Ukishtakiwa Mahakama ya Kimataifa (ICC)gharama za kuhudhuria kesi nani analipa?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,372
Wakuu,

Naomba Kufahamishwa;

Mosi,Iwapo Afisa fulani au mtu Fulani kutoka nchi yoyote ile mwanachama wa Mahakama ya kimataifa(ICC) iliyopo The Hague,Uholanzi ameshtakiwa na inatakiwa kufika mahakamani hapo je Gharama za kwenda huko nani analipa?

Tuchukulie mfano Afisa wa Polisi Tanzania anatakiwa kuhudhuria kesi Kule na hana nauli inakuwaje?

Nakumbuka hapo Kenya wale watuhumiwa walikuwa wanaitwa 'The Ocampo four' ambapo miongoni mwao alikuwepo Rutto na mtangazaji mmoja wa Redio ambao walikuwa wakihudhuri kesi na kurudi Je zile gharama zilikuwa zinalipwa na nani?

Pili,iwapo umekamatwa na kushikiliwa huko The Hague,Je gharama za mavazi nani anagharamia,tuchukulie Kiongozi wa waasi amakamatwa hakujiandaa akasafirishwa na ana mavazi yake aliyovaa tu,anapohudhuria Mahakamani,Je atavaa nguo hizohizo kila mara au kuna kuna utaratibu gani?

Naomba ufafanuzi.
Asante
 
Kwenye ule Mkataba wao wa The Hague, unaonesha gharama zote zitalipwa na Serikali ya nchi husika ambayo Mwalifu anatoka. Ndo mana Makosa yanayoshtakiwa kule ni yale Makosa yenye maslahi mapana na nchi. Kitaalam wanaita 'rem publicam'
 
Ikiwemo gharama za mawakili wa utetezi kwa mtuhumiwa?
 
Wanalipa wenyewe ICC ,refer kesi ya Uhuru kenyata na rutto...walikusanya mashahidi wenyewe na kuwahifadhi nchi tofauti , wanalipa mawakili wanaokutetea, wanakupa makazi na kila kitu...all cost wanakacover wao......
 
Reference Uhuru Kenyatta: alishtakiwa kama mtu binafsi na ilibidi akabidhi Nchi kwa Ruto na kwenda kule kama individual.

Serikali inachoweza kusaidia kama utakaidi kwenda ni kukukamata then ICC wanakuja kukubeba kwa gharama zao
 
Aisee kumbe ndivyo ilivyo,ndio maana naona huwa wanapiga suti tu,
Asante kwa maelezo
 
Swali zuri.....! Wapi Amsterdam atusaidie hapa ndo kwa kuonyesha umahili na kuzoa points..! Popote alipo atafutwe
 
Reference Uhuru Kenyatta: alishtakiwa kama mtu binafsi na ilibidi akabidhi Nchi kwa Ruto na kwenda kule kama individual.

Serikali inachoweza kusaidia kama utakaidi kwenda ni kukukamata then ICC wanakuja kukubeba kwa gharama zao
Asante,na hizo gharama ambazo ICC inatumia wanatoa wapi?au ni michango ya wanachama wake
 
Asante,na hizo gharama ambazo ICC inatumia wanatoa wapi?au ni michango ya wanachama wake
ICC is funded by member states.

Additional funding inatoka kwa voluntary contributions kutoka kwa baadhi ya Serikali. Kwa mfano, kama Russia inamuona Magufuli kama kikwazo, inaweza kutoa mchango mkubwa wa hiari then ikapenyeza agenda chini ya carpet kuzusha kesi tu. Is it clear now?😊
 
ICC is funded by member states.

Additional funding inatoka kwa voluntary contributions kutoka kwa baadhi ya Serikali. Kwa mfano, kama Russia inamuona Magufuli kama kikwazo, inaweza kutoa mchango mkubwa wa hiari then ikapenyeza agenda chini ya carpet kuzusha kesi tu. Is it clear now?
 
Back
Top Bottom