Ukiritimba wa Tanesco sasa kwisha

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
WAKATI gumzo kuu nchini kwa sasa ni juu ya hali mbaya ya kifedha ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) mazungumzo yanaendelea kuhusu Tanesco kukodisha sehemu ya mfumo wake wa gridi ya taifa ya usambazaji umeme kwa kampuni binafsi ya kimataifa ili iusambaze katika mikoa ya kusini.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk. Idris Rashid, aliyathibitisha hayo jana na kueleza kuwa shirika hilo kwa sasa linashauriana na kampuni ya Canada ya Artumas Group Inc., kuhusu mkataba wa muda mrefu wa ukodishaji miundombinu ya usambazaji umeme.

Chini ya makubaliano ya miaka 20 yanayojadiliwa sasa, Artumas itakodi miundombinu ya usambazaji umeme katika mikoa ya Mtwara na Lindi na kuwapatia wateja umeme.

Hii itakuwa mara ya kwanza Tanesco inakodisha miundombinu yake kwa kiwango kikubwa hivyo tena kwa muda mrefu kwa kampuni binafsi.

Mtwara na Lindi ni mikoa ambayo ina eneo la Kilometa za mraba 24,000 na wakaaji wapatao milioni 2.

Taarifa kamili za ukodishaji huo bado hazijapatikana, lakini maofisa wa serikali wamesema ukodishaji huo utaisaidia kifedha Tanesco inayokabiliwa na ukata.

Kwa sasa Tanesco ina ukiritimba wa biashara wa sekta ya umeme na lengo hilo la serikali la kuunda taasisi tatu tofauti za kufua umeme, kuusafirisha na kuusambaza bado liko mbali kutimia.

Haijaeleweka vizuri ni lini majadiliano baina ya Tanesco na Artumas yanatarajiwa kukamilika.

Vilevile haijafahamika kama kampuni hiyo ya kigeni ya Artumas itaweka viwango vyake vya kulipia umeme au itaendelea kutumia viwango vinavyotozwa na Tanesco vilivyoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

Tanesco inazalisha megawati 560 za umeme nyingi zikiwa kwa nguvu ya maji na pia inanunua megawati 200 za umeme kutoka kwa wazalishaji binafsi.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,008
3,666
Nadhani ni wazo zuri sana ila cha kutizama ni hawa artumas wapi wanapoendesha shughuli kama hizo na kama zipo zinaendaje? na wapi wamewahi kukodisha na kuendesha shughuli za umeme? Hilo ndio muhimu isije ikawa Richmond nyingine.

Nadhani ni wazo zuri ukichukulia kuwa, hakuna shirika katika mashirika yote tuliyokuwa nayo, tuliyotaifisha na tuliyoanzisha wenyewe ambalo limenifanikiwa, mimi silijui na kama lipo basi lipo-lipo tuu kama ilivyo Tanesco. Bora tuyakodishe kwa wenye uwezo wa kuendesha shughuli hizo kuliko kung'ang'ania kitu ambacho hatukiwezi. Alimradi tu kuwe na mikataba ya wazi na itazamwe vizuri tusije tukaishia sisi tuliokodisha ndio tunawalipa waliokodisha.

Halafu mbona kuna wazo linakuja kuwa hatuna cha kuwakodisha ila ni kausanii kamaneno tuu haka? Tunawakodisha nini? si tuseme kweli tunawaachia waendeshe shughuli hizo, sisi zimetushinda. Nadhani hapa inaonesha neno kubinafsisha linaumiza roho za watu wengi ndio maana linaanza kutumika neno kukodisha.

Hivi Tanesco kuna nini cha kuwakodisha hawa Artumas?
 
Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
321
65
WAKATI gumzo kuu nchini kwa sasa ni juu ya hali mbaya ya kifedha ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) mazungumzo yanaendelea kuhusu Tanesco kukodisha sehemu ya mfumo wake wa gridi ya taifa ya usambazaji umeme kwa kampuni binafsi ya kimataifa ili iusambaze katika mikoa ya kusini.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk. Idris Rashid, aliyathibitisha hayo jana na kueleza kuwa shirika hilo kwa sasa linashauriana na kampuni ya Canada ya Artumas Group Inc., kuhusu mkataba wa muda mrefu wa ukodishaji miundombinu ya usambazaji umeme.

Chini ya makubaliano ya miaka 20 yanayojadiliwa sasa, Artumas itakodi miundombinu ya usambazaji umeme katika mikoa ya Mtwara na Lindi na kuwapatia wateja umeme.

Hii itakuwa mara ya kwanza Tanesco inakodisha miundombinu yake kwa kiwango kikubwa hivyo tena kwa muda mrefu kwa kampuni binafsi.

Mtwara na Lindi ni mikoa ambayo ina eneo la Kilometa za mraba 24,000 na wakaaji wapatao milioni 2.

Taarifa kamili za ukodishaji huo bado hazijapatikana, lakini maofisa wa serikali wamesema ukodishaji huo utaisaidia kifedha Tanesco inayokabiliwa na ukata.

Kwa sasa Tanesco ina ukiritimba wa biashara wa sekta ya umeme na lengo hilo la serikali la kuunda taasisi tatu tofauti za kufua umeme, kuusafirisha na kuusambaza bado liko mbali kutimia.

Haijaeleweka vizuri ni lini majadiliano baina ya Tanesco na Artumas yanatarajiwa kukamilika.

Vilevile haijafahamika kama kampuni hiyo ya kigeni ya Artumas itaweka viwango vyake vya kulipia umeme au itaendelea kutumia viwango vinavyotozwa na Tanesco vilivyoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

Tanesco inazalisha megawati 560 za umeme nyingi zikiwa kwa nguvu ya maji na pia inanunua megawati 200 za umeme kutoka kwa wazalishaji binafsi.

Kinachotakiwa ni mkataba ambao ni wazi, na uliojadiliwa kwa kina na wadau wa sector husika. Wananchi waelimishwa juu ya mpango husika, usiingie kinyemela na kusababisha pengine maumivu mengine kwa Watanzania. Na huu mpango utakuwa mzuri tu pale ambapo bei ya umeme itapungua kwa mtumiaji na upatikanaji wake kuwafikia watu wote million 2 wa mikoa hiyo.
 
Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
15

Ni mpango mzuri kama utasaidia wananchi wengi kumudu gharama. Tatizo la tanesco ni kushindwa kukusanya madeni sababu hawana orodha kamili ya wateja. SOmetimes private company nakuwa serious sio business as usual. Sayansi na technolojia tunakoelekea kama hatuna umeme wa wananchi wengi basi tutakuwa na maendeleo ya kurudi nyuma badala ya mbele.
 
Lusajo

JF-Expert Member
Feb 25, 2008
456
30
Yaani mimi nilivyosikia ni Kampuni ya Canada nikajua imewahi kufanya kazi sehemu zingine za dunia, kumbe inafanya kazi zake Tanzania tuu. Wahindi wengi tuu wanakaa Canada kwa hiyo ni rahisi kwa wao kuanzisha kampuni na kuiita jina lolote halafu kuchukua tenda Tanzani. Halafu ni mkataba wa miaka 20 kwa hiyo kama kampuni ni kimeo tutaisubiri mpaka miaka 20 ipite na itakuwa inaendelea kula hela tuu, kwa sababu hao watu wenyewe ambao wana saini mikataba sijui kama wana akili nzuri au ni "special". Tanesco inabidi kuwa makini sasa hivi.
 
Akili zao kama za CHENGE
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom