Ukiona vijana wanaandamana kwenda kwa Rais kudai kuangalia TV ni mzigo kwa Taifa

kanone

JF-Expert Member
Oct 10, 2013
6,188
1,576
Nimesikitishwa na KUONA habari kwenye magazeti inayosema vijana wa chadema kuandamana kwenda kumuona rais magufuli wakidai haki ya kuangalia tv asubuhi ,kwa maana ya bunge,
Ni aibu kwa kizazi hili kinachojiita vichana wa kimapinduzi,

Naamini rais atasikitika na kuudhunika pamoja na mipango YAKE AMBAYO ili ifanikiwe mtaji wake mkubwa ni vijana lkn ndo wanaomba kuangalia TV asubuhi
Ni aibu,
 
Waalimu Wako Ni majipu
Watu wanaandamana kudai haki ya kupata habari bila kuingiliwa na kupangiwa na serikali
Wanajaribu kuzuia precedent mbaya na ya hovyo kabisa ya kupangiwa nini na wakati gani wa kuangalia
 
Nimesikitishwa na KUONA habari kwenye magazeti inayosema vijana wa chadema kuandamana kwenda kumuona rais magufuli wakidai haki ya kuangalia tv asubuhi ,kwa maana ya bunge,
Ni aibu kwa kizazi hili kinachojiita vichana wa kimapinduzi,

Naamini rais atasikitika na kuudhunika pamoja na mipango YAKE AMBAYO ili ifanikiwe mtaji wake mkubwa ni vijana lkn ndo wanaomba kuangalia TV asubuhi
Ni aibu,

Inabidi turudi kule kwenye mila ambapo kijana kabla ya kuoa au kuolewa wazee walikuwa wanatuma asubuhi watu kutizama kama huyo kijana au msichana asubuhi hiyo kaamuka yuko shambani au yuko nyumbani.Wakikuta mida ya asubuhi yuko nyumbani wakati kijiji kizima kiko shambani wanajua huyo msichana au mvulana hastahili kuolewa wala kuoa sababu ni mvivu atakuja ua watoto kwa njaa na familia itakufa kwa njaa.

Nawapoongeza baadhi ya wachaga Mtu akitaka kuoa vile wanavyohoji una hela,una nyumba,una gari una kazi yakueleweka wewe?

Hao watakaothubutu kuandamana video zote ziwachukue vizuri tena mno mtu kama una binti yako au kijana asije oa au kuolewa na hao waandamanao kwa upuuzi kama huo na mida ya kazi.Vijana kwa umri huo ilitakiwa wawe makazini sio maandamano mabarabarani.
 
Kupata habari kwa wakati ni haki ya kikatiba hiyo...Hapo ndipo demokrasia inapaoanzia...
 
Kupata habari asubuhi na si jioni ni muhimu sana,tunamiss vitimbwi vya bungeni
 
Kupata habari kwa wakati ni haki ya kikatiba hiyo...Hapo ndipo demokrasia inapaoanzia...

Katiba haijataja muda iwe saa ngapi wa kupata hiyo habari WALA katiba haijasema kwa jina ni CHOMBO kipi KINACHOTAKIWA kutoa hiyo habari .

Ukienda kisheria habari zinatakiwa zitolewe na chombo husika kinachozalisha hizo habari ambacho ni bunge.Sio serikali au vyombo vya serikali.Ni sawa na habari za ujambazi ukitokea mtoa habari ni msemaji wa polisi.Huwezi kwenda shinikiza kuwa TBC atoe hizo habari nenda kazichukue wewe unayezitaka hizo habari polisi.Polisi wakikataa kukupa ndio useme wamekiuka katiba.Lakini huwezi shupalia chombo kisichozalisha hiyo habari eti kitoe.

Hivyo yeyote anayetaka habari za bunge yuko huru kuzipata bungeni wakati wowote aende akashinde huko bungeni maana huko ndiko zinakozalishwa.

Polisi wakiruhusu hayo maandamano hawatakuwa sahihi.Kama bunge limekataa kuwapa habari waandishi wa habari au TV au radio au mtu binafsi aliyeenda kuziomba waende huko wakalalamike kuwa uhuru wa habari UMEMINYWA kwa sisi tuliotaka habari za bunge kunyimwa na bunge.
 
Hujui ndio kituo pekee cha tv tunachokigharamia wa tz wote

Hizo ni assumptions katiba na sheria hazisemi.Ok andamana ukimwagiwa washawasha ukadakwa upelekwe mahakamani basi utaenda kueleza hizo assumptions zako
 
Inabidi turudi kule kwenye mila ambapo kijana kabla ya kuoa au kuloewa wazee walikuwa wanatuma asubuhi watu kutizama kama huyo kijana au msichana asubuhi hiyo kaamuka yuko shambani au yuko nyumbani.Wakikuta mida ya asubuhi yuko nyumbani wakati kijiji kizima kiko shambani wanajua huyo msichana au mvulana hastahili kuolewa wala kuoa sababu ni mvivu atakuja ua watoto kwa njaa na familia itakufa kwa njaa.

Nawapoongeza baadhi ya wachaga Mtu akitaka kuoa vile wanavyohoji una hela,una nyumba,una gari una kazi yakueleweka wewe?

Hao watakaothubutu kuandamana video zote ziwachukue vizuri tena mno mtu kama una binti yako au kijana asije oa au kuolewa na hao waandamanao kwa upuuzi kama huo na mida ya kazi.Vijana kwa umri huo ilitakiwa wawe makazini sio maandamano mabarabarani.
Hao vijana ni wachadema INA maana most of them watakuwa wachagga so pitia upya comment yako uitafakari
 
Hao vijana ni wachadema INA maana most of them watakuwa wachagga so pitia upya comment yako uitafakari
Inawezekana kweli wengi wa vijana watakaoandamana ni vijana wa wachaga lakini ndio maana wanaandamana Dar es salaam.Ingekuwa moshi wazee wangewatokea na viboko wangewacharaza bara bara.Kwamba haiwezekani kijana mida ya kazi badala ya kuwa mgombani na kwenye shamba la kahawa awe barabarani kuandamana.Hakuna maandamano wala hayajawahi tokea maandamano ya vijana kilimajaro wakati wa kazi tokea mfumo wa vyama vingi uanze miaka zaidi ya ishirini iliyopita.

Maandamano yote ya kipuuzi hufanyika kwenye mikoa ya Arusha,Dar es salaam,mwanza,Mbeya,Iringa na huko mikoa ya kusini kwenye maeneo ambako watu hawajitambui linapokuja swala la kufanya kazi.
 
NIngekuwa Magufuli ningetimus Mkurugenzi wa TBC pamoja na Waziri wake kwa kukosa namna ya kuliwezesha shirika la umma kupata mapato mengi zaidi kupitia kulirusha bunge live.

Yaani hiyo haikutakiwa hata kuwa na hasara:

1.Wangeuza matangazo kwa vituo binafsi au

2.Kutafuta wafadhili wa kukifadhili kipindi cha Bunge,

Lakini Mkurugenzi na Waziri wote wanachofikiria ni ruzuku tu,hawana mawazo mbadala,hawa wangetakiwa kuchapwa viboko halafu na kupigwa chini.
 
Nimesikitishwa na KUONA habari kwenye magazeti inayosema vijana wa chadema kuandamana kwenda kumuona rais magufuli wakidai haki ya kuangalia tv asubuhi,

Vijana na TV sasa hivi linaelekea kuwa ni tatizo kubwa la kitaifa.Vijana kutwa wanaangalia MOVIE iwe usiku iwe mchana wao ni kukodolea macho TV.Hawafanyi homework za shule hadi upige kelele.Hawalali ni TV tu.Huu utamaduni ulioibuka wa kupenda kuangalia TV hasa kwa vijana utazalisha kizazi cha vijana maskini mno.Inabidi kama nchi kuanza ku-discourage ikiwezekana TV ziwashwe masaa machache tu kwa siku halafu zizimwe na TCRA.
 
Nimesikitishwa na KUONA habari kwenye magazeti inayosema vijana wa chadema kuandamana kwenda kumuona rais magufuli wakidai haki ya kuangalia tv asubuhi ,kwa maana ya bunge,
Ni aibu kwa kizazi hili kinachojiita vichana wa kimapinduzi,

Naamini rais atasikitika na kuudhunika pamoja na mipango YAKE AMBAYO ili ifanikiwe mtaji wake mkubwa ni vijana lkn ndo wanaomba kuangalia TV asubuhi
Ni aibu,

Waambie hao vijana waende wafanye shughuli za kujitafutia kipato na si kutumika kama toilet paper, hiyo tv hana na anakaa nyumba ya giza, sasa anaomba aoneshwe tv wapi. Waache utoto hao vijana
 
Back
Top Bottom