Ukiondoa redio na televisheni, watu wengi wanaamini zaidi taarifa za kusikia kwa mtu kuliko zinazoandikwa mitandaoni..

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Sio maneno yangu, ni utafiti..

Kama utakavyosoma kwenye jedwali hapo chini, imebainika kuwa wabongo wengi kwanza kabisa wanaamini sana wanachokisikia kwenye redio.. Kisha wanaamini wanachokiona kwenye TV.

Huko mikutanoni wanaamini kiasi maana washatiwa ndimu sana, kwenye magazeti pia imani imepungua sio kama zamani..

Kimbembe hapa kwenye mitandao... Wanachagua sana nani wa kuamini.. Mfano JamiiForums inaaminika sana.. Mtu anaweza kusoma kitu lakini ili apate uhakika lazima aone kama JF kimeripotiwa au la.. Huo ni mfano!

Kinachochekesha.. Walio wengi wanaamini zaidi wanachoambiwa kuliko wanachokisoma mtandaoni...

Unasemaje?

9.JPG
 
Mmh.. Kwahiyo huo utafiti unataka kusema humu mitandaoni tunalishana matango pori ama? Daadeki!

Hata hivyo imani itazidi kukua kwa sababu mitandaoni ndipo chimbuko la taarifa nyeti zote kwa sasa.. Tatizo mitandaoni bado kuna fujo sana, vumbi likitulia pataaminika.

Kuhusu Redio hapo ni kweli tupu. Hasa vijijini. Yaani huko redioni ukanjanja unadhibitiwa sana na TCRA wakikunasa unafanya mzaha wanarara na wewe mbere!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom