Ukiondoa matukio ya Michezo, 90% ya matukio mengine mubashara (live) duniani huwa siyo halisi na bayana (off live record )

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Kama neno lilivyo (Mubashara/Tv Live coverage)!

Likiwa na maana ya kuona matukio kwa wakati kupitia luninga au Simu janja pasipo kuwepo eneo la tukio!

Pamoja na nia njema za wavumbuzi Wa teknolojia hii kulenga kuonesha kila kitu kinachotendeka eneo la tukio kama ambavyo kingeonekana endapo mtazamaji angeamua kuhudhuria eneo hilo!

Ukiondoa kabumbu na michezo; Utekelezaji wa "live coverage" umeonyesha kupigwa vita sana hususani nchi zinazoendelea, kiasi kwamba wanahabari huogopa kuchukua matukio yanayoaibisha!

Mfano!
Nchini MAREKANI; Rais Trump alipokuwa akitoa utetezi wake mbele ya viongozi Wa bunge la seneti, tuliona live ambavyo hakumsalimia (shake hands) spika, pia tuliona spika alivyoichanachana ile hotuba ya Trump na kuitupa kwenye dustbin!

Hii inamaana gani?
(Waliokuwapo waliona na tuliokuwa live tuliona, hiyo ndiyo maana ya MUBASHARA! (Yaani asiyekuwepo anashuhudia)

Sasa Tuangalie nchi zinazoendelea zinafanya nini kwenye matukio mubashara!
  • Mrusha matangazo anatakiwa afiche madhaifu yoyote yanayoonekana pale!
  • Na ikitokea Tukio dhaifu limeoneshwa basi huwa lipo ndani ya mpango kazi tangu mapema (planned event)
  • Serikali huwa ipo tayali kuficha udhaifu huo Kwa gharama yoyote, badala ya kutumia gharama hizo kutatua changamoto iliyooneshwa!
Mfano; Serikali inaweza gharamia kuendesha kesi Kwa million 200 kumshitaki Mwandishi wa habari au mtu aliyereport habari dhaifu inayohitaji kutatuliwa kwa million 50 tu!

Hivyo matukio mengi ya mubashara huwa yanaficha na kuchujwa taarifa ukiondoa michezo!

Ninaposema Michezo inajitahidi kufanya "live coverage" ninamaanisha hata kama kuna makosa, sote tunayashuhudia Kwa pamoja!

Mfano! Timu yetu ya Yanga ilipo fungwa goli na refa akaamua ipigwe kona! Sote tuliona "LIVE"

Hakika nchi zinazoendelea upande Wa taarifa mubashara bado tuna wingu zito sana la kitumwa! Hatujui kutofautisha maana ya live na recorded!

Kazi ya kuchuja au kukwepesha habari mubashara ni matumizi mabaya ya AKILI.
 
'* Na ikitokea Tukio dhaifu limeoneshwa basi huwa lipo ndani ya mpango kazi tangu mapema (planned event)'

Kwa hio CNN hua wanapanga na Trump kumuonyesha Live Upumbavu anaoufanya sio?

Hii habari yako nayo ni FAKE NEWS.
 
Huku kwetu watu wa camera wanaambiwa kabisa ikitokea jambo la kufedhehesha asirekodi kabisa au ahamishe camera.ikitokea vinginevyo wanahariri kabla ya kurusha..
 
Toa mfano wa tukio la kuaibisha unalohisi liliwahi kutokea kwa nchi yoyote inayoendelea na likafanyiwa editing ili kuficha ile aibu.
 
'* Na ikitokea Tukio dhaifu limeoneshwa basi huwa lipo ndani ya mpango kazi tangu mapema (planned event)'

Kwa hio CNN hua wanapanga na Trump kumuonyesha Live Upumbavu anaoufanya sio?

Hii habari yako nayo ni FAKE NEWS.
Unajua kusoma lakini au unajitoa ufahamu! Hicho kipengele ulichokinukuu kilikuwa kwenye para ya nchi zinazoendelea! Sasa huyo Trump ni rais Wa nchi inayoendelea?
 
Huku kwetu watu wa camera wanaambiwa kabisa ikitokea jambo la kufedhehesha asirekodi kabisa au ahamishe camera.ikitokea vinginevyo wanahariri kabla ya kurusha..
Ikiwezekana hata wanaweza kuikana habari nzima kuwa ilikuwa igizo
 
Hawa ndio waliokula kalimati na mchuzi wa ndimu wakamix na togwa pembeni senene akakandamizia na mayai akala na miwa akapiga na kachumbari akadokeza na supu ya popo akapata na mchemsho wa sungwi akasukumiza na mbatata akala na mihogo akamalizia na komamanga!

Vumilieni vinyampo vyake msimseme Sana.
 
Rais Mwinyi alivyopigwa makofi pale msikitini lile tukio lili-rushwa Live na kwny taarifa ya habari ITV kiroho safi.

Kwa hio hii nayo ilikua imepangwa sio?
Hivi unaelewa matukio ya kimkakati yalivyo!? Kipindi kile upepo ulikuwa unaelekea wapi?
 
TBC yeyote anayehojiwa anasifu juhudi za serikali,hata wale wanaohojiwa mtaani au matukio ya taarifa ya habari.

Kuna vipindi kama machinga smart (wafanyabiashara wadogo),yupo na meza ya machungwa na katon moja ya maji na soda unakuta anasifu tu.

Bomba la maji limekatika miezi 5 imeunganishwa wakianza kuhojiwa wanaanza kusifia.Sijui watu kama hao wanatokeaga wapi mtaani hakuna hata wa kusema changamoto inayowakumba hata siku moja

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Nahitaji ufafanuzi wa namna serikali inavyoweza tumia milioni mia mbili kumshitaki mwandishi wa habari.
 
Nahitaji ufafanuzi wa namna serikali inavyoweza tumia milioni mia mbili kumshitaki mwandishi wa habari.
Inaweza kumsafilisha mtuhumiwa kutoka mkoa Wa magharibi kwenda mashariki kusomewa mashitaka Kwa ndege au msafara Wa magari matatu, kumbuka watu wote hao wanalipwa posho na mishahara, wakimsomea kesi, mawakili Wa serikali na majaji n.k watalipwa Kwa ajili ya kesi, wakimuweka lumande miezi 6 kwenda na kurudi mahabusu, kula, ulinzi n.k vyote ni Pesa, upelelezi na kukusanya ushahidi na safari posho na matakataka kibao ya kesi yote ni Pesa, kuaanda mashahidi zote ni Pesa,...mambo ni mengi sana hadi kesi kuisha DPP anakuwa hana nia ya kumshitaki mtuhumiwa Pesa inayokuwa imetumika inatiosha kujenga zahanati
 
Mambo mengi uliyoyaandika hapo hayana uhalisia, ni porojo tu.

Yaani hapo nilipo bold, umeandika uongo mkuu. Hakuna kitu kama hicho. Hujui namna kesi zinavyoendeshwa, unapotosha watu hapa.
 
Mambo mengi uliyoyaandika hapo hayana uhalisia, ni porojo tu.

Yaani hapo nilipo bold, umeandika uongo mkuu. Hakuna kitu kama hicho. Hujui namna kesi zinavyoendeshwa, unapotosha watu hapa.
Hujui kitu wewe!
 
Back
Top Bottom