Ukiondoa wastaafu wanaosubiri mafao yao, ni kundi gani jingine linaisoma namba zaidi?

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
4,874
2,000
Binafsi naona wastaafu ndio kundi pekee waliomaliza kuzisoma namba zote hapa duniani.

Kuna wastaafu wengine wana miaka 2,3 n.k hawajalipwa stahiki zao.

Kila siku wakienda PSSSF wanaambiwa bado hiki, wakikamilisha hiki wanaambiwa bado kile. Then hupewa kakenda ya kulipwa, hapo sasa shughuli inaanza tena.

Kama mtumishi hana mradi wowote wallah anaweza kufa kwa njaa au pressure pindi atakapostaafu maana kipindi cha kusubiria mafao hakitabiriki.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,244
2,000
Hawa watu huwezi kukuta mwanasiasa anawatetea kwa dhati.

Wanasiasa wameshambulia mifuko ya hifadhi kama nyuki.

1- Mbowe amewahi kukopa huko Milioni 600 sidhani kama amewahi kurejesha.

2- Zitto amepiga sana NSSF enzi za Ramadhani dau.

3- Wanasiasa wa CCM sisemi maana wao ni sugu tena with full impunity.

4- Serikali ndio kabisa inaichukulia hiyo mifuko kama hazina yake ndogo.

So sad.
 

Spicegold

Member
Mar 5, 2021
15
45
Asalaam Aleykum

Hili tatizo limekuwa endelevu na Ni kwasababu Policy Makers hasa Wabunge wao hawazungushwi,wala hawapewi "Empty Promises"

Inaingiaje akilini mtu unakamilisha viambatanishi vyoote then unapewa tarehe ya kurudi,halafu unaambiwa kimepanda kimeshuka.
PSSF ni virus inayoua wastaafu.

Sijajua kuhusu NSSF Kuna mbunge aliongea vizuri Sana Kama mtu ana clip anaweza kuiweka ,tuende tufike mahali kipimo Cha Rais kuwa madarakani Ni jinsi atavyoshuhulikia Mafao ya Wastaafu bila kuwachosha hivihivi asipitishwe
 

IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,195
2,000
Kuna waliomaliza mikataba yao pesa zao wanapewa asilimia 33 tuu nyingine mpaka baada ya miezi 18
Hivi sheria ya fao la kujitoa imeshapita au bado?
Imepita, maana haijafutwa. Mwendazake aliipiga stop tuu kwamba isianze kutumika kipindi kile, ilitakiwa aelekeze ifutwe au ifanyiwe changes.
 

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
624
1,000
By the time mtu unagonga miaka 50, ni vyema kuanza kujiandaa na kustaafu kwa kuhakikisha angalau una nyumba yako (usiniambie kujenga haiwezekani hasa kwa familia ambayo baba na mama wote wanapata mishahara).

Angalau una ka gari kagumu na fuel efficient kama Vitz au IST, una ka akiba benki angalau milioni kumi na pia uwe unamiliki miradi midogo midogo hasa ya kilimo na ufugaji.

Tofauti na hapo ni stress tupu baada ya kustaafu!
 

Chris wood

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
898
1,000
Ndugu yangu kamaliza chuo 2014 mpaka sasa hivi navyicoment yuko ndani kajifungia amelala full depression, no job

Kibaya zaidi hana hata mchumba

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Daa ndio nilikuwa naanza fm5 mpaka na mimi nimemaliza degree halafu nimeunga nae kwenye foleni.

Ila sijawahi experience maisha mabovu ya stress kama kukosa ajira, majobless tunakazi.

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,066
2,000
Ndugu yangu kamaliza chuo 2014 mpaka sasa hivi navyicoment yuko ndani kajifungia amelala full depression, no job

Kibaya zaidi hana hata mchumba

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Wity mie ntakubali mnipopoe tu, mshauri atoke hapo alipo mpe fare aende mkoa! Jamani kuna siri kubwa sana ya kutoka mahali ulipo ukaenda mbali kbs. Shida ya wanadaresalama wameuzoea mji wanaona wakitoka hapo hakuna kwingne kwa kwenda!

Mie ni muumini sana wa kutoka kwenye comfort zone!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom