Ukiona wazazi au ndugu zako hawakusapoti au kukutia moyo katika harakati zako za kutafuta maisha, anza kujitakari

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Japo sio wote lakini ukiona wazazi wako au ndugu zako hawakusapoti au kukupa moyo katika harakati za kutafuta maisha anza kujitafakari mapema.

Ukiona unamwelezea mzazi wako mipango yako ya badae ya kimaendeleo kama vile kujitegemea kuoa, kufungua biashara, kutafuta maisha alau wao hawakusapoti wala kukutia moyo, anza kujitafakari.

Tena kuna wengine ukitaka kuchukua maamuzi magumu ya kufanya jambo la kimaendeleo wao wanakwambia utulie huku hawana msaada wowote na wewe ikishafikia hatua hiii anza safari ya kujitafakari.
 
Pole sana kwa yanayokukuta

We may encounter many defeat but we must not defeated

Be yourself, everyone else is already taken

Kua muamuzi wa maisha yako kwani wewe ndiye mmiliki wa maisha yako, ulikuja Duniani peke yako na utaondoka peke yako, love the life u live, live the life u love.
 
Wajibu mkubwa wa mzazi pia ni kuanza kumuandaa mwanae ili aje awe flani, na mtoto anapo andaliwa na mzazi ni rahisi sana kumshirikisha mzazi katika kila mipango na hitaji lake wakati anapo kua.

Ukiona mzazi hamsapoti mtoto wake, basi ujue kuna tatizo kati yao lililo tokea hapo kabla ambapo yawezekana kijana hakua mtii/msikivu kwa mzazi wake ama mzazi hakuwajibika vyema kwa mtoto wake.
 
Duniani ulikuja peke yako,na utaondoka peke yako,hutaondoka na mama, baba, dada, au kaka

Furaha yako, ni wewe tu, usitegemee sana msaada wa hali na mali kutoka kwa familia yako, zipo familia ambazo huwa na mikakati ya kusaidia vijana wao wasimame vzr,kiuchumi,wenzetu wa Ki Asia hii wanafanya sana, nimeiona pia kwa Wachaga,na baadhi ya familia za nyanda za juu kusini,Mbeya,songwe.

Usipokuwa makini,familia yako,kwa maana ya wazazi,kaka,dada,wajomba,wanaweza kuwa chanzo Cha wewe kutokupiga hatua,
Watoto lazima uwape pa kuanzia,Kama leo hii,karne 21,#ajira ni ngumu,fikiria watoto wanaozsliwa leo,maisha yao yatakuwaje miaka 20 ijayo,lazima kuwaandalia pa kuanzia,biashara,nyumba,ardhi,mtaji.
 
Ukiona hizo dalili anza kujiengua ndani ya familia ufanye maisha yako kimya kimya hii dunia ina Siri kubwa sana.

Inawezekana wazazi wako wamekugeuza wewe Msukule hivyo unavyoonekana mjinga mjinga hauwezi kitu ktk maisha na ndio wao wanazidi kupata mpunga.
 
Japo sio wote lakini ukiona wazazi wako au ndugu zako hawakusapoti au kukupa moyo katika harakati za kutafuta maisha anza kujitafakari mapema.

Ukiona unamwelezea mzazi wako mipango yako ya badae ya kimaendeleo kama vile kujitegemea kuoa, kufungua biashara, kutafuta maisha alau wao hawakusapoti wala kukutia moyo, anza kujitafakari.

Tena kuna wengine ukitaka kuchukua maamuzi magumu ya kufanya jambo la kimaendeleo wao wanakwambia utulie huku hawana msaada wowote na wewe ikishafikia hatua hiii anza safari ya kujitafakari.
Hata ikitokea Wazazi, Ndugu na Marafiki baadhi Wakakuchukia au Kukutenga bado Muumba Baba Mwenyezi Mungu hatokutupa na atakuokoa tu.
 
Huwa naona hakuna stress mbaya kama kusubiria watu wakushike mkono au wakuelewe kwa unachokifanya.

Binafsi Kama sijamkosea mtu kiasi cha kutengwa na familia, bhasi ni Kheri niishi stress za kutokuwa na kitu, at least huwa zinaisha ila stress za hivyo huwa ni kama gereza, ukiingia hutoki na hata ukipata mafanikio na usipate wa kukupigia makofi bado hutoridhika.
 
I feel your pain my son , nilishawahi kusajiri biashara ,nikaset na kaofisi kabisa nikaenda home na kikampani profile changu na registration documents kumuonyesha mshua kwamba hajalea ndezi katikati ya maongezi akaniambia nimtumie cv yangu kwa email ana rafiki ni member ya bodi ya wakurugenzi wa shirika flani la vindege vidogodogo kama vibajaji vya angani apo ndio ule usemi wa "once a pimbi always a pimbi" kwamba hata upige yope hautaacha kuonekana pimbi issue ni kufanya majambo yako mwenyewe don't live to impress your folks utakufa na depression
 
Back
Top Bottom