Ukiona wapinzani wapo kimya tambua chama tawala kinafanya vyema

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Upinzani katika mfumo wa vyama vingi ni kioo kwa chama kinachotawala. Maana wapinzani huwa wanakosoa pale mtawala anapokosea.

Tangu mama aanze vyema kwa kuupiga mwingi mpaka wapinzani wakaanza kumsifia kwa kila namna anavyoendesha nchi ni dalili tosha kuwa chama tawala kinafanya vyema.

Kero kama ya tozo ya miamala kutatuliwa kwa muda mfupi ni dalili njema pia, japokuwa ilitakiwa ifutwe kabisa. Najua huko mbele itafutwa hasa baada ya zahanati, shule na vituo vya afya kukamilika.

Kama chama tawala cha Ccm hakifanyi vizuri, tunavyowajua wapinzani hasa Act wazalendo, Cdm na Cuf wangelianza kuleta maneno.

Kwq mwendo huu wa wa serikali ya mama Samia kuchapa kazi huku ikitatua kero za wananchi ni vyema wapinzani wakapongeza japo kiduchu.
 
Yani nyie mnajali wapinzani tu basi.
Natamani mama amtembelee yule kansela wa ujerumani bi Anjela, achukue desa lake alifanyie kazi. Anjela kaiongoza nchi yenye changamoto nyingi kwa ustadi sana.
 
Vyema kwa kubambikia, kuonea na kunyanyasa wapinzani tena kwa msaada wa wale wanaolipwa kwa kodi za wananchi. Acha utani, waambie ukweli kwa ustawi wa taifa letu na sii uangalie ustawi wa tumbo lako pekee.
 
Back
Top Bottom