Ukiona watu wanapenda pesa kuliko utaifa, ujue taifa linaangamia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiona watu wanapenda pesa kuliko utaifa, ujue taifa linaangamia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shayu, Nov 2, 2011.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Ukiona watu wanapenda pesa kuliko utaifa ujue taifa ndio lina angamia! Moyo wa utaifa umotoweka, hii changamoto kwa kiongozi yeyote makini na mzalendo, umoja wetu ndio nguvu yetu, tulitumikie taifa letu kwa nguvu moja.

  Ufisadi hutugawa, lakini haki hutuleta pamoja, tunahitaji kiongozi atakayetuunganisha na kutumikia taifa letu, ili tujitegemee na tutengeneze mamlaka mpya duniani.

  Ubinafsi Mwisho wake tutapigana wenyewe kwa wenyewe, nchi yetu imekuwa na magenge ambayo yanasuguana sio kwa maslahi ya taifa hili, bali ubinafsi, wameligawa taifa hili kwa uroho, lakini Sisi tunahitaji kujenga taifa imara kwa vizazi vyetu, tunahitaji kujitegemea na kujenga uchumi wetu wenyewe ili watu wetu wawe wenye kuheshimika. Ni Aibu kwa viongozi wetu kusaka uongozi hadi kwa waganga wa kienyeji mtu kama huyu hafai kuongoza wananchi ni mbinafsi na mroho anataka uongozi kwa faida zake binafsi na anasa, Kiongozi wa kweli ni yule anaye organize watu kutumikia taifa lao wenyewe, sio yule anayetumia nafasi hiyo kujinufaisha na kuisha maisha ya anasa wakati watu wake wakiteseka.
  Tumekuwa taifa lisilokuwa na mwelekeo, wananchi hawajui wanapoelekea ni nini mission ya taifa, tumekuwa watu wa binafsi na wenye choyo. Ubinafsi huondoa mantiki ya watu kuishi katika taifa, kama taifa ni lazima tujue nini kimetuunganisha na wapi tunataka kuelekea, Kujumuika kwetu kwa pamoja ni ili tuwe na maisha mazuri kuliko haya tuliyo nayo, ili tuishi kwa amani, undugu na upendo, ili kulinda taifa letu dhidi ya maadui wa kigeni. Haki za kila mmoja wetu ni muhimu ili kujenga taifa lenye umoja. Tuna taifa ambalo watu wake hawajui wajibu wao kwa nchi yao wenyewe , hii ni hali ya hatari sana. Ni lazima tujenge taifa amabalo vijana watajua wajibu wao kwa taifa, hili ni jambo muhimu sana. Taifa huvunjika na kusambaratika kabisa, msifikiri kwamba mtaishi milelele katika nchi hii kama hatukujenga misingi ya umoja na mshikamano wetu. Ni lazima tufikirie upya juu ya ujenzi wa taifa letu na mustakabali wetu kama taifa.
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa aina hiyo ya Taifa watu wake uamini kuwa kila kitu kinawezekana kwa njia ya Pesa.Na kuwa hata Mapenzi nguvu yake kubwa ni Pesa.Na ndio maana mabinti wengi wa sasa kwenye miji yetu mikuu wamekuwa ni watumwa wa vibabu vyenye fedha kwa kuwa hawna jinsi wanataka kukaa kwenye nyumba kubwa na kuendesha magari ya gharama kubwa.

  Kila kitu kimekuwa pesa mpaka heshima ya familia imekuwa mwenye fedha ndio anasikilizwa na familia hata kama ni ya wizi.
   
 3. Poriposha

  Poriposha JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Shayu.... una mawazo pevu kiasi ila tatizo Now LIFE LIMEKUWA TIGHT MNO ndio maana inakuwa hivyo
   
 4. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Huo ndio mwanzo wa ufisadi.
   
Loading...