Ukisema Jini tayari kuna majini miatatu karibu yako. Kila mtoto mchanga huguswa na jini dakika moja bada ya kuzaliwa. Vitabu vya dini vinasemaje?

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,809
6,081
UHUSIANO ULIOPO KATI YA BINADAMU NA MAJINI, UNAJUA VITABU VYA DINI VINAWAZUNGUMZIAJE MAJINI?

VIUMBE MAJINI NI NINI?NA WANAFANYA NINI?VIPI MAHUSIANO KATI YA MAJINI NA BINADAMU? VITABU VITAKATIFU VINAZUNGUMZIAJE HILI SUALA?

Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa Moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita.
Viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;

Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.

Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vile

vile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.
Taifa la Majini limegawanyika katika makabila Milioni Sabini na mbili (72,000,000) na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka.

Idadi ya Majini ni kila Binadamu mmoja kuna Majini 300 na wanaishi katika Majumba yetu, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa.

Majini wako katika aina Mbili (2); Maruhani na Mashetani.
Maruhani ni Majini wema ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na wanawasaidia Binadamu katika mambo mengi.
Mashetani ni Majini Waovu ambao ni wakorofi na wanawaletea Watu madhara na Matatizo mara kwa mara.
Baba wa Majini anaitwa JANN ambaye kimaumbile yeye ana tofauti ndogo na wenzie kwamba yeye ameumbwa kwa ulimi wa Moto.

Pamoja na mambo mengi wanayoyafanya Majini na kujihusisha na binadamu, Majini vilevile wanafanya kazi za Malaika hasa zile za mambo ya kupeleka Habari na kuwalinda Binadamu, mambo ya doria za Angani. Kazi hizi siyo zao lakini kwa vile wanapenda kuiga mambo basi huiga hata kazi ambazo siyo zao.

Majini na Binadamu wana sifa zinazofanana kwani wote wana akili na wote watahesabiwa siku ya Kiama na watazawadiwa kwa mema yao na maovu yao, wote wanakula na kuzaa.
Kama ilivyo, kuna wataalamu wa Kijini wenye fani sawa na Wataalamu wa Kibinadamu wenye kufanya kazi zinazofanana.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya Majini na Binadamu ni kwamba; Majini hawana maumbile maalum na wana uwezo wa kujibadilisha katika maumbile mbalimbali ingawa wengi wa Majini wapo katika maumbile ya paka, nyoka na ndege.
Binadamu wao wana umbile maalum ambalo halibadiliki.
Majini wana uwezo wa kuwaingia Binadamu wakati Binadamu hawana uwezo wa kuwaona Majini isipokuwa kwa ufundi maalum.

Namna Majini wanavyowaingia Binadamu iko katika njia tatu:-
1.
2. Njia ya kwanza (1): ni kama Remote Control; Hii inamfanya yule aliyedhibitiwa kuweza kuelewa au kuwa na fahamu zake lakini anakuwa hawezi yeye mwenyewe kuudhibiti mwili wake na anasema yale anayotaka yule Jini.
3. Njia ya Pili (2); Jini humwingia Binadamu ndani ya utosi na kuingia katika Mfumo wa Damu. Hii inamfanya yule Binadamu kupoteza fahamu na anakuwa haelewi kabisa kinachoendlea na anafanya yote anayotaka yule Jini.
4. Njia ya Tatu (3) ni ile ya Jini kukaa nyuma ya Binadamu. Njia hii humfanya yule Binadamu anakuwa hapotezi fahamu ila anakuwa hawezi kufanya lolote na mwili wake.

{mospagebreak}

Majini vilevile wana uwezo wa Kusafiri kwa kasi ya upepo bila kutumia chombo chochote; Binadamu hana uwezo huo isipokuwa kwa msaada wa Majini.

Hiyo ni kusema kwamba mambo yote yanayofanywa na Wachawi na Wanga hayawezekani isipokuwa kwa msaada wa Kijini.

Jambo la muhimu ni kwamba pamoja na uwezo mkubwa walionao Majini, Wanadamu wana uwezo wa Kumtawala na Kumdhibiti Jini na vivyo hivyo Majini nao wanaweza kumtawala na kumdhibiti Binadamu wote kwa kutumia utaalamu maalum.
Wako Majini wa kila Dini na kila Kabila, na kuna watu wanaofuga Majini kwa kujikinga, na kwa kuboresha kazi zao au kujipatia utajiri. Pia kuna watu wanaofunga ndoa na Majini kwa kutumia utaalamu au kwa hiari za Majini hao.

Wabaya wa Majini ni Mashetani ambao wengi hawana Dini na ndio wanaoharibu mimba za Wazazi na kufanya mapenzi na watu usingizini bila hiari zao.
Kuepuka usichafuliwe kimapenzi, kabla ya kulala piga Bismillahi kwa Muislamu au taja jina la Yesu mara tatu kwa Mkristo.

MAUMBILE YAO YAKOJE?


• Majini wana maumbile makuu manne (4);
• Wanakuwa katika maumbile ya Nyoka.
• Wanakuwa katika maumbile ya Nge.
• Wanakuwa katika maumbile ya Mbwa.
• Wanakuwa katika maumbile ya Paka (Mweusi).
• Kuna Majini wengine hawana maumbile yeyote na hawa shughuli yao ni kuruka hewani kuzunguka huku na kule na husafiri mbali kwa mara moja yaani kufumba na kufumbua.


SURA ZA MAJINI NA MASHETANI:

Majini sura zao ni za kutisha na mfano wake ni kama Matunda ya Mti wa Zaqum ambao unatoa matunda yenye sura mbaya na yanayofanana na mawe.
Majini wanakuwa na mkutano kila siku nyakati za kuchomoza na kuzama Jua na nyakati hizo ndizo ambazo wanafanya maasi yao.

Fitna na Maasi yao mengi wanafanyia upande wa Mashariki.
Majini vilevile wanaweza kujigeuza kama mbwa mweusi au paka mweusi kwa sababu Majini wanapenda Rangi Nyeusi kwa sababu ya kiza.

WANAKULA NINI?

Subscribe uzi huu mengi hujayajua bado


Itaendelea

Asalaam kudo
 
Mkuu Kudo naweza pewa ushahidi mwingine kua Mungu alianza kuumba majini kabla ya binaadamu?
Usitumie Quran
 
Kabla sija comment chochote naomba tu niseme kuwa hakuna jini mzuri NEVER hapo ni Sawa na kusema kuna mganga na mchawi eti kisa mganga anaweza kukusaidia ndo umuite mzuri usisahau wote wanafanya kazi ya shetani hata kama wanamuomba Mungu katika kazi zao still wao ni wabaya tu maruhan,mashetani,waganga,wachawi,freemasonry, wote ni shetani katika vitengo tofauti
 
Ila majini tuna wa-Overrate mno, sisi binaadam ni bora kuliko malaika na majini. Ukifanikiwa kufungua Sixth sense of organ na third eye baasi hakuna kiumbe kitakacho kusumbua. Mungu katupa uwezo mkubwa binaadam kuliko viumbe vyoote endapo tu mtu ukijitambua wewe ni nani..
Ndio maana sayanyi ya majini ni Primitive haiendelei lakini yetu inakua kila kukicha
 
Elimu hii umeipata katika kitabu gani ?
Ninavyojua mimi, hakuna Jini zuri au jema hata moja, yote ni maovu na hayamsadii binadamu zaidi ya kumharibu.
Umesoma vitabu vingapi kuhusu majini?!
Kifupi Ni kwamba ili uyajue mengi kuhusu vilivyoko katika dunia hii iwe kwa kusoma ama kuona lazima kuwe na garama yake hivyo si kila kitu utajua kirahisi eti kwa kusikia ama kuamini unajua ya kuwa iko hivi ama vile

Mimi sijui vyote bado nahitaji kujifunza hivyo basi kama unajua chochote kuwahusu unaeza kuweka hapa tufaidike wote kuliko kuja kama kusuta hivi

Siri ya maarifa mengi ipo katika kitabu cha dini ambacho ni Quran na Bible na huwezi kuyajua mengi kama hujaviweka pamoja vitabu hivi
 
Mkuu Kudo naweza pewa ushahidi mwingine kua Mungu alianza kuumba majini kabla ya binaadamu?
Usitumie Quran
Ukinilimit namna ya kukujibu sitaweza kukujibu,ila tambua ya kuwa majini waliishi hii dunia katika miaka mig nyuma kabla ya uwepo wa mwanadamu na alijengea himaya kubwa ya utawala katika enzi ya Jann na Jadda,
Kuumbwa kwa mwanadamu kwa udongo ni kama kureplace kuumbwa kwa mwanadamu kwa Moto ambapo mwanadamu wa udongo amekuja kuwa juu ya moto na nadhani waona moto hauwezi kuwaka juu ya udongo ila udongo huweza kukaa juu ya moto

Soma taratibu nilichokujibu utaelewa kwa sababu gani moto umekuwa wa kwanza kuwapo duniani kabla ya udongo
 
Umesoma vitabu vingapi kuhusu majini?!
Kifupi Ni kwamba ili uyajue mengi kuhusu vilivyoko katika dunia hii iwe kwa kusoma ama kuona lazima kuwe na garama yake hivyo si kila kitu utajua kirahisi eti kwa kusikia ama kuamini unajua ya kuwa iko hivi ama vile

Mimi sijui vyote bado nahitaji kujifunza hivyo basi kama unajua chochote kuwahusu unaeza kuweka hapa tufaidike wote kuliko kuja kama kusuta hivi

Siri ya maarifa mengi ipo katika kitabu cha dini ambacho ni Quran na Bible na huwezi kuyajua mengi kama hujaviweka pamoja vitabu hivi
Hapana mimi sijasuta
Nilikuwa nauliza tu na kama ni siri yako basi.
Unajua vijana wasomi wa siku hizi hawataki kudanganywa jambo, wanataka unapoleta mada flani unaweka na chanzo cha hiyo habari.
Isije habari hiyo ikaonekana kama ni uzushi wa mtaani tu, kama Jini ni Zuri weka ushahidi wa maandiko yaliyoasisi huo uzuri wa Jini.
La sivyo wasomi hawatakuelewa kabisa.
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom