Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,522
- 24,010
Juzi jioni nmetoka zangu town nikapita mitaa ya kona bar mida ya saa tatu hivi. Muda nao ulikuwa umeenda kiasi ila nikawaza kila siku nasikia changu changu leo ngoja nijipatie hata mmoja nionje wakoje. Maana kuna jamaa yangu hata kuoa hataki anasema yeye akijisikia hamu anaenda anapata changu basi maisha yanasonga mbele.Basi nami nikaenda nikakamata changu mmoja. Jaman changu ni watamu sana tena nlipata mkavu kabisa. Nikamla hivi hivi sikutaka hata kutumia kitu kingine. Nikagonga wawili then ndo nikaagiza ugali nikala na changu mwingine tena. Yule mama anayajua mambo acha kabisa. Changu alikuwa amekaangwa na kuungwa na pilpil kidogo tangawizi na vitunguu swaumu. Kwan hata nlikumbuka nyumbani? Niliwagonga wale changu kwa ugali nikashushia na pepsi baridi ndo huyo nikaanza kuelekea home. Miaka yote nakula samaki sato,kibua na wengine wengine ila nmeonja changudoa sasa siachi.