Ukishangaa ya musa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukishangaa ya musa

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by vukani, Mar 10, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi unajua kisa cha huu msemo wa "ukishangaa ya Musa utakutana na ya Firauni?

  Haya ungana na mimi katika simulizi ya kisa hiki……

  Hapo zamani sana enzi za himaya ya Firauni (Farao) kulikuwa na mivutano ya kimamlaka kati yake na Musa.(Yule Musa anyesimuliwa katika Biblia, aliyewatoa wana wa Israel kule utumwani Misri na kuwapeleka katika nchi ya ahadi)
  Firauni alikuwa akishidana na Musa ambaye alikuwa akiongozwa na Mungu.
  Basi ilikuwa ni kawaida watu kwenda kwa Firauni kupeleka mashauri yao inapotokea kutofautiana.


  Firauni alikuwa akitolea maamuzi mashauri hayo, ambapo maamuzi yake mengi hayakuwa na haki na yalijaa utata mtupu. Lakini ikatokea baadhi ya watu wakawa hawaendi tena kwa Firauni kwa kuwa walipoteza imani kwake na badala yake wakawa wanaenda kwa Musa ambaye alikuwa akisifika sana kwa kutoa maamuzi ya haki na yaliyokubalika na pande mbili.

  Basi ilitokea mtu mmoja alikuwa akisafiri kwa miguu, kutoka mji mmoja kwenda mji mwingine, na kama unavyojua zamani kulikuwa hakuna usafiri wa magari au ndege, sana sana ilikuwa ni ngamia tu.

  Wakati akiwa njiani akiendelea na safari yake alijisikia njaa na kwa mbali aliona shamba la mahindi, alipofika katika shamba hilo akakata mahindi mawili matatu na kukoka moto pale pale shambani na kuyachoma kisha akala na baada ya kushiba akaondoka zake na kuendela na safari yake…
  Mara mwenye shamba akafika katika shamba lake na kukuta kuna mahindi yame katwa na kuchomwa pale pale shambani na kuliwa, akaamu kufuatilia nyayo za mwizi wake..

  Yule mtu alikuwa akiendelea na safari yake bila kujua kuwa kuna mtu anamfuatilia nyuma.
  Wakati akiendelea na safari yake mara akaona njiwa mzuri aliyenona yuko juu ya mti, akaokota jiwe na kumrushia yule njiwa na kumpiga sawia.
  Akamchukua na na kumchinja, shida ikawa ni wapi atapata moto ili amchome njiwa wake na kumla.

  Alipoangalia kwa mbali aliona kuna moshi unafuka, akaamua kuufuata ule moshi mpaka akatokea kwenye kijumba kimoja cha masikini mmoja na mkewe, alipobisha hodi akatoka mama moja mjamzito kwenye hiyo nyumba. Mama huyo alikuwa peke yake kwani mumewe alikuwa hayupo alikwenda kuhemea kijiji cha jirani.
  Yule mama alikuwa amekoka moto nje ya nyumba kwa ajili ya kupikia, yule bwana akaomba ambanike njiwa wake, akaruhusiwa.

  Wakati anambanika yule njiwa alikuwa akinukia ile mbaya, kiasi cha kumtamanisha yule mama mwenye mji,lakini kutokana na kutomjua yule bwana akaogopa kumuomba.
  Basi yule bwana alipomaliza kubanika njiwa wake na kuiva akaaga zake na kuondoka huku akitafuna njiwa wake na kuendelea na safari.

  Huku nyuma yule mama kutokana kutamani sana yule njiwa akapata uchungu sana kwa kitendo cha yule bwana kuondoka bila hata kumpa kipande cha nyama,na kutokana na kuwa na kisirani na hasira mimba ikatoka.
  Mumewe aliporudi akamkuta mkewe amelala nje ya nyumba akiugulia kwa maumivu ya tumbo,alipomchunguza akagundua kuwa mimba imetoka.

  Alipomdadisi, mkewe akamsimulia kisa cha yule mpita njia na njiwa wa kubanika kuwa ndio sababu ya mimba kutoka. Yule bwana akawa anamuhudumia mkewe, na mara yule bwana aliyeibiwa mahindi katika shamba lake akafika pale na kukuta yale matatizo, na baada ya kusimuliwa habari ya mpita njia na njiwa wa kubanika ndipo na yeye alipoeleza kisa cha kuibiwa na mahindi na kumtuhumu mpita njia na njiwa wa kubanika kuwa ndiye muhusika.

  Ikabidi waungane muibiwa mahindi na yule, mkewe aliyepoteza ujauzito kumfuatilia yule mpita njia.
  Hawakwenda umbali mrefu wakamkuta mpita njia amejipumzisha chini ya mti akipunga upepo, wakamkamata na kumweleza makosa yake, mpita njia akajitetea kuwa hakuiba mahindi bali alikata na kuchoma pale pale shambani kutokana na njaa na kuhusu mimba kutoka alikanusha kuhusika kwa sababu yeye alijichomea njiwa wake na kujiondokea zake baada ya kuruhusiwa na yule mama mwenye nyumba na wala hakujua lililotokea nyuma yake.

  Wale watu hawakumuelewa na wakakata shauri wampeleke kwa Musa ili kumshitaki.
  Walipofika kwa Musa, wote walisikilizwa kila mtu kwa nafasi yake na baadaa ya Musa kutafakari akatoa hukumu kuwa yule bwana aadhibiwe kwa kuchapwa bakora kisha aondoke zake….

  Duh!! Ile hukumu haikuwaridhisha wale jamaa, ikabidi waende kwa Firauni, wakitegemea kupata haki zaidi kwani hukumu ya Musa waliiona kama imempendelea yule mpita njia.

  Walipofika kwa Firauni, kama kawaida yake aliwasikiliza wote kila mtu kwa nafasi yake, kisha akatoa hukumu.

  Hukumu nyenyewe inasemaje…soma hapa chini…

  Firauni akasema yule mpita njia akabidhiwe shamba avune mazao yote kisha apande upya na kuyatunza mpaka yafikie katika hatua kama ile aliyoikuta ndipo amkabidhi mwenye shamba lake. Na kuhusu yule bwana ambaye mkewe alipoteza ujauzito, akasema yule mke akabidhiwe kwa mpita njia akakae nae mpaka apate ujauzito, ukishafikia miezi kama ile iliyotoka amrejeshe kwa mwenyewe….

  Duh!!! Jamaa wakachanganyikiwa na ile hukumu wakaondoka pale kwa Firauni kimya kimya na wakamua kumsamehe mpita njia kwani hakuna aliyekuwa tayari kutekeleza ile hukumu.
  Na hapo ndipo ulipozuka msemo wa "Ukishangaa ya Musa utakutana na ya Firauni"
   
 2. Pilato2006

  Pilato2006 Senior Member

  #2
  Mar 10, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  imetulia
   
 3. o

  omwana Member

  #3
  Mar 10, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imenichekesha saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana tu jamani!!!!!
   
 4. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,694
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  ha ha very nice lol lakini mi nilikuwa najua huu msemo umetokana na ile story ya kwenye bible pale Musa alipoenda kwa Firauni na kumuomba awaachie wana wa israel wakamtumikie Mungu wao naye akasema toa ishara Musa akaweka fimbo yake chini ikageuka nyoka watu wakashaaa maajabu ya musa lkn firauni akaauru waganga wake na wenyewe wafanye mambo nao wakaangusha fimbo zao na kugeuka nyoka watu wakashangaa tena haaaa


  "am just thinking"
   
 5. senator

  senator JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hahahaha Vukani hii imesimama..duh nilikuwa siyajui haya atiii:D:D
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160

  ....Utastaajabu ya Firauni.
  It is very nice.
   
 7. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Babu nimekukubali
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mi nikitazama naona wote wawili Musa na Firauni walikuwa bogus katika maamuzi yao!..Musa nae, how come mtu aliyetenda kama huyu mgeni aadhibiwe kuchapwa viboko?
  Anyway, ni hadithi hii!
  Aksante Mkuu!
   
 9. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,657
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  PJ tupe uamuzi wako ingekuwa wewe ungefanyaje!??
   
Loading...