Ukiona Rais wa nchi analindwa sana ujue Rais huyo hakuchaguliwa kwa kura halali

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,268
Ukiona Rais wa nchi analindwa kwa ulinzi wa hali ya juu sana, kwa mitutu na wanajeshi wengi, ujue huyo Rais hayupo hapo alipo kwa kura za wananchi wa Taifa hilo. Hivyo muda wote ana wasiwasi ya kuondolewa kwenye kiti alichakalia kibatili.

Ukiona Rais analazimisha kila mwananchi amuimbe yeye tu. Ujue hana uhakika na kuchaguliwa tena na Wananchi kwa awamu inayofuata, hivyo analazimika kulazimisha kila raia kumuimba yeye ili kuaminisha watu kuwa anakubalika.

Ukiona Rais wa nchi analazimisha watumishi wa Umma (wanaolipwa kodi za Wananchi) kumuimba yeye na kuwalazimisha Watumishi hao kujiunga na chama chake yeye, maana yake Rais huyu anajua kabisa kuwa hajawatimizia mahitaji muhimu watumishi hawa hivyo ili kutokumsumbua katika madai ni kuwatisha na kuwalazimisha wote wawe waimbaji wake wa mapambio.

Ukiona Rais wa nchi analazimisha kupendwa na kila mtu kwenye Taifa, ujue Rais huyo ana matatizo binafsi. Haelewi hata anachokifanya, maana anapingana na nature na ukweli wenyewe wa mambo kuwa, watu hawawezi kuwa na mtazamo sawa.

Ukiona Rais wa nchi hataki wapinzani wake wazungumze, wahoji na kuwachukulia Wapinzani wake kama "wahaini" katika Taifa, ujue Rais huyu katika Serikali aliyopo imefanya maovu mengi sana kuliko kawaida. Ikiwemo, mauaji ya raia, wizi, ubadhirifu n.k

Ukiona Rais wa nchi analazimisha watu wote kuikubali Serikali na kumkubali Rais kwa kila anachokifanya, ujue Rais huyo hajatekeleza mambo ya Wananchi badala yake ametekeleza matamanio yake na kuacha mahitaji ya Wananchi. Hivyo anawalazimisha Wananchi wakubali kuwa, matamanio ya Rais huyo ndio mahitaji ya Wananchi.

Unaweza kuongeza na wewe ndugu msomaji!!

Mohonia Joseph
 
Atakuwa Ali Bongo tu huyu.
 
Kweli...
Tatizo wako mabara yote, wakiongozwa na zile "Powerful Nations"?! Na wale ukifanikiwa kujuwa bajeti za kuwalinda ma-rais wao utakaa mdomo wazi, maana hawalingani na sifa za kuwalinda, naanza na "Trump".,,,..
 
Ukiona kuna RED BRIGADE zaidi ya 500 wanamlinda sana kiongozi mmoja tu ,ujue kuna hujuma kubwa kisiasa inapangwa
Hao wanaomlinda ndo hao hao watakaomuondoa
Screenshot_20190224-164800.png
 
Ukiona mtu anampinga RAIS kwa kila jambo

hata akiongeza madawa hospitali

hata akijenga bwawa la kuzalisha umeme ambao utakuwa bei chee

hata akitoa elimu bure

ujue mtu huyo hata akilipwa mshahara na Rais bila kufanya kazi
bado atampinga

MUSA aliwatoa wana wa israel utumwani na bado walimpinga

ole wenu kizazi cha nyoka
 
Obama alilindwa kuliko marais wote, hakuchsguliwa kwa kura? Papa anslindwa kuliko marais wote, naye hakuchaguliw Kwa kurs. Acheni kujitoa ufaham
Nani sasa analimdwa kuliko maRais wote? Obama au Papa? Tupe ufahamu.
 
Back
Top Bottom