Ukirusha mshale, ukasikia 'Chwiiii chwiiiii!' Jua umempata:iko hivyo bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukirusha mshale, ukasikia 'Chwiiii chwiiiii!' Jua umempata:iko hivyo bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Jul 13, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Wenyeji wa mikoa ya kati hata ile ambayo uwindaji ni moja ya shughuli zao. Wanamsemo usemao,"Ukirusha Mshale Usiku Mawindoni,ukisikia chwiiii!" Jua umempata mnyama uliyemlenga. Hali hii ni dhahiri kabisa katika vikao vya bunge linaloendelea Dodoma. Wabunge wa upinzani hususani wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi wamekuwa wakirusha mishale ambayo mawaziri na wabunge wa CCM wamekuwa wakilia, "Chwiiiiiiiiiiiiiii, Chwiiiiiiiiiiiii, chwiiiiiiiiiiiiiiii !" Hali hii inaonesha bayana mishale inawapata.

  Hoja ya ufisadi na mafisadi katika akaunti ya EPA ilipotolewa kwa mara ya kwanza bunge lililopita, wabunge wa CCM wakiongozwa na spika wakati huo, Mh. Sitta wakazomea. Spika akasema hayo ni majungu.

  Hoja ya posho katika bunge liendeleao imewainua takribani mawaziri na wabunge wote wa ccm. Wakasimama kupinga hoja hiyo kwa nguvu zao zote.

  Katika kikao cha jana, Mh. Kafulila (NCCR) amesema,'serikali ni legelege'. Kauli hiyo ilisababisha mawaziri zaidi ya watatu kuomba mwongozo kwa spika.

  Mh. Maalim Seif pia amepongeza CDM na NCCR kwa hoja ya posho walioisimamia kidete, hadi kieleweke.

  Nawapongeza wabunge wa upinzani (nina maanisha, CHADEMA na NCCR-Mageuzi) kwa kulenga ipasavyo mishale na mikuki yao. Maana kila mkuki na mshale waliouchagua wakiurusha mlengwa hulia chwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii !
   
 2. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Umenena.
   
 3. Chigwiyemisi

  Chigwiyemisi JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 531
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Imetulia
   
 4. M

  Msharika JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  umekuna vizuri
   
 5. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  halielenga ana shabaha na ajafanya makosa...
   
 6. R

  Rajakulanga Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii imetulia, ccm hawana msimamo... na hata huyo Sitta haeleweki kama CCJ!!!!!!!!!
   
 7. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mkuu samahani, masahihisho kidogo, ungeandika hivi "Aliyelenga ana shabaha na hajafanya makosa"
   
 8. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 322
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maalim Kawaeleza Wazee wenziie, wabia katika serekali kuwa Serekali ije na hoja ya nguvu kuhalalisha Posho......na akatoa mfano kama yeye ni makamo wa raisi na analipwa mshahara kwa kazi hiyo na moja kati ya kazi zake ni kushiriki vikao vya baraza la mapinduzi jee...sasa yeye analipwa posho ya nini kwa kushiriki vikao?
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Upo sawa kabisa sasa Wapinzani rusheni mishale ya sumu utaskia chwiiii mara moja tu
   
 10. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Haya maneno wanayajua magamba ndo maana gamba sita jana usiku aligonga meza kidogo azimie maana angewekwa hewani kwa ujinga wake
   
Loading...