Ukipata kazi Dar na mkoani ndani huko utachagua ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukipata kazi Dar na mkoani ndani huko utachagua ipi?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by mkonowapaka, Nov 20, 2010.

 1. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Habari za leo wandugu

  Juzi kati apa kuna jamaa yangu alipata kazi kampuni za simu 2 tofauti. Moja ilimuajiri kwa nafasi ya hapa Dsm na nyingine ilitaka impeleke huko Sumbawanga... Tofauti ya mishahara ilikua kama laki 1 tu i mean ile ya mkoani ilizidi kwa laki 1. Jamaa akaikataa ile ya mkoani akabaki Dar, hakuwa na ishu yoyote hapa Dar ya ziada...!

  Mimi nilishamshauri, wewe ungemshauri vp aende porini au abaki mjini!?
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  kama kwenye pay slip ya sumbawanga ilizidi laki 1 in real life ilizidi laki hata 3. Life in sumbawanga +other towns upcountry is cheap. Ukiingia hutamani kutoka.
   
 3. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,097
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  pamoja na hayo mkuu, life in remote areas ina matatizo yake washikaji zako wanaweza kuwa wale wanywa gongo maarufu in that place, given that you'll be having money with no life challenges unaweza kuishia kubaya sana.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mimi niko uko uswekeni mnakokusema yaani marafifki zako ni RC, DC, RPC sasa kaa Dsm utaona kama waweza mingle na hao watu.

  Huku uswekeni unaweza save b'se maisha ni cheap then unaenda spend Dsm wakati wa likizo.

  DSM kuna joto, foleni na karaha za hapa na pale
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mkuu please usikuite uswekeni na wa Dar - Yombo Buza, Charambe etc aiteje?

  Ndiyo raha ya mkoani hiyo, mshahara ukiwa ni kuanzia laki nne tu, rafiki zako ni RC, RPC, RAS, DAS, DC, OCD. hulali njaa. Na hali ya hewa ni murua kabisa.
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  itakuwa ajabu utoke dar uende mkoani ku-grap kazi ya U-Afisa Mtendaji wa Kijiji au Afisa Mtendaji wa Kata. Maana hapo kwenye blue pana -portray kazi hizi-kukimbizana na wapika gongo na wanywaji wake.
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  inategemea na mtu binafsi anavyoyachululia maisha, na jinsi anavyotaka maisha yake yawe, Mwingine nje ya kazi anataka ajishughulishe na biashara za hapa na pale, maduka (nguo, vifaa vya ujenzi, nk), bar nk.

  Sasa wengi wa hao wanapenda kuwa katika miji mikubwa ili ku-monitor biashara zao, wengine ule mshahara anaopata unamtosha na hajaamua kuwa maisha yake yawe wapi, hivyo huyo yuko radhi kukaa kokote, na wengine ni watu wa starehe kila weekend ni kujirusha tu hivyo mjini kwake ni poa zaidi

  Hapa hakuna formula kila mtu na utashi wake tu
   
 8. B

  Brodang Member

  #8
  Nov 20, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DaTZ TRUE KITUKO
   
 9. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mikoani ni kuzuri kwa kutafuta pesa na dar ni kuzuri kwa kutumia pesa.

  Kwa sasa ningemshauri aende mkoa akakusanye pesa ili aweze kuja kuitumia jijini dar hapo baadae. Isitoshe mikoani matumizi si makubwa ukilinganisha na dar na pia hali ya hewa bado ni nzuri.

  Mwambie anunue laptop na moderm ya zantel ili aweze kupata japo huduma ya internet akiwa huko mkoani


   
 10. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Umefika Yombo buza au huko Charambe ? au unasifu mahala kwa uzuri wa jina, like Regeant Estate,Oysterbay etc

  Grow up dude...??!!
   
 11. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,283
  Trophy Points: 280
  Hiyo ya Sumbawanga bado ipo? i have great ideas for cellphone companies especially in rural areas...
  please answer me ASAP! sijali ni kampuni gani..na hata kama mshahara utashushwa to the sam ya huo wa Dar..pse!!!
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  stupid, didi I ever mentioned regent estate or oysterbay?
   
 13. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,770
  Trophy Points: 280
  Huyo ni mwehu.............. atakufa na tai shingoni........ Fikiri hili...........

  Kuna watu wa kampuni za simu wapo mikoani............siku walipopata nafasi hizo walisita sana.....lakini leo hii ukiwaambia warudi Dar hawataki hata kusikia..........Hao jamaa ni ma-Engineer.........sababu za msingi kwao kukataa kurudi Dar ni hizi..........
  1. Akiwa huko ana usafiri ambao 100 percent of time analo yeye.......... hebu fikiri akitoka asubuhi kwenda Kirando wale abiria waliochwa na SUMRY wote wake.............. mara kwenda na kurudi ..............HAGUSI MSHAHARA

  2. Ofisi yake ni gari alilonalo amabalo linajazwa mafuta na kampuni............. anajipangia mwenyewe aende mnara gani na lini........pamoja na kwamba kuna wakati atapigiwa simu na NETWORK MANAGEMENT CENTRE (NMC or NOC) lakini ana uhuru wake.

  3. Kula vijiwe vyao ni pamoja na ma RPC, wakuu wa wilaya, wakuu wa matrafic nk

  4. Heshima yao ni kubwa sana huko kiasi kwamba huduma za kijamii kwao ni meremko

  5. Bei ya vyakula (say maziwa pale njia ya kuelekea KARAGWE LITA 5 NI Tshs. 2000/= wakati huku dar hiyo ni bei ya lita moja)

  WAKITOKA HUKO MKONI WANAKUJA KUWANUNUA WOOTEE NA KAMA UMEPANGA NDO UNANUNULIWA PAMOJA NA NYUMBA
   
 14. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,770
  Trophy Points: 280
  Kwa huku Dar hakuna wanywa Gongo........??? Ndugu.....Ulaya ni popote swala ni hela.............. unaweza ukaishi polini kabisaa lakini ukawaleta FM akademia waje wapige nyumbani kwako
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,770
  Trophy Points: 280
  Vile vile wengi wa wanaomention uzuri wa DAR ni wale wanaoishi nyumba za ajabu msasani maandazi road IN THE NAME OF GHOROFA LA JIRANI........... NAWEZA NIKAISHI MANZESE NA NIKAYAFANYA MAZINGIRA YANGU YAKAWA YA DUNIA YA KWANZA..............
   
Loading...