Ukiona watu wazima na akili zao wanafanya hivi kwa mwizi ujue kuna tatizo kubwa-Edson wa JF

hii picha inatia kinyaa na leo sijui wanajihisije hao jamaa kwa kile walichofanya jana
 
kwa staili hii, nchi imerudisha ubepari. acha watwana watumikie mabwana zao. Ukisoma picha kuna habari nyingi za kuandika. 1. Maslai yao yaliwekwa rehani. 2. Uozo uliopo ni wa wengi. 3. Kuna siri nzito ingefichuka. 4. Anawasaidia sana maswala ya kifedha. Nisaidieni nyingine.

....anawachukulia wake zao. Jamani mi hata sielewi hawa kama kweli wana akili timamu jamani. Kwenye live reception kuna mama mmoja mweupe mnene alionekana mwenye furaha sana. Sijui ndiye alikuwa PS wake? Alikuwa na furaha 'as if' ile ilikuwa ni harusi ya binti yake wa kumzaa!
 
mi ciku iz hata vidole vya kutaip comments vimekufa ganzi...!

nikae tu kimya....better this way!

mna heri mlioko ulaya,asia na america!hakika mna heri ninyi....na nisingewashauri hata kufikiri kuyafanya maisha yenu tanzania!please

Maneno mazito haya TEAMO! duuh, kweli mkuu mfumo unakukera, pole sana kaka....taratibu tutafika.
 
kuna tatizo kubwa kweli ndugu yangu...hayana akili bali ni matope...tena ndo yale yale unayakuta uwanja wa fisi jioni yanakunywa matap tap...huku nchi giza tupu...ukienda kuomba kulipa ankala yanaendelea kudai rushwa ...."pum...fu"
 
Hivi kati ya hawa watu wazima (?) hakuna hata moja humu ndani JF atueleze japo kidogo ni kitu gani hasa kiliwatuma hadi mkaamua kulisukuma hilo gari la mwizi mkubwa ? Nina hakika hapo wizarani mnapitiapitia humu ndani, hebu pateni ujasiri wa ama kutetea kitendo chenu hicho au kuwaomba radhi Watanzania waliochukizwa na usaliti wenu huo. Mnajisikiaje hivi sasa baada ya baba huyo (!) kupelekwa likizo kwa mara nyingine na kama mtakuwa mmevunjika moyo poleni kwa hatua iliyochukuliwa na bunge.
 
Wadanganyika ndivyo tulivyo tunanung'unika tu,mm naamini walio wengi pale walisukuma gari pasipo kujijua na kila mtu aliogopa asionekane hayupo pmj na jairo so kila mtu alikimbiza bawa lake hii ni hadithi ya kunguru muoga,ila ni fedhea,aibu kwa wasomi na wafanyakazi wa idara hiyo,ngoja tuone manake sinema bado inaendelea
 
Kila kitu huku ni ushabiki tu, sasa hawa wote wanaweza wakakamilishiwa mahitaji yao na huyu jamaa, ninachoshukuru baada ya siku chache waliaibika vibaya mno, acheni ushabiki wa vitu ambavyo hata mungu havimrudishii sifa na utukufu bali ni ubatili mtupu
 
Tuwaombee maana hizo sio nafsi zao. Nahisi ni mapepo kwa sababu ktk hali ya kawaida 2 hakuna mtz wa sasa hivi anayeweza kufanya hayo waliofanya hawa. AIBUUUUUUUUUUUU
 
WEZI UTAWAJUA KWA MASABURI YAO!!!!!!
MWIZI HUMTETEA MWIZI MWENZIE HASA AKIJUA AMESEVU
ONA MASABURI HAYO, WATU WAZIMA OVYOOO GEUKENI TUONE SURA ZENU!!!
<!-- google_ad_section_end -->
 
Back
Top Bottom