausi boyi ambao wanajenga roho za kutokujali kwa watoto, roho za kutokuwa na huruma maana wanaoshinda na watoto hawawaoneshi huruma zaidi ya ubabe.

No wonder mama yuko mahututi watoto wanaenda kumuona dakika za mwisho, hawakumbuki hata kumshika shindo vizuri asiumie, au wampe walau maji akate kiu hata kumsemesha masikioni tuu kama anawasikia au hata kumshika mikono kumuonesha mama tuko pamoja....

Mzazi kama hukumfunza mwanao namna ya kuenenda akiwa humu ulimwenguni kwa kutenda mema kwa wengine na kwa ajili yake, kamwe usitegemee akutendee mema utapohitaji akufanyie hivyo.

Bibi K.
Sio kila samaki anastahili kukunjwa. Unaanzia wapi kumkunja perege😁

Methali husika husema hivii:-
"kambale mkunje angali mbichi"
 
Kama nilivyokujibu: wameji-judge wenyewe. Ni wenyewe wamekwenda too far na kuachia watu wafanye conclusion wanayotaka. Nikuambie: Lile gharofa lililoungua Uingereza miaka siku za nyuma na kuuwa watu lilileta sokomoko sana baada ya baadhi ya watalii kuwa wanakwenda pale kupiga selfie. Hii ni baada kabisa ya tukio lakini watu wengi wanakasirishwa kwa sababu ilionekana kama siyo ubinadamu. Kuna mifano mingi sana ya watu wengine mpaka wamefukuzwa kazini baada ya kupiga selfie na maiti au watu wanaogua. Hawa watoto wa huyu mama waliofanya hili tukio ni washenzi wa kiwango cha juu. Tena wanaonekana kabisa ni watu wazima. Kweli mama yako yuko hoi hospitalini anakaribia kufariki wewe unapata ujasiri wa kujipiga selfie na kisha uipost kwenye mitandao ya kijamii? Wangekuwa ndugu zangu ningewachapa fimbo kwani wameaibisha familia nzima.
Ondoa hasira, fikiri nje ya box.
Last moment ya mama yao mpendwa wameweza kui document.

Wengi hamtanielewa na kudhani nawatetea, la hasha najaribu kuibua fikra fikirishi.
 
Ondoa hasira, fikiri nje ya box.
Last moment ya mama yao mpendwa wameweza kui document.

Wengi hamtanielewa na kudhani nawatetea, la hasha najaribu kuibua fikra fikirishi.
Una-document last moment ya mtu anayefariki halafu una-share kwenye social media? Ukiitwa idiot utakasirika? Halafu unajiona kweli ''umefikiria nje ya box''?
 
Una-document last moment ya mtu anayefariki halafu una-share kwenye social media? Ukiitwa idiot utakasirika? Halafu unajiona kweli ''umefikiria nje ya box''?
Usikimbilie kutukana! Usiegemee kwenye fikra kosoefu.
Najua hujawahi kufiwa na mzazi wako.

Laiti ungejua uzito wa neno "buriani" (a moment you wish to reverse)
 
Usikimbilie kutukana! Usiegemee kwenye fikra kosoefu.
Najua hujawahi kufiwa na mzazi wako.

Laiti ungekua uzito wa neno "buriani" (a moment you wish to reverse)
Sijatukana hata kidogo. Kufiwa na mzazi hakuna uhusiano wowote na kujipiga selfie na mtu aliye kwenye mateso makali tena karibia na kifo halafu una-share kwenye social media. Angalau wangebaki na hiyo iwe kumbukumbu yao lakini siyo kupost dunia nzima ione mama yao anavyoteseka na wenyewe wako busy kujipiga picha. Hii siyo hulka ya kibinadamu. Kuna namna nzuri zaidi na ya heshima ya kuchukuwa kumbukumbu.
 
Unawezaje kumsaidia kupunguza maumivu ya mtu anayekufa!

Usihamaki tafakari kwa kina.
 
Kuna watu wanaujasiri wa khali ya juu sana

Hivi unapata wapi nguvu za kupiga selfie ukiwa unatabasamu na mama yako aliye mgonjwa mahututi kiasi hiki na bado kafa unapost picha hiyohoyo mtandaoni.

Picha inajieleza kabisa mama anapambania uhai wake angalia sura za watoto🤔

Angalia picha ambatanishi, ungekuwa wewe ungeweza?

Tujifunze matumizi sahihi ya mtandao

Sidhani ni ukweli itakuwa mambo ya nigeria movie
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom