Ukisikia paaa

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
761
252
''Ukisikia paaa jua imekukosa, aliyepiga amefanya makosa'', ni nini hii, ni risasi.

Kuna kitu kimoja kinakera sana, nilijaribu kuuliza nikaambiwa si hitilafu ni makusudi tu, kitu hicho ni mlio wa pikipiki unaosikika kama risasi, wajuvi wanasema kuna kitu waendesha pikipiki wanafanya wanapoingiza gia namba mbili kutokee mlio wa risasi.

Kinachokera ni usumbufu wanaopata watu hasa wazee, wajawazito na watoto lakini hata baadhi ya wagonjwa na wasio wagonjwa milio hiyo inastusha kama hukuitarajia, tunaomba vyombo husika vitoe onyo kama jambo hili linafanyika makusudi. Mwenye ujuzi zaidi juu ya hili atuelimishe zaidi kama ni hitilafu au kusudi, nawatakia siku njema.
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,208
8,681
Kero za mijini hizo.
Kuna baadhi ya mafundi uchwara wanafanya modification kwenye exhaust na kuzifanya itoe mlio abnormal, hata mimi naboreka sana na kelele zile.
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,831
4,230
''Ukisikia paaa jua imekukosa, aliyepiga amefanya makosa'', ni nini hii, ni risasi.

Kuna kitu kimoja kinakera sana, nilijaribu kuuliza nikaambiwa si hitilafu ni makusudi tu, kitu hicho ni mlio wa pikipiki unaosikika kama risasi, wajuvi wanasema kuna kitu waendesha pikipiki wanafanya wanapoingiza gia namba mbili kutokee mlio wa risasi.

Kinachokera ni usumbufu wanaopata watu hasa wazee, wajawazito na watoto lakini hata baadhi ya wagonjwa na wasio wagonjwa milio hiyo inastusha kama hukuitarajia, tunaomba vyombo husika vitoe onyo kama jambo hili linafanyika makusudi. Mwenye ujuzi zaidi juu ya hili atuelimishe zaidi kama ni hitilafu au kusudi, nawatakia siku njema.

hakuna chombo husika cha kushughulikia kero hii, wako bize na kero zenye rushwa nyingi na si huu ujinga wa bodaboda
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom