Ukiona mwanamke anaikataa ndoa jua yamemfika hapa!

Habari za muda huu wakuu

Nimejiskia kushare historia yangu ya safari ya ndoa KWA UFUPI SANA wakuu ukiona mwanamke kachoka kavumilia mengi

Mimi ni mwanamke mwenye watoto3 niliolewa miaka14 iliyopita nkajaliwa watoto wa3.

Nimeishi kwenye ndoa ya mateso kwa miaka 12 hadi nilipoona inatoshaa na kuamua kukaa pembeni kujiepusha na malumbano.

Kwa kifupi tulipoingia kwenye ndoa na aliyekua mume wangu nikiwa naanza kazi wakati huo yeye alishafanya kazi sehemu tofautitofauti kwani hata kwa umri ni mkubwa kwangu amenipita miaka karibu 10

Tulipoana mwenzangu alikua anafanya kazi mbali na mimi (mikoa tofauti) na wakati huo mimi nilikua nafanya kazi ya mkataba mfupi. Tulikubaliana nisiache kazi hadi hapo nitakapopata kazi kule alipo.

Mungu mkubwa miezi miwili baada ya ndoa niliconcive nikaendelea na kazi hadi nilipojifungua.

Wakati nikiwa mjamzito nilianza kuhisi mwenzangu hajui majukumu yake kwani alikua anajua nilikua nalipwa kidogo sana tena nalipwa kwa wiki lakini hakuwahi kunisupport chochote kama mke iwe kodi, mavazi, au pesa ya kula.

Ikitokea amenipa pesa basi ujue labda laki1 au moja na nusu kwa miezi 6 tena baada ya kuomba sana na kulalamikiwa sana.

Mtoto wangu akiwa na miezi5 kazi yangu iliisha tukaamua niungane mwenzangu anakofanyia kazi. Tuliishi kwa amani, mwenzangu akiwa anaenda kazini Mimi nabaki nyumbani pia aliahidi kunitafutia kazi.

Basi wakati huo nikiwa mama wa nyumbani mtoto anaweza akawa anaumwa mwenzangu anaenda pharmacy ananunua dawa ananiambia nimpe yeye anaenda kazini.

Nilikuwa nabaki nyumbani nina chakula tuu ila senti tano sina. Kuna kipindi nilibaki na mtoto akazidiwa sina hata vocha ya kupiga sim.

Nilihisi kumpoteza mwanangu nikaomba wasamaria wema msaada mwanangu akatibiwa nikiahidi nitawalipa pesa zao. Jioni aliporudi mwenzaàngu nilimwambia alinyamaza nikampa namba za walionisaidia na kiasi walichonipa.

Hakuonyesha Kujali ila baada ya siku 2 aliwatafuta na kuwapa pesa yao. HAPO KENGELE ZA HOFU ZILIANZA KULIA KICHWANI NIKAONA ILI NIISHI MIMI NA MWANANGU LAZIMA NIFANYE KAZI.

Kama mwanamke yoyote nilimweshim sana mume wangu sikutaka kabisa kumuudhi nilikua naongea nae kwa busara kuhusu maisha na majukumu yetu kama wazazi ila hakuwahi kunipa majibu ya wasiwasi niliokua nao wala kuonyesha njia ya kupata suluhu. Niliumia na kuogopa sana na moyoni nilijua lazima nifanye kazi sana.

Basi nikampigia kaka yangu aliyekua ananitaftia vibarua, nikamwambia kaka huku sina kazi mwaka sasa,nikamwomba anitumie msg kuna kazi (japo haikuwepo) ili niweze kuomba nauli na kurudi sehemu ambayo ni kama nyumbani na ni rahisi hata kupata msaada

Nilirudi nikatafuta kazi nikapata na maisha yakaendelea.

Mwenzangu hakuwahi badilikaaa, kila kitu nilikua najifanyia mwenyewe, kodi, matibabu, kula, kuvaa na bills zote. Ikitokea amekuja basi ataweka laki mezani itatumika na kwisha kabla hata ya yeye kuondoka..lakini hasemi kitu achilia mbali mimi kumwambia nimekopa hapa na pale kujikimu. Kuna wakati niliomba wakubwa zake wamshauri lakini hakuna lililobadilika.

Miaka 5 baada ya ndoa nilikuja kugundua na wanawake kibao Kati yao akiwa girlfriend wake wa shuleni ambae alikua mke wa mtu ambae katika mawasliano yao ya email waliapa kutokuachana.NILIUMIA SANAAA NIKASEMA BASI NDOA STAKI TENA MAANA NATESEKA BILA SABABU ZA MSINGI.

Aliomba msamaha sikuweza kumsikiliza wazazi wakaanza kusuluhisha na baada ya kama miezi8 yaliisha tukaanza upya. Tuliishi hivyo siku zikawa zinasonga sikuskia tena habari za wanawake ila huduma ya familia haikuwepo bila ugomvi na ukitokea ametoa labda ada ya mtoto kama ni 1M atatoa laki4 na akishaoa hiyo chakula, matibabu, kodi, kuvaa sio juu yake🤗 uksema umjaribu kwa kumshauri kumhamishia mtoto shule za serikali anakataa

Miaka mi3 iliyopita hali ilizidi kuzorota, watoto 3 mzigo akanizidi, nikamwambia lazima kukaa na kujadili mstakabali wa familia hapo kwa Mara ya kwanza alinitukana na kuniambia sitakiwi kumsemesha chochote kwani kila ninachomwambia anakijua......nilishangaa nikasema majukumu tuu yanatufikisha hapa! Wacha ninyamaze.

Baada ya siku chache nikagundua kumbe ana wanawake wanamsumbua hata yule old girlfriend bado yuko nae

Hapa ndipo nilifanya maamuzi kwamba mimi na yeye basi. Tuna watoto wazuri na nawapenda sana nadhani hata yeye anawapenda japo siwezi kumsemea....

Sikuona sababu ya mimi kuendelea kuishi na mtu ambaye

1.Hanijali

2.Hanipi support yoyote na zaidi

3.Ananisaliti kitu ambacho ni hatari magonjwa haya mengi tusijeacha watoto kizembe

Aanakuja akiomba msamaha nimemsamehe kabisa lakini siwezi kurudiana nae

Nilichoka roho, akili na mwili hata akioa leo aoe tuu

Nilichoka kufanya majukumu ya mama na ya baba na kusalitiwa juu

Hapa ndipo nawashangaa Dada zangu, unakubalije kuzaa watoto wa 3 na mpuuzi kama huyu? Ukishazaa mmoja unaleta figisu Usizae tena!

Watu hawabadiliki
 
Pole sana dada, hawa watu ni wps sn kubdilika, kumuona tu kwa nje huwez jua km ni mtu sahihi au lah..anaweza akabadilikia kwnye ndoa au kwenye uchumba, na lait km wngebdilikia kwny uchumba bs ata ucngekbl kuolewa nae....tafkr km unaona atabdilika bx msamehe tu lkn km moyo wako bd unasema kuwa c mtu sahihi... Bx leave him...live ur life...believe that u can live without a man, because you have ur job and u can manage the neeeds of ur children... Even though its not enough salary.
 
Hapa ndipo nawashangaa Dada zangu, unakubalije kuzaa watoto wa 3 na mpuuzi kama huyu? Ukishazaa mmoja unaleta figisu Usizae tena!

Watu hawabadiliki

Kweli watu hawabadiliki mkuu, na mimi nimeshaelewa sasa nimemove on....
Siwezi kuishi nae tena ila sijutii kuwa na hawa watoto... Nawapenda sana wanangu na namshukuru Mungu kwa hilo
 
Wanawake wengi wanagugumia tu na hizi ndoa, basi tu ndio vile tena!!!
Una uhakika gani kuwa wanaume wengi hawagugumii?
Haya mambo wanaume huwa hatuongei.
Na stress zetu wakati mwingine huwa zinamaliziwa kwa wanawake wa mtaani tu.
 
Nakubaliana na wewe lakini kuna mambo mengi yanayofanya mtu akute anavumilia
1.Ni kuamini kwamba tumetoka kwenye makuzi tofauti nimpe mwenzangu muda wa kujifunza
2.Upendo unaokua nao unaweza kukufanya uamue kuvumilia
3.Watu waliokuzunguka kama wazazi, watoto na ndugu

Ila mwisho wa yote kama mtu hataki kubadilika ipo siku utachoka tuu
Mimi naona kama uliwahi kufunga ndoa kabla hujamuelewa vizuri tabia yake, na kilichokufanya umuamini labda ni huo utofauti mkubwa wa umri na kama ulimuelewa labda ulijua mkifunga ndoa atabadilika, hilo ni kosa kubwa tabia ya mtu haibadiliki, naimani umejifunza kitu kikubwa jali wanao
 
Pole sana ndugu yangu, tatizo haya mambo tukisema sana tunaambiwa tunataka usawa.
 
Back
Top Bottom