Ukipokea ukumbuke kuna siku utatakiwa Utoe

Chemwali

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
397
178
loh Binadamu bwana kwa kusahau,nina harusi ya mdogo wangu,tukapatana wenyewe wana familia tuchomoane till tuwe na kianzio,sasa ili kutunisha mfuko nikasema on my side i hate michango(kwakuwa maisha ni magumu na wengi wanachukia) nitadeal na wale niliowachangia ..loh wenye fadhila wamerespond hao wengine unaona kama mtu anataka kujikausha..sitawadai ila ukumbuke ulipokula so usisahau kurudisha...michango ya harusi siku hizi ni DECI ukichangisha ndivyo utakavyorudisha
 
Watz tubadilike, mambo yakuchangisha watu tuachane nayo. Mbona enzi za wazazi wetu walikuwa wanakomaa wao wenyewe? Hivi tunashindwa nini kubadilika? Nachukia sana michango hasa nikikumbuka maisha yanyuma yalikuwa magumu kwani wengine mungu anajua tu, halafu mtu anajua unafanya kazi sasa anakuletea kadi kila kukicha haya sio mambo kabisa. Nikula uso wa mbuzi tu, bora nimsaidie mwenye shida ya matibabu au shule kuliko harusi.
 
Nami nina usemi kama wako lakini watu hao hao wanaoumia kutoa ndio walinichangisha hadi harusi za jirani zao na vipaimara vyao juu
 
Ambao hawajafunga ndoa miongoni mwa wanabodi hili waongoze njia kwa kufanya harusi zisizo na gharama ya kufa mtu.
 
kwa Tanzania hii, na hasa Dar michango ya harusi huwezi kukwepa hata ufanyeje, ninachoshauri ni kwamba jikune unapofikia maana usipoangalia mshahara wako woote unaishia kwenye michango ya harusi
 
pole ndugu...

kuchangia sana sio guarantee kwamba siku ya siku watakuchangia.... ni kujitia umasikini tu
 
Back
Top Bottom