Ukiondoa ndoa na misiba: Makanisa na misikiti hayana Faida kwa Waumini

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Kuna watu huwa nawaambia, Ikitokea taasisi iliyoserious kabisa kuhudumia mambo hayo mawili ya ndoa na misiba hata kwa malipo kidogo ya mwaka kama bima.

Ni watu wachache sana wataendelea kusali haya makanisa yaliyogeuka maduka siku hizi.

Makanisa mengi yamekuwa na viongozi wasiyo waadilifu.

Viongozi wa dini wamegeuza milango ya makanisa kama Duka lao la biashara.

Ni jambo la kawaida sana siku hizi kumkuta padre au mchungaji anaendesha gari ya bei mbaya.

Hapo ndipo ujiulize pesa wanapata wapi kama siyo sadaka, na upigaji wa mali za kanisa ni nini?

Sasa hivi mbinu kubwa wanayoitumia kuiba pesa ni kupitia miradi ya ujenzi na viwanja wanavidalalia.

Ni aibu sana kwakweli!

Kwahiyo ikitokea taasisi ikajipambanua kuja na sera mbadala kutoa huduma za ndoa na misiba hakuna atakayesali makanisa haya.
 
Kuna ibada kuu tatu duniani kwa binadamu

Kuzaliwa
Kuoa/kuolewa
Kifo

Hizi ni muhimu umwone kiongozi wako wa dini
 
Kuna ibada kuu tatu duniani kwa binadamu

Kuzaliwa
Kuoa/kuolewa
Kifo

Hizi ni muhimu umwone kiongozi wako wa dini

Kabla dini zetu hizi hazijakuja huku Africa, walifanyaje wazee wetu?

Tatizo ukiyafanya hayo mambo kiasili yetu utaonekana mshamba na mshirikina.
 
Dawa ni kuachana na hizi dini mi nimesha sign out mambo ya makanisa kwa sababu neno MICHANGO NA TOA yanatamkwa mara nyingi kuliko neno YESU KRISTO AMA MUNGU.
 
Dawa ni kuachana na hizi dini mi nimesha sign out mambo ya makanisa kwa sababu neno MICHANGO NA TOA yanatamkwa mara nyingi kuliko neno YESU KRISTO AMA MUNGU.
halafu wakizipata wanakusimangia nazo
 
Dawa ni kuachana na hizi dini mi nimesha sign out mambo ya makanisa kwa sababu neno MICHANGO NA TOA yanatamkwa mara nyingi kuliko neno YESU KRISTO AMA MUNGU.

Mahubiri mengi inazungumzwa zaka na sadaka tena wanatia na vitisho ili uogope mimi kwangu hilo halipo
 
Mambo mengine yanachekesha kama sio kuhuzunisha,utawezaje kusemea jambo kubwa namna hii kijumlajumla,umefanya utafiti ?au umefanya rejea wapi?.wangapi wanaomba wawe na maisha mema,wangapi wanaomba waepushwe na shida walizo Nazi,wangapi wanawaombea watu wengine wenye shida?makanisa na misikiti yanafanya mambo makubwa kuliko ndoa&mauti,wewe unaona watu Walpole,wanyenyekevu hujui ni Nazi za watumishi.ndoa zinafungwahata kimila na kiserikali na ni nyingi xa kutosha
 
Wanasaikolojia wapo! Kuhusu Aman na upole ni kwasababu ya jeshi la polisi na serikali usijidanganye unaletwa na makanisa haya yanayotupigia miziki usiku kucha
 
>>>Hujaongelea kuhusu Shule zao ..awali..msingii..sekondari...chuoooo....

>>> Huduma za afyaaa....zahanati...kituo cha afyaa...hospitali...hospitali maalumu...

>>>vituo vya ushauri/malezi maalumuuuu...

Je hivyo navyo TUACHANE NAVYOOOOOOOOOOOOOOO....ukipenda boga penda na mti/ua lakeee....
 
Picha hiyo inajieleza vizuri
IMG-20191109-WA0000.jpeg
 
Back
Top Bottom