Ukishangaa nguvu ya mafisadi kwenye uspika, utazimia kwenye baraza la mawaziri.


Mwangaza

Senior Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
198
Likes
2
Points
33

Mwangaza

Senior Member
Joined Feb 26, 2008
198 2 33
UKISHANGAA nguvu ya mafisadi kuhakikisha wanamuweka speaker atakayewalinda, UTAZIMIA ukisikia baraza la mawaziri. Kwa mwenye kusoma nyakati ameshajua kina nani watakuwa mawaziri, kina nani watakuwa wakuu wa mikoa,kina nani watakuwa wakuu wa wilaya na kinanani wataingia bungeni kwa kuteuliwa. Hapo kazi ni kulindana kulindana tu, ni kuhakikisha wanakula mpaka ukoko na kuficha wananchi wasijue wa kuruhusiwa kuyajadili.

Nani alaumiwa hapo?? Si sisi wenyewe tumewaruhusu watuongoze?? si wenyewe tumewapigia kura wakaingia bungeni watuibie vizuri??

Nchi imeshauzwa hii, ohoo ..hamkuona hata kura zao za moni walivyopitisha wenye uwezo wa kutoa rushwa zaid, na rushwa ikabarikiwa na kiongozi wao. Sasa hapo cha kushangaa ni nini hapo? kama tuliona kwenye kura za maoni mapemaa , lkn tukawachagua tena! Sasa TUTEGEMEE MAUMIVU ZAID YA JANA.

Wadau, hivi mnategemee mkuu atamlinda askari mwaminifu, wakati na yeye ni mtuhumiwa..ahaa wapi hilo haiwezekani. Atakachofanya ni kumpoteza kila anayengia kwenye anga zao. NA HAYO NDIO TUNAYOYAONA NA TUTAKAYOENDELA KUYAONA.
 

KAPONGO

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
1,401
Likes
195
Points
160

KAPONGO

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
1,401 195 160
Itakuwa kinyaa na kichefuchefu km watu kama akina masha, wataingia mjengoni kwa mlango wa nyuma wa uteuzi wa Rais...na yatakuwa ni matusi ya nguoni kwa umma
 

Kiti

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
237
Likes
12
Points
35

Kiti

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
237 12 35
Tunamsubiri Mramba arudi bungeni kwa dirisha dogo la usajili. Hivi Kingunge naye atarudi? Toka niko shule ya Msingi namsikia Kingunge mbunge, waziri. Sasa niko karibu miaka 50 bado yumo tu. Tumesikia mambo aliyofanya ubungo terminal lakini atarudi tu, ndo kashika hirizi ya Chama cha Mafisadi
 

Forum statistics

Threads 1,204,948
Members 457,641
Posts 28,177,752