Ukisikia kuchoka kwa watanzania basi ni huu mkasa wa jana katika ofisi ya Kinondoni

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
Source: ITV news

Jana jioni kuliripotiwa kuzuka kwa vurugu la kukata na shoka kati ya raia na mgambo wa manispaa ya Kinondoni katika ofisi za mkuu wa wilaya hiyo. Chazo ni baada ya mgambo kumshambulia raia moja ambaye walimkuta akisubiri daladala katika kituo hicho na kumfaninisha na chinga waliyekuwa wakimtafuta. Baada ya mgambo hao kutembeza kichapo cha mbwa mwizi kwa raia huyo, wananchi hawakuridhika na upumbavu huo ndipo wakajibu mapigo kwa mawe na kila silaha iliyopatikana. Hizi ni dalili za kuchoka na vitendo vy auonevu.
 
Hawa 'mgambo' hawajatambua kwamba wao wanatumiwa kwa manufaa ya 'wakubwa', kuwakandamiza na 'kuwaweka sawa' wanyonge. Huu ni ule mfumo wa 'divide and rule', lakini ipo siku ambayo (Toba Yarabi!) wasio-nacho 'watachoka kabisa' na kuamua kushika sime, mapanga, mishale, upinde, mikuki, marungu na mashoka, na kuanza kuwavamia walio-nacho, wakianzia kwa vibaraka wao, ambao ni askari polisi, mgambo, na wengineo.

Kinachotokea Kenya ni vita kati ya wasio-nacho na walio-nacho. Mali nyingi za matajiri zimeteketezwa, maduka na majengo yamechomwa moto, watu wameporwa magari yao, wamevamiwa nyumbani mwao. Maeneo kama Westlands, Eastleigh, Lavington, Kyuna, na kwingineko, wenye-nacho ambao ni watu wanaomiliki magari ya kifahari wanaogopa kuyaendesha, kwa kuhofia kuvamiwa na wasio-nacho ambao wanaranda mitaani na silaha zao za kijadi, wakiwawinda walio-nacho.

Hawa mgambo wawe makini, kwani iko siku yatakuja kuwakuta. Wao pia ni wanyonge, lakini hawajapevuka kisiasa. Hawajui kwamba wanatumiwa tu... hako ka-mshahara kao kadogo ndiko kanakowafanya wawapore raia wengine ambao maisha yao ni ya duni, huku wenye-nacho wakichekelea na kuomba waendelee hivyo hivyo. Kama wangetaka waache, si wangewapa mishahara inayostahili?

Akina Kanali Massawe waache unafiki; kama ni suala la uhalifu, basi na hao askari mgambo walioiba mali halali za wamachinga wakamatwe, wachunguzwe na washtakiwe mahakamani.

Tuache unafiki!
 
Back
Top Bottom