Ukipewa timu ya AZAM utafanyaje ili angalau iwe kama TP Mazembe

swa
Timu za simba na yanga mtazamo wangu simepewa Muda wa kutosha na zimethibitisha zaidi ya majungu, marktime za kisoka na Maneno maneno hazitatufikisha popote...

Nilipoiona AZAM na bosi tajiri yuko nyuma yake nikasema afadhali angalau tumepata team ambayo itakwenda hadi club bingwa duniani icheze na wakina Madrid au Barca.

Lakini kila nikiichungulia naona haina uwezo wa kuvuka siasa za simba na Yanga.

Mimi sio mpenzi wa soka ila ni mfuatiliaji wa karibu kila kitu kinachoendelea nchini.

Unadhani nini kikifanyika team ya tajiri huyu iwe angalau kama TP mazembe.

SWALI ZURI SANA.

Kwanza kabisa AZAM Watafute kocha mwenye profile kubwa sana kuliko AZAM na pia kocha mzuri (binafsi wachukue makocha kutoka nchi hizi mbili German na France. Sababu ni kwamba nimegundua makocha wa hizo nchi mbili wanawajua sana kuwatumia wachezaji wa kiafrica vizuri na mbinu za kiafrica wanazijua vizuri pili kocha aje kable ya msimu kuisha yaani zimebaki match 10 basi kocha awe ameshakuja ili aangalie wachezaji anaowataka hata kama wataingia hasara aje akae mwaka mzima ili kwanza asome wachezaji wote wa kitanzania na uchezaji wao huku akifuatilia kwa karibu soka la nchi zingine. kingine fungu la usajili apewe yeye na yeye ndiye ataamua mchezaji wa kumsajili hata kama atasema fukuza 10 leta 10 msikilizeni halafu mtakuja kuniambia
 
Ni kufumua benchi la ufundi lote,kocha,waswahili wote nafukuza.
Naleta kocha mwenye cv iliyoshiba,naajiri watu ambao hawafungamani na hizi timu za kurithi kutoka misri na south africa..
Pesa nyingi nawekeza kwa wachezaji wenye majina makubwa...nanunua kutoka klabu kubwa kama Mazembe,alahly,mamelod,na club zingine kubwa nachukua wachezaji hatari barani africa ili kuimarisha timu iwe kubwa kwa nguvu ya pesa kama Mancity&Psg.
Wachezaji wa ndani nakuwa nawatoa kwenye academy wanapandishwa timu ya wakubwa kidogo kidogo.
Hata ufanyaje bongo grains za Simba na yanga haziishi hata uwalete watu wa nje ,tff inaziogopa Simba na yanga ,ni rahisi tff kuwakata point timu zingine kama Azam lakini si kwa simba na yanga,mwisho wa siku timu kubwa zinabaki zile zile mbili
 
Huu ni upumbavu wanaofanya Tff kama vipi timu zingine zifutwe zibaki hizo mbili wanazozisujudia.
 
Kitu kingine kikubwa kinacho push timu kufanikiwa ni fanbase kubwa

Azam hata wakifungwa hakuna presha wala hasira kutoka kwa mashabiki.

Ningeshauri timu zote ligi kuu na madaraja ya chini kuanzisha matawi na mifumo ya wanachama, hiyo ndio njia rahisi zaidi ya kutengeneza local fanbase.
 
Timu za simba na yanga mtazamo wangu simepewa Muda wa kutosha na zimethibitisha zaidi ya majungu, marktime za kisoka na Maneno maneno hazitatufikisha popote...

Nilipoiona AZAM na bosi tajiri yuko nyuma yake nikasema afadhali angalau tumepata team ambayo itakwenda hadi club bingwa duniani icheze na wakina Madrid au Barca.

Lakini kila nikiichungulia naona haina uwezo wa kuvuka siasa za simba na Yanga.

Mimi sio mpenzi wa soka ila ni mfuatiliaji wa karibu kila kitu kinachoendelea nchini.

Unadhani nini kikifanyika team ya tajiri huyu iwe angalau kama TP mazembe.
Iache kuingilia ushabiki wa Simba na mwenzake Yanga baasi. Iajiri mtu kama senzo (neutral) asiyekuwa na upande kati ya Simba na Yanga
 
Uza wachezaji wote halafu kanunue wa TP Mazembe.
Simple tu
Jina linawaangusha....inatakiwa wabadili jina.....au wabadilishane majina na Yanga au Simba...Yaani wachezaji walewale lakini timu iitwe Yanga au Simba utashangaa inaweza ikachukua ubingwa wa Ligi kuu
 
Back
Top Bottom