Ukiona mwanaume hakupi hela mpaka umuombe jua kuwa wewe huna thamani

seifutz

Member
Jul 18, 2021
34
113
Ukiona mwanaume hakupi hela mpaka umuombe jua kuwa wewe huna thamani kwake, kwasababu mwanaume yoyote anapopenda sehemu neno sina hela huwa halipo kwake na hutoa hela bila kuombwa na mwanamke. Mwanaume humtoa thamani mwanamke muomba hela na humtafsiri kuwa sio mwanamke mwenye mapenzi ya kweli.

Mwanaume anaweza kutoa hela nyingi kwa mwanamke asiyemuomba hela lakini hutoa pesa kidogo kwa mwanamke muombaji hela. Tafsiri ya mwanaume kwa mwanamke asiyeomba hela huwa ndio mwanamke sahihi na mstahamilivu hata kwenye vipindi vigumu.

Hela hutakiwi kuiomba kwa mwanaume ila unatakiwa kuonesha thamani kama hela atakupa yeye mwenyewe bila kuomba, na uzuri wa mwanaume ukiijenga thamani kwake wala hana ajizi kukupa hela. Mwanamke aliefundwa na akafundika kamwe hawezi kuomba hela kwa mwanaume, matokeo ya kutokufundwa ndio hili wimbia la omba omba tunaloliona zama hizi.

Nafasi ya hela kwenye mapenzi ya dhati ni ndogo sana na sio kweli kuwa ukipendwa kwa dhati ndio hupewa hela. Hela hutumika kununua bidha au thamani ya kitu ukiona wewe muda wote ni kuomba omba hela tu jua kuwa, mbele ya mwanaume kwake hukuona kama bidhaa na sio mwanamke mwenye thamani mbele yake.

Kama baba yako mzazi kashindwa kukutatulia changamoto zako za kimaisha, vipi kijana uliyekutana nae mtandaoni akutatulie changamoto za maisha yako yote? Acha kuomba omba hela kwa mwanaume unapunguza thamani yako na mwisho wa siku utapewa talaka kweupe kwasababu wanaume hawapendi kuombwa hela.

pesa.jpg
 
Back
Top Bottom