Ukishafikisha miaka 20 na kuendelea na bado unawategemea wazazi kwa asilimia 100, umekwisha

Mnataka kufananisha life style ya mbele na nchi zetu, bado tuna hatua za kupiga tufikie kiwango hicho cha kuwafanya vijana 20's wajitegeme, zaid zaid tutazalisha majambazi tukifosi
Unajua mtu akisema, nataka mwanangu akifika umri fulani aanze kijitegema, hali ya kuwa hajamuwekea misingi thabiti, ni sawa na kupiga kelele tu.

Inabidi kijana aandaliwe kujitegemea.
 
Mzazi anayetegemea mtoto ajitegemee katika 20's bila kumuandalia mazingira anakuwa hatimizi majukumu yake. Pia mazingira yanatofautiana familia kwa familia. Na kila mtu ana wakati wake wa kusimama peke yake.

Ungesema kuwa akiwa na miaka 20's na bado ukawa umeridhika na maisha ya nyumbani kwenu na huna mpango wowote wa kujitegemea, hapo kweli tatizo lipo.

Tutiane moyo, maana naamini hakuna kijana aliyekamilika anayefurahi kumtegemea mzazi wake maisha yake yote.
 
Unajua mtu akisema, nataka mwanangu akifika umri fulani aanze kijitegema, hali ya kuwa hajamuwekea misingi thabiti, ni sawa na kupiga kelele tu.

Inabidi kijana aandaliwe kujitegemea.
Unaongelea mtoto huyo atoke familia inayojiweza kimtindo, mara nyingi familia masikini watoto wenyewe binafsi maisha ndiyo yana washape kuwa na mfumo wa kujitegemea
 
Mwanangu akishafikisha 23 na anajielewa..nitamtoa kwangu hata kwa tarumbeta.
Kiuhalisia hatatakiwi kuwafukuza , inatakiwa tuwatengenezee mazingira na kuwashauri kujitegemea na kuwajenga ili wawe na shauku ya kujitegemea na waondoke nyumbani wenyewe.

Pia baadhi ya wazazi waache tabia za kulazimisha baadhi ya watoto kuwakatalia kuondoka nyumbani kisa tu inaonekana Kama vile mtoto anawakimbia wazazi hii nayo c tabia nzuri kwa mustakabali Wa maisha ya badae ya mtoto
 
Unajua mtu akisema, nataka mwanangu akifika umri fulani aanze kijitegema, hali ya kuwa hajamuwekea misingi thabiti, ni sawa na kupiga kelele tu.

Inabidi kijana aandaliwe kujitegemea.

Acheni kukwepesha mada, hoja sio kusimama kimaisha... bali ni ile kuanza kujitegemea.

Hii sio lazima iwe kutoka familia bora, kijana aanze kuwa yeye... hata inapobidi sapoti apete lakini sio 100%.
 
Back
Top Bottom