Ukiona mwanaume hakupi hela mpaka umuombe jua kuwa wewe huna thamani

Lakin wanawake tumeumbwa kuhudumiwa ama unasemaje ,sisi tunapokea tu
Kama ww ni Mke wangu sawa kabisa. Nitakuhudumia na family nitaihudumia pia as the head of the family. Tatizo hii ya wasichana kupokea pokea hela za Wanaume imewaharibia wadada wengi sana maisha na kuua ndoto zao.
 
Sababu ni Umaskini tu wa mali na elimu. Jamani pambaneni watoto wenu wasikulie kwenye dhiki ili mzazi uweze kumhudumia mahitaji yake yote. Asijehudumiwa na mwanaume.
Me naona ni tabia tu maana mzazi/baba alisimamia shoo full maana ni wa kipato cha kati, maza nae hakikuwa kikubwa ila aliwekeza kwangu. Pamja na hayo kuomba kwa boy kama kawa..
 
Me naona ni tabia tu maana mzazi/baba alisimamia shoo full maana ni wa kipato cha kati, maza nae hakikuwa kikubwa ila aliwekeza kwangu. Pamja na hayo kuomba kwa boy kama kawa..
Tabia kama hizo zinaletwa na umaskini wa mali/ hela, umaskini wa elimu, na umaskini wa fikra. Wazazi hata wa kipato cha kati, wengi wana umaskini wa elimu ya malezi na elimu ya fikra. Anashindwa kupambana kumlea mtoto wa Kike akakua bila ya kuwa omba omba. Unakuta wazazi wenyewe wanataka mtoto awe chanzo cha kipato hata kutegemea Mahari iwasaidie. Pia wazazi wanashindwa kufundisha mtoto wa Kike kwamba kudanga ni jambo lenye hasara maishani, na pia wanashindwa kumfundisha ASIWE NA TABIA YA KUSHOW OFF. Mimi nime-date Wadada kadhaa lakini unakuta badala ya aniombe hela ya mtaji wa biashara au ya kufanyia maendeleo, ni bora aniombe hela ya kusuka nywele, hela ya kununulia iPhone, hela ya kununulia nguo nk. Wengi ndio wananunuliwa hizo iphone kwelikweli, ila shule na vyuo wanaacha, mimba wanapachikwa na wanaume wanakimbia majukumu ya malezi, future inaharibika, na hata ukimwi wanaupata.
 
kuna wanawake wengine wamezidi jamani !

kama una notebook ujumlishe pesa alizokuomba ndani ya mwezi basi ni 80% ya mshahara wako kachukua wote.

asubuhi kizinga,mchana kizinga,usiku kizinga na ukila mbususu bado kizinga.
 
Tena madem ukiomba K basi hapo utapigwa invoice mpk unakuja mmla ushatumia sana hela

Ova
 
Kumuhudumia mwanamke kwa MAHITAJI YAKE YA MSINGI ni wajibu wetu, tatizo dada zetu hawajui mahitaji yao ya msingi, kwao mpaka Iphone 13 ni hitaji la msingi.

Tatizo dada zetu hawajui tofauti kati mahitaji yao ya msingi na luxury ,wengi wao wanazani luxury ndio basics hapa sasa ndipo wanapo pishana na waoaji.
 
Ukiona mwanaume hakupi hela mpaka umuombe jua kuwa wewe huna thamani kwake, kwasababu mwanaume yoyote anapopenda sehemu neno sina hela huwa halipo kwake na hutoa hela bila kuombwa na mwanamke. Mwanaume humtoa thamani mwanamke muomba hela na humtafsiri kuwa sio mwanamke mwenye mapenzi ya kweli.

Mwanaume anaweza kutoa hela nyingi kwa mwanamke asiyemuomba hela lakini hutoa pesa kidogo kwa mwanamke muombaji hela. Tafsiri ya mwanaume kwa mwanamke asiyeomba hela huwa ndio mwanamke sahihi na mstahamilivu hata kwenye vipindi vigumu.

Hela hutakiwi kuiomba kwa mwanaume ila unatakiwa kuonesha thamani kama hela atakupa yeye mwenyewe bila kuomba, na uzuri wa mwanaume ukiijenga thamani kwake wala hana ajizi kukupa hela. Mwanamke aliefundwa na akafundika kamwe hawezi kuomba hela kwa mwanaume, matokeo ya kutokufundwa ndio hili wimbia la omba omba tunaloliona zama hizi.

Nafasi ya hela kwenye mapenzi ya dhati ni ndogo sana na sio kweli kuwa ukipendwa kwa dhati ndio hupewa hela. Hela hutumika kununua bidha au thamani ya kitu ukiona wewe muda wote ni kuomba omba hela tu jua kuwa, mbele ya mwanaume kwake hukuona kama bidhaa na sio mwanamke mwenye thamani mbele yake.

Kama baba yako mzazi kashindwa kukutatulia changamoto zako za kimaisha, vipi kijana uliyekutana nae mtandaoni akutatulie changamoto za maisha yako yote? Acha kuomba omba hela kwa mwanaume unapunguza thamani yako na mwisho wa siku utapewa talaka kweupe kwasababu wanaume hawapendi kuombwa hela.

Mm mbona sipo hivyo?nikiombwa hela sitoi na nikipata dem ambae c muomba hela sitoi kwa hiari mpk aombe...
 
Nyie wanawake akili inawazaga kupewa tu, kutafuta hamjui Aisee mna ufala mwingi sana na Kwa Hali hii tunapoelekea sijui kama watu wataendelea kuoana, Yaani mnafikia kulinganisha kupendwa na kupewa hela??? Hela za Nini? Zina uhusiano gani na hisia zenu? Kwahio mnamaanisha Wasio na hela hawastahili kupendwa, kuoa? Mnaangalia upendo wa kweli au pesa nyie? Mnatafutaga ndoa au Ajira? Mmekuja kutusaidia Nini Sasa kuzaa na kukizi haja tu za kimwili? Vipi mumeo akifa akakuachia watoto na wewe umezoea kupewa tu utafanyaje kama sio kujiuza? Jifunzeni kutafuta wenyewe bhana kupewa pesa sio kupendwa, ungekuta ndo kupendwa wale wanaojiuza ndo tuseme wanapendwa sana na Wanaume? maana wao Kila muda wanapewa pesa.
 

Umenichekesha wewe mtu..
Kuna binti akawa analia Simtafuti wakati nikimcheck tu ni mwendo wa Kusema sijalaa...mara sijui naumwa nataka nikanunue dawa akisema shida ya hela ukimpotezea ananuna Hela helaa helaaa hapana aisee hata nikionaga msg yake kujibu nlikuwa naogopa... njaa za chips haziishi
 
Kuna binti akawa analia Simtafuti wakati nikimcheck tu ni mwendo wa Kusema sijalaa...mara sijui naumwa nataka nikanunue dawa akisema shida ya hela ukimpotezea ananuna Hela helaa helaaa hapana aisee hata nikionaga msg yake kujibu nlikuwa naogopa... njaa za chips haziishi
Huyo Binti ni Mwanachuo?
 
Back
Top Bottom