Ukiondoa tabia ya kuwarubuni wabunge wa CHADEMA wahamie CCM, Dkt. Bashiru ni kiongozi makini na mjamaa

Wapiga vigelegele bado wapo? Ina maana mpaka sasa hawajaona mapungufu makubwa ya kiuongozi aliyoyafanya mwendazake? Mwenda zake badala ya kuliunganisha Taifa yeye alikuwa ameligawa kwenye vipande vidogovidogo mithili ya chupa iloanguka toka juu ya ghorofa mpaka chini kwenye jiwe gumu matokeo yake baadhi ya hivo vipande vimejificha ambapo ni hatari kwa afya ya Taifa hapo baadae
 
Kiukweli chini ya uongozi wa katibu mkuu Dkt. Bashiru, CCM imepata mafanikio makubwa sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Sasa mali za chama zinajulikana bayana na miradi yote ya CCM inajulikana tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa watangulizi wake kuanzia Dkt. Gama hadi kanali Kinana.

Tatizo moja la uongozi wa Bashiru ni ule utaratibu wa kuwarubuni wapinzani na kuja kuwapa vyeo serikalini wakati UVCCM kuna hazina ya kutosha ya wasomi.

Itoshe tu kusema Dr Bashiru bado anafaa kuongoza CCM labda kama vyombo vimemmulika pahala.

Kazi Iendelee!
Mkuu you are beating a dead horse!
 
Kati ya watu waliopata hasara kuhama CHADEMA ni Dr. Mashinji. Mpaka sasa hajalambishwa cheo chochote tangu atie nia.
 
Tz tumepoteza dira, hatuendi tulikotamani na tunaongozwa na wasioona faida ktk kujitegemea kwetu kama nchi huru. Wanadhani kuwategemea weupe na kuwatetemekea ndo kutatupa maendeleo na kujitegemea.

Mwl. Nyerere aliandika ktk development&freedom akimaanisha hivi vitu haviachani. Hauwezi ukajiita umeendelea na wakati huna Uhuru wa ndani ya nchi yenu.

Leo wenye mawazo ya kujitegemea wanauwawa na imekuja siasa kali ya kuwaondoa ili kutawaliwa kurudi mezani. Wanawaaminisha eti wanaweza kuwasaidia kuendelea na kusahau kuwa Uhuru kamwe hawatakaa wawape

Kwa sasa ni rahisi mgonjwa wa ukimwi akaishi +50 na akafikisha 100 kuliko kiongozi anayesimamia nchi yake na kujitegemea kuishi japo kwa miaka 10.

Nilishawahi kusema mtu kama Nyerere, JPM, na hata hawa akina Bashiru dunia ya leo si sehemu salama kwao kuishi. Ni sawa ilivyo bahari huwa si sehemu ya kukaa uchafu na badala yake itautema tu. Sasa hawa wema pia dunia si sehemu salama kwao, naturally itakutema tu. Dunia ni sehemu ya maovu na waovu kustawi, ni mahala ambako mabaya yana nguvu sana na kulindwa na ndo maana wezi wa kuku wanaozea jera na wauza sembe wanatamba mitaani. Uharamia ni mkubwa na ukijifanya kuuzuia utaishia kupotea kwa corona ya kisasa.

Machoni hatupendi ubaya na maovu japo rohoni tunahusudu ktk maovu na waovu, wenye wema kwao mbinguni na duniani ni kwetu sie wazee wa mishemishe
eeeehh

hapo kwa Bashiru na jiwe ni mtazamo wako Ila kumuweka hapo Nyerere ni kukosa adabu na heshima

Nyerere alikuwa kiongozi aliyependa haki na amani si vema kumfananisha...na hao.

Asante
 
bashiru ni mwanasiasa mpuuzi sana. namshangaa mama kampa hata huo ubunge.a alitakiwa arudishwe chuoni akasome.
 
Kiukweli chini ya uongozi wa katibu mkuu Dkt. Bashiru, CCM imepata mafanikio makubwa sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Sasa mali za chama zinajulikana bayana na miradi yote ya CCM inajulikana tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa watangulizi wake kuanzia Dkt. Gama hadi kanali Kinana.

Tatizo moja la uongozi wa Bashiru ni ule utaratibu wa kuwarubuni wapinzani na kuja kuwapa vyeo serikalini wakati UVCCM kuna hazina ya kutosha ya wasomi.

Itoshe tu kusema Dr Bashiru bado anafaa kuongoza CCM labda kama vyombo vimemmulika pahala.

Kazi Iendelee!
Huyo Mrundi Bashiru ndiye alikuwa anaandaliwa na Mwendazake kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2025. Yaani kweli hicho kiazi ndiyo cha kuwa Rais wa Tanzania? Alipoona yeye amepata kuwa Rais kwa sababu ya misuguanao ya JK na Lowassa mwaka 2015, akaona ngoja atuletee Mrundi mwingine.

Ila Mungu anajuwa kuchukua hatua. Kwanza kapeleka Jehanam roho ya Mwendazake, huyu naye Bashiru anasubiria ripoti yake ya uchotaji fedha za BOT akiwa mbunge wa viti maalum
 
Nafurahi kuona vibarua wote mmelipwa posho ya March hakuna deni tena, ngoja mzigo ukate na uchelewe kulipwa tena posho ya April hatutaacha kuona rangi yako.
Hahahaaaa...... Kesho CCM inazaliwa upya wabunge 20 wa Chadema kuhudhuria mkutano mkuu!
 
Kiukweli chini ya uongozi wa katibu mkuu Dkt. Bashiru, CCM imepata mafanikio makubwa sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Sasa mali za chama zinajulikana bayana na miradi yote ya CCM inajulikana tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa watangulizi wake kuanzia Dkt. Gama hadi kanali Kinana.

Tatizo moja la uongozi wa Bashiru ni ule utaratibu wa kuwarubuni wapinzani na kuja kuwapa vyeo serikalini wakati UVCCM kuna hazina ya kutosha ya wasomi.

Itoshe tu kusema Dr Bashiru bado anafaa kuongoza CCM labda kama vyombo vimemmulika pahala.

Kazi Iendelee!
Hakua anawarubuni alikua anawanunua kwa pesa kama kawaida ya fisiem
 
Kiukweli chini ya uongozi wa katibu mkuu Dkt. Bashiru, CCM imepata mafanikio makubwa sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Sasa mali za chama zinajulikana bayana na miradi yote ya CCM inajulikana tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa watangulizi wake kuanzia Dkt. Gama hadi kanali Kinana.

Tatizo moja la uongozi wa Bashiru ni ule utaratibu wa kuwarubuni wapinzani na kuja kuwapa vyeo serikalini wakati UVCCM kuna hazina ya kutosha ya wasomi.

Itoshe tu kusema Dr Bashiru bado anafaa kuongoza CCM labda kama vyombo vimemmulika pahala.

Kazi Iendelee!
Asante kumpigia kampeni za uteuzi kurudishwa chamani ukatibu mkuu sawa nitafikiria
 
Hafai hasa kwa nafasi ya KM sababu he is too robot, hajui chama na hajui kinafanyaje kazi from the grassroot, Yeye na mwendazake wamepitisha vijipolicy vya ajabu vimepelekea maumivu na ufukara hata kwa watumishi wa chama, Mfano ni makusanyo kuhamia acc moja ya makao makuu. Huyo polepole ndio hamna kitu anajisifia viongozi wa wilaya na mikoa kuwa na toyota hardtop hajui hata mafuta wanapata vipi, bure kabisa waondolewe wote wapewe wana CCM chama chao.
 
Back
Top Bottom