Domo Kaya
JF-Expert Member
- May 29, 2007
- 531
- 60
Majira
Na Rehema Mwakasese.
Jeshi la Polisi nchini kupitia kikosi cha Usalama barabarani, limepiga marufuku madereva kupokea simu au kupiga simu wakati wakiendesha magari na watakao bainika kufanya hivyo watatozwa faini ya sh, 200,000/= papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kikosi cha usalama wa Barabarani , Bw. James Kombe, alisema zipo sababu nyingi zinazosababisha ajali barabarani ikiwemo madereva kupokea au kupiga simu wanapoendesha magari.
Kamanda Kombe alisema watu wengi wamekuwa na tabia ya kuendesha magari huku wakizungumza na simu, hivyo husababisha ajali za kizembe.
Alisema askari wa Usalama Barabarani wataanza operationi hiyo mara moja kwa kushirikiana na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA).
Mbali na hilo Kamanda Kombe alisema madereva wanaondesha magari yaendayo mikoani waongezwa muda wa kuendesha magari usiku ambapo mwisho utakuwa ni saa sita na si saa nne.
Alisema kuwa mwanzo madereva walikuwa wanaendesha mwisho saa nne, lakini wameona abiria wengi wanalalamika ndio maanda wakaongeza hadi saa sita, ili waweze kufika mapema zaidi.
Pia alisema kuanzia sasa dereva wa basi la abiria atapewa leseni la daraja 'C' akiwa na umri wa miaka 30 na mwisho wa kuendesha ni miaka 60.