Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 353
KKN wewe unapendekeza faini iwe kiasi gani? Mimi nadhani labda iwe 40,000.
Nakubaliana na wewe kabisa kwa kiwango hicho kuwa hapa UK ambako uchumi wake uko juu sana kulinganisha na nyumbani, faini ya kosa kama hilo haizidi pound 60!
Lakini bado najiuliza polisi wametumia vigezo gani ku arrive kwenye hiyo figure? As far as I know, ajali nyingi bongo zinasababishwa na 'drink drive' na wengi mtakubaliana na mimi kuwa very little is being done to stop this. Nenda Rose Garden, Brake Point au Makumbusho Ngwasuma ikipiga uone jinsi car parks zilivyojaa- and almost 90% ya wenye magari wanakanyaga mtungi kwa kwenda mbele bila kujali and no one cares,inaonekana ni kitu cha kawaida tu!
Bado kuna tatizo la watu kuendesha magari barabarani wakati hawajui sheria hata kidogo, na hili kwa kiasi kikubwa nitawalaumu polisi kwa kuwa ukiwa na hela yako hata kama hujui kuendesha- utapata leseni! Ukivunja sheria ukitoa rushwa- unaendelea na safari yako! Bado kunamadereva kibao wanaondesha daladala na mabasi ya kwenda mikoani kwa kutumia leseni feki na polisi wanajua hili!
And mbaya zaidi Rais mwenye kila ikitokea ajali mbaya ya barabarani, badala ya kuja na mikakati ya kupunguza ajali hizi -anaishia tu kusema 'ajali haina kinga', 'kazi ya mungu haina makosa'!